settings icon
share icon
Swali

Yesu alikuwa msalabani kwa muda gani?

Jibu


Yesu alikuwa msalabani kwa takribani masaa sita. "Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na waalimu wa sheria na wazee walimdhihaki wakisema, Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Ati yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini. Alimtumainia Mungu na kusema ati yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka" (Mathayo 27:41-43). Kusulubiwa ulikuwa mtindo wa Ufalme wa Kirumi ulitumia hapo kale ili kutekeleza adhabu ya kifo kwa wale waliopatina na makosa ya jinai. Sulubu ilitengewa watumwa, wageni, waasi na wale waliopatikana na hatia ya uhalifu mbaya zaidi.

Wayahudi wanaoamini utawala wa Mungu, ndio wamwangamize Yesu na kudumisha mamlaka yao, walipanga njama ya kushawishi utawala wa Kirumi kwamba Yesu lazima auwawe (Marko 14:1; angalia Yohana 19:1215). Viongozi wa Kiyahudi walimsuta Yesu kwa kuchochea uasi na kujitangaza kuwa Mfalme. Shitaka hili la uasi ndio maana Yesu alimalizia kuangikwa msalaba wa Kirumi badala ya kupigwa mawe hadi kufa, namna ya jadi ya mauaji ya Wayahudi.

Kusulubiwa haikusudiwa kuua pekee bali kuwashawishi wenginge wasifanye makosa kama hayo. Waadhiriwa wa sulubu walikuwa wahaibishwe, na mara nyingi waliachwa uchi wakiwa wametundikwa mtini. Msalaba ulibeba fedheha na sheria ya Kiyahudi ilisema kuwa ulileta laana (Wagalatia 3:13; 5:11). Sulubu ilikuwa ya maumivu ya kufa kwa sababu ilikuwa njia ya kufa pole pole na ya machungu. Kulingana na hali, watu wengine wangeishi kwa siku baada ya kutundikwa msalabani.

Kujibu swali la ni muda ambao Yesu alikuwa msalabani ni gumu mno kwa sababu mifumo miwili ya kutunza wakati imetumika katika Injili. Mathayo, Marko na Luka wanatumia mfumo wa Kiyahudi wa kutunza wakati. Yohana anatumia mfumo wa Kirumi. Kwa kutumia mfumo wa Kiyahudi, Marko anasema, "Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini. Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha" (Marko 15:24-25). Kulingana na vifungu hivi, Kristo alianza kusulubiwa 9:00 A.M.

Pia kwa kutumia mfumo wa Kiyahudi wa kuhesabu wakati, Mathayo anasema kuwa, "Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa" (Mathayo 27:50). Baada ya hayo askari wa Kirumi alihakikisha kifo chake (Yohana 19:34), na mwili wa Yesu uliondolewa. Yesu alikuwa amekwisha kuwa msalabani trakribani toka 9:00 A.M. hadi 3:00 P.M., jumla ya masaa sita.

Yohana anaongeza kusimulia habari yote kuwa kujaribiwa kwa Yesu mbele ya Pontio Piloto kulikuwa kunaendelea kulingana na mfumo wa Kirumi wa wakati, "yapata saa sita" (Yohana 19:14). Jinsi Warumi walianza kuhesabu wakati wao usiku wa manane, "saa sita" zitaanza 6:00 A.M.

Kwa hiyo kwa kutumi mfumo wa Kirumi:
"saa sita"= 6:00 A.M. Yesu alihukumiwa na Pilato.

Kwa kutumi mfumo wa Kiyahudi
"saa ya tatu"= 9:00 A. M. Usulubisho ulianza,
"saa ya sita" = 12:00 P.M. (adhuhuri). Giza likaanza.
"saa ya tisa" = 3:00 P. M. Yesu alikufa.

Kwa kuyaweka yote pamoja, majaribio ya Yesu karibu saa 6:00 A. M. Kusulubiwa kwake kukaanza takribani saa tatu baadaye, na akafa baada ya saa sita baadaye.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alikuwa msalabani kwa muda gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries