settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu alikuwa na nywele refu?

Jibu


Michoro mingi huonesha picha za Yesu ni za mwanaume wa asili ya kiarabu akiwa na macho ya rangi ya samawati na nywele ndevu yenye rangi ya kunde. Ni muhimu kuelewa kwamba michoro hii ya kawaida huenda ikawa sio kile Yesu alionekana. Yesu alikuwa kabila ya Kiyahudi, na hivyo kuna uwezekano kuwa alikuwa na ngozi nyeupe ya kunde, macho ya samawati, na nywele ya kunde au nyeusi. Yese angeonekana kama mtu halisi kutoka Mashariki ya kati anavyoonekana. Hakuna mahali Biblia inatupa maelezo ya Yesu, kwa hiyo mtu yeyote asije na funzo lolote kuhusu vile Yesu alikuwa anaonekana. Na hatimaye, lazima tuelewe kwamba haijalilishi vile alikuwa anaonekana. Ikiwa ingejalisha, basi Biblia ingekuwa na maelezo ya kimwili.

Ikiwa rangi ya ngozi yake, macho na nywele vile tunaiona katika michoro si sahihi, sembuze urefu wa nywele Yake? Yesu kuoneshwa kuwa na nywele refu pia kunaeza kuwa si sahihi? Tena, si rahisi kukanuni, jinsi Biblia haisemi chochote kuhusu urefu wa nywele yake. Lakini Yesu alionekana kama mwanaume wa asili ya Mashariki ya Kati ya karne ya kwanza AD/BK (Baada ya Yesu kuzaliwa), kuna uwezekano kuwa michoro ya usanii si sahihi katika urefu wa nywele yake pia. Michoro mingi ya usanii humwonyesha Yesu akiwa na nywele ionekenayo kama ya kike. Huku hakukuwa na sheria yeyote ya Kiyahudi, wanaume wa Kiyahudi kitamaduni walikuwa na nywele fupi kuliko wanawake wa Kiyahudi.

Kunalo changio la Paulo katika 1 Wakorintho 11:14, "Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?" Urefu wa nywele ya Yesu ungekuwa chochote kile kilifaa kitamaduni kwa mwanaume. Nywele ya Yesu ingeonekana ya kiume. Sasa, chenye hiyo inamaanisha hasa ni jambo la kujadiliwa. Je! nywele yake ingekuwa unaguza mabega? Pengine. Je! kuna uwezekano kuwa Yesu alikuwa na mtindo wa nywele ilikatwa kwa mashine au alikuwa na nywele fupi? Huenda haikuwa. La msingi ni kuwa ingeonekana kama ya kiume. Na hiyo inaonekana kuwa hoja ya Paulo katika 1 Wakorintho 11:3-15. nywele ya mwanaume lazima ionekane ya kiume. Nywele ya mwanaume lazima ionekane ya kike. Chenye hii inamaanisha inaweza kuwa tofauti kutoka tamaduni hadi tamaduni, lakini la msingi husalia kuwa hivyo bila kusingatia utamaduni.

Kwa hivyo, Yesu alikuwa na nywele refu? Jibu linategemea kile kinachomaanishwa kuwa nywele "refu." Je! kuna uwezekano kuwa ilikuwa refu kuliko urefu wa nywele mwanaume wa asili ya siku hizi? Naam. Je! kuna uwezekano iliku refu kiwango ilionekana kuwa ya kike? La. Lakini kama vile rangi ya Ngozi, nywele, na nywele, urefu wa nywele hatimaye havijalishi. Sio vya maana tena kwa Yeye kuwa mkombozi wa ulimwengu (Yohana 1:29) na njia pekee iendayo mbinguni (Yohana 14:6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu alikuwa na nywele refu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries