settings icon
share icon
Swali

Ikiwa Yesu ni fidia yetu, ni kwa nini alikufa wakati wa Pasaka badala ya siku ya maridhio?

Jibu


Kila mojawapo ya dhabihu ya Agano la Kale iliashiria Kristo. Dhabihu ya Pasaka ilikuwa mfano wa Bwana Yesu Kristo kama Kondoo wa Mungu. Kondoo wa pasaka alifaa kuwa wa kiume, bila mawaa au dosari yoyote, na hakuna mfupa wowote ungevunjika. Yesu alitimiza taswira hii kikamilifu. Kama vile Waisraeli walitia damu ya dhabihu kwa imani, vile vile tunatumia damu ya Kristo isiyo na doa katika milingoti ya nyoyo zetu. Katika njia hizi zote, "Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo" (1 Wakorintho 5:7).

Upishi wakati mwingine huibuka kwamba dhabihu ya pasaka haikuzingatiwa kuwa fidia; badala yake, fidia ilitolewa kwa Wayahudi kupitia siku ya upatanisho (Yom Kippur). Kwa hivyo, Yesu, amabye aliuawa siku ya Pasaka na ambaye pia anaitwa "Pasaka yetu katika Agano Jypia, hangeweza kuwa fidia ya dhambi.

Kuna njia mbili za kukabiliana na ubishi huu. Kwanza ni kuonyesha jinsi Yesu alitimiza ishara ya siku ya fidia. Yesu alizibeba dhambi zetu kwa mwili wake mwenyewe (1Petro 2:24) na kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu (Waebrania 2:9). Kwa kufanya hivyo, alitoa dhabihu bora kuliko ile ya siku ya fidia ya Agano la Kale- ni bora kwa sababu dhabihu ya Kristo ilikuwa ya milele. Ilikuwa ya hiari, na haikufunika dhambi tu bali iliiondoa kabisa (Waebrania 9:8-14).

Pili, kabiliana nalo ni kuonyesha kuwa kuwa utamaduni wa Kiyahudi ulitazamia dhabihu ya Pasaka kuwa fidia; hiyo ni kusema, mbele za Mungu kijikondoo kiliondoa dhambi. Kijikondoo cha Pasaka chini ya ghadhabu ya Mungu iliyomwagika, na hivyo kufunika dhambi za yule aliyekuwa akitoa dhabihu. Haya ndiyo Rashi msemi mkuu wa Kiyahudi aliyeheshimika enzi za kale aliyasema: "ninaona damu ya Pasaka na kukupatanisha… kwa upole niakuhurumia kwa sababu ya damu ya Pasaka na damu ya tohara, na kuridhia nyoyo zenu (Kutoka 15, 35b, 35a).

Wakati wa pigo la kumi na la mwisho kule Misri, dhabihu ya Pasaka kihalisi iliokoa mtu binafsi kutoka kifo (Kutoka 12:23). Kwa misingi ya toleo la ukombozi ya damu ya Pasaka kifungua mimba aliishi. Pia Rashi anachangia: "ni kana kwamba mfalme alisema kwa mwanawe: 'jua kwamba ninawashitaki watu kwa makosa ya jinai na kuwahukumu. Na kwa hivyo nipe zawadi ndiposa iwapo umeletwa mbele yangu na mashtaka niweze kutupilia mbali makosa hayo.' Kwa hivyo Mungu akasema: 'sasa nimesikitika na adhabu ya kifo, lakini nitakwambia vile nina huruma juu yako kwa sababu ya damu ya Pasaka na damu ya kutahiriwa nitakufidia'" (Kutoka 15. 12, kuhusu Kutoka 12.10).

Kijikondoo cha Pasaka kilileta fidia kwa nyumba ya Myahudi katika usiku ule wa ishara ya hukumu na ukombozi. Mwalimu Ibrahimu Ibn Ezra pia anaunganisha Pasaka na fidia: "Alama ya damu ilinuiwa kuwa fidia kwa wale waliokuwa ndani ya nyumba ambao walishiriki pasaka ya dhabihu na pia ilikuwa ishara ya ule malaika wa uharibifu kupita nyumba hiyo" (Soncino Chumash, pg. 388).

Wakati Yohana mbatizaji alimwona Yesu, alielekeza kidole kwake na kusema, "Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu" (Yohana 1:29). Yesu ndiye "mwana-kondoo wa Pasaka" sababu alikimya mbele ya waliomshitaki (Isaya 53:7) na kifo chake kiliibeba ghadhabu ya Mungu, na kuifadhi maisha ya wengi waliomwamini, na kuwapa uhuru wafungwa wa dhambi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa Yesu ni fidia yetu, ni kwa nini alikufa wakati wa Pasaka badala ya siku ya maridhio?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries