settings icon
share icon
Swali

Kuna umuhimu gani wa Yesu kula na wenye dhambi?

Jibu


Pindi tu baada ya kumwita Mathayo amfuate, Yesu alikula chakula na "watoza ushuru wengi na wenye dhambi" katika nyumba ya Mathayo (Marko 2:15). Mathayo alikuwa mtoza ushuru na "wenye dhambi" hawa walikuwa wendani wake na marafiki ambao walichukua muda wao kukaa na Yesu. Mathayo alitaka kuleta wendani wake wa karibu kwa Yesu. Waandishi ana Mafarisayo ambao walidharau watoza ushuru walilalamika, lakini hatua ya Yesu ya kutumia muda wake kutangamana na wenye dhambi ulikuwa kadri na dhamira yake ya kuwatafuta na kuwakomboa waliopotea (Luka 19:10).

Katika siku za Yesu, walimu na viongozi wengine wa kiroho walifurahia heshima na kuhenziwa katika jamii ya Wayahudi. Karibu kila mtu waliwatizamia Mafarisayo. Walikuwa wafuasi wakuu wa Sheria, walikuwa walezi wa mila, na walikuwa mfano wa utauwa. Katika msimamo wao sugu, waliwatenga wale walioonekana kuwa wenye "dhambi"- wale ambao hawakufuata mfumo wao wa masharti. Mafarisayo na viongozi wengine wa dini wa siku za Yesu hakika hakuna vile wangehusiana na watoza ushuru, ambao walijulikana sana kwa wizi wa fedha zilizowekwa amana kwao, na uhusiano wao na Warumi ambao waliochukiwa.

Yesu alichagua kulan a wenye dhambi kwa sababu walihitaji kujua toba na msamaha zilikuwa zinapatikana. Huduma ya Yesu ilipozidi kukua, hivyo ndivyo umaarufu wake miongoni mwa watu waliodharauliwa katika jamii. Katika wakati mmoja Mathayo alikuwa mwendani wa karibu sana wake, kwa asili Yesu alikuwa karibu sana na wale wa kiwango cha chini/maskini katika jamii. Kutumia muda wake Pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi ilikuwa kawaida, kwa kuwa Yesu "hakuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi" (Marko 2:17). Ikiwa Yesu angeweza kuwafikia waliopotea lazima alikuwa na njia ya kuwasiliano nao. Alienda mahali kulikuwa na hitaji kwa sababu "Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi" (Luka 5:31).

Kukaa katika karamu iliyoandaliwa na Mathayo, Yesu alivunja itikadi za kijamii na kukishifu udini wa Mafarisayo na mfumo wa kuafikia utakatifu. Ukweli kwamba Yesu alikula na wenye dhambi unaonyesha kuwa aliangazia utamaduni bali alijali miyo ya watu. Walakini Mafarisayo walidharau watu kwa sababu ya matendo yao ya zamani, Yesu aliona hitaji lao la kiroho.

Wakati wote wa huduma ya Yesu, aliwafikia wale wote walimhitaji. Aliwasiliana na mwanamke wa Samaria katika kisima-hii ikiwashangaza mitume wake (4:27). Katika Luka 7, alimsamehe mwanamke aliyepatika akifanya usherati, na katika Marko 7 alimsaidia mwanamke Msirofoinike, aliguza mtu mwenye ukoma katika Luka 5, na katika Luka 19 aliingia kwa nyumba ya Zakayo na kula naye. Tena na tena aliwaguza wasioguzika na kupenda wasio pendeka.

Yesu alikuja kuokoa wenye dhambi. Mila, itikadi za tamaduni, na kukunjamana kwa wachache hakujalishi wakati nafsi inaingia katika mahali inakusudiwa. "Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye" (Yohana 3:17).

Yesu aliwaona watu binafsi, sio vitambulisho vyao tu. Alikuwa na huruma na kutafuta kukidi mahitaji yaliyoletwa kwake. Kwa kushiriki neno la Mungu, Yesu alikula na wenye dhambi na alitumia wakati wake na wao. Kuona haya yote bila shaka wenye dhambi wote walitiwa moyo wa kumjua vyema. Walimtambua Yesu kama mtu mwadilifu, mtu wa Mungu- miujiza aliyoifanya ilikuwa ushuhuda kwa hilo- na waliona huruma yake na uaminifu wake.

Yesu hakuruhusu hadhi ya kijamii au desturi ya kitamaduni kuongoza uhusiano wake na watu. Kama Mchungaji Mwema, alitafuta kondoo waliopotea mahali popote walikuwa wamepotelea. Wakati Mathayo alitayarisha karamu ya jioni, Yesu alikubali mwaliko. Ulikuwa nafasi mwafaka ya kushiriki Habari njema ya ufalme na wale walihitaji kuusikia sana (ona Mathayo 4:23). Alilaumiwa kwa sababu ya hatua yake na wanasheria wenye haki nafsia wa siku hizo, lakini lawama hizo hazikumzuia.

Tofauti na Mafarisayo, Yesu hakuitaji watu kubadilika kabla waje kwake. Aliwatafuta, akakutana nao mahali walikuwa, na akawapa neema katika hali zao. Mabadiliko huja kwa wale wanaomkubali Kristo, lakini lazima badiliko haya yawe ya ndani nje. Fadhili za Mungu huwaongoza wenye dhambi kwa toba (Warumi 2:4), na Yesu alikuwa mwingi wa fadhili.

Yesu alituonyesha kuwa hatupaswi kuruhusu desturi za kitamaduni kuamua ni nani tutamhubiria neno. Wagonjwa wanahitaji daktarin. Kondoo waliopotea wanahitaji mchungaji. Je tunamwomba Bwana wa mavuno kutuma wafanyi kazi shambani (Luka 10:2)? Je! Tuko tayari kwenda sisi wenyewe?

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna umuhimu gani wa Yesu kula na wenye dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries