settings icon
share icon
Swali

Msingi wa tabia ya mafundisho ya Yesu ni upi?

Jibu


Tabia msingi ya mafundisho ya Yesu ni muhimu huku yakiwa rahisi hata kwa mtoto kuelewa; ni ya kiroho huku yakiwa ya manufaa katika maisha ya kila siku. Kwa msingi, Yesu alifunza kuwa alikuwa utimizo wa unabii wa Musa, kuwa Mungu anahitaji zaidi ya utiifu wa nje wa sharia, kwamba wokovu huwajia wale wanamwamini Kristo, na kuwa hukumu inakuja kwa wasioamini na wasiotubu.

Yesu Kristo alifunza kuwa kila mtu anahitaji wokovu na kuwa mahali mtu yupo maishani haiwezi toa mwelekeo wa dhamani yake kwa Mungu; Kristo alikuja kuwaokoa watu kutoka pande zote za maisha. Wala dhambi ya kale ya mtu ina uwezo wa kupata msamaha, na Yesu anawahimiza wafuasi wake kuwasamehe wengine vile yeye amewasemehe (Mathayo 18:21-35; Luka 7:47). Zakayo alikuwa mtoza ushuru tajiri sana ambaye bila shaka alikuwa anadharauliwa na kila mmoja katika mji wake (Luka 19:7), lakini alichukua muda wake na kukaa nay eye. Yesu akasema, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii" (Luka 19:9). Sababu? Zakayo alikuwa amemwamini Yesu, ikidhihirishwa katika toba yake ya dhambi za zamani na akaapa kuishi maisha ya hisani (Luka 19:8). "Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea," Yesu akawaambia wale walio mtizama kwa makini (Luka 19:10). Hakujali mtu aliye potea ni nani, tajiri au maskini, mume au mke, fukara au mfalme. Kila mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:3).

Yesu pia alifundisha kuwa njia inayoenda kwa Mungu in kwa Imani, na sio kwa matendo mema. Alisifu Imani (Luka 7:9) na akawapa changamoto wale waliotegemea matendo yao (Mathayo 7:22-28). Tajiri mdogo wakati mmoja alimuuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?" (Marko 10:18). Kristo hakuwa anakana uungu wake au uzuri wake mwenyewe, bali alijua huyu mtu tajiri mdogo hakuwa anamtambua Yesu kama Masiha. Katika swali lake, Yesu alikuwa anaweka wazi kuwa chochote huyu mtu alifikiria kumfanya mtu "mwema" kilikuwa uongo, kwa sababu hamna mtu anaweza kitu ili awe mwema kiwango cha kurithi maisha ya milele (Yohana 14:6). Viongozi wa dini wa enzi hizo za Kristo walikuwa na mtizamo sawia na huyu tajiri mdogo, wakifunza kuwa kuitunza sheria ya Mungu ingemfanya mtu kukubalika mbele za Mungu. Kunao watu wengi hii leo ambao hufikiri kuwa maisha yao "mazuri" na matendo "mazuri" yatatosha kuwafikisha mbinguni.

Yesu alimwambia huyu mtu tajiri kuwa lazima auze mali yake yote na kumfuata Yeye (Marko 10:21). Yesu alisema sio kwa sababu uhisani unamfanya mtu kuwa haki, bali ni kwa sababu alikwisha mjua huyu mtu kuwa pesa ndizo zilikuwa mungu wake. Huyu mtu tajiri alidhani alikuwa akiitunza sheria; tamaa ilikuwa jambo hangeweza kuacha. Aligeuka nyuma na kumwacha Yesu kwa huzuni sababu, "kwa maana alikuwa na mali nyingi" (Marko 10:22). Kristo alifundisha kuwa Yeye pekee ndiye chanzo cha maisha ya milele. Ikiwa mtu anataka kurithi maisha ya milele. Ikiwa mtu anataka kurithi maisha ya milele, lazima amfuate na kumwabudu Kristo pekee (Yohana 6:45-51; 8:31; 10:27; 15:4, 14).

Katika kiini cha mafundisho ya Yesu ni habari njema ya kuja kwa Ufalame wa Mungu. Ufalme umetajwa zaidi ya mara hamsini katika vitabu vya Injili. Wingi wa mifano ya Yesu ilikuwa juu ya Ufalme (Mathayo 13:3-9; 13:24-30; 13:31-32; 13:33). Kwa kweli, Yesu alisema, alitumwa kwa makusudi ya kuhubiri kuja kwa Ufalme (Luka 4:43).

Yesu alifunza kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa umeanza duniani kupitia huduma yake. Dhihirisho lilikuwa wazi: katika utimilifu wa unabii, vipofu waliona, wafu wakafufuliwa, na dhambi zikasamehewa. Lakini Yesu pia alifunza kwamba kunayo sehemu ya Ufalme ambayo haijakuja (Luka 9:27). Ufalme wake unaenea na siku moja utaonekana wazi (Luka 13:18-21). Kwa kile kijulikanacho kama "sala ya Bwana," Kristo alisema kuwa waombe ufalme wa Mungu uje (Mathayo 6:10). Yesu aliwafunza wanafunzi wake kukumbuka wito wao: wao ni vyombo vya neema ya Mungu wanaposhiriki habari njema ya kuja kwa Kristo. Watu wanapozidi kuja kwa Kristo, ndipo ufalame unazidi kuonekana katika ulimwengu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Msingi wa tabia ya mafundisho ya Yesu ni upi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries