settings icon
share icon
Swali

Je, ni imani gani za Yesu pekee / Je, kuna umoja wa Pentekoste?

Jibu


Shirika la "Yesu peke yake", pia linajulikana kama Pentekoste ya umoja au teolojia ya umoja, inafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, lakini inapinga umoja katika Uungu. Kwa maneno mengine, teolojia ya umoja haitambu watu tofauti wa Uungu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ina aina mbalimbali-wengine wanaona Yesu Kristo kama Mungu mmoja, ambaye wakati mwingine anajionyesha Mwenyewe kama Baba au Roho Mtakatifu. Mafundisho ya msingi ya umoja wa Pentekoste/ Yesu peke yake ni kwamba Yesu ni Baba na Yesu ni Roho. Kuna Mungu mmoja ambaye anajidhihirisha mwenyewe kwa njia tofauti.

Mafundisho haya ya Wapentekoste ya Yesu pekee yamekuwa nasi kwa karne nyingi, kwa namna moja au nyingine, kama modalizimu au (modalism). Modalizimu au (modalism) inafundisha kwamba Mungu anajidhihikwrisha kwa aina tofauti au njia tofauti-wakati mwingine kama Baba, wakati mwingine kama Mwana, na wakati mwingine kama Roho Mtakatifu. Lakini vifungu kama Mathayo 3: 16-17, ambapo Watu wawili au watatu wa Uungu wanapinga mtazamo wa kawaida. Mfumo wa modalizimu au (modalism) ulihukumiwa kama mfumo potovu mapema karne ya pili A.D. Kanisa la kwanza lilipigana sana na maoni kwamba Mungu ni mtu wa pekee ambaye alifanya kazi kwa aina tofauti kwa nyakati tofauti. Wanasema kutoka kwa Maandiko kuwa umoja wa Mungu ni dhahiri kwa kuwa zaidi ya Mtu mmoja wa Uungu mara nyingi huonekana wakati mmoja, na mara nyingi huzungumana na kila mmoja (mifano: Mwanzo 1:26; 3:22; 11: 7; Zaburi 2: 7, 104: 30; 110: 1; Mathayo 28:19; Yohana 14:16). Pentekoste ya umoja / fundisho la Yesu pekee sio la kibiblia.

Dhana ya umoja wa Uungu, kwa upande mwingine, iko katika Maandiko. Sio wazo ambalo linaeleweka kwa urahisi na akili ya kibinadamu. Na kwa sababu mtu anapenda kila kitu kuwa na maana katika theolojia yake, mfumo kama vile wa Yesu pekee-bila kutaja Mashahidi wa Yehova-mara kwa mara kutokea kujaribu kueleza hali ya Mungu. Bila shaka, hii haiwezi kufanyika bila kufanya vurugu kwa maandiko ya kibiblia. Wakristo wamekubalii kwamba asili ya Mungu haiwezi ckuelezwa kupitia mapungufu tunayopenda kumvika. Tunamwamini Mungu wakati anasema, "Maana mawazo yangu sio mawazo yako, wala njia zako si njia zangu, asema BWANA, kama mbinguni ilivyo juu kuliko dunia, vile vile njia zangu ni za juu kuliko njia zako na mawazo ni ya juu kuliko mawazo yako "(Isaya 55: 8-9). Ikiwa hatuwezi kuelewa mawazo na njia zake, tunakubali kwamba hatuwezi kuelewa kikamilifu asili yake .

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni imani gani za Yesu pekee / Je, kuna umoja wa Pentekoste?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries