settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu atakuja mawinguni (Ufunuo 1:7)?

Jibu


Ufunuo 1:7 yasema, "Tazama! Anakuja na mawingu, na kila jicho litamwona, hata wale waliomchoma; na makabila yote duniani yataomboleza kwa sababu yake. Naam, ndivyo itakavyokuwa! Amen." Aya hii inaleta pamoja vifungu vingine viwili: Mathayo 26:64, ambamo kwamba Yesu anaambia baraza kuu kuwa watamwona Mwana "akija mawinguni"; na Zakaria 12:10 ambayo inasema kuwa wakaaji wa Yerusalem wataomboleza wakati watakapomwona "yule waliyemchoma."

Wengine wamejaribu kufananisha Ufunuo 1: 7 kwa kuipa maana nyingi za mifano kama vile "mawingu." Lakini hakuna haja ya kutafuta maana zilizofichika hapa, kwa maana kifungu kinamaanisha kile kinachosema, kama vile vifungu hivyo viwili inavyovinukuu. Hakuna kitu kingine cha kusema juu ya kauli kwamba "Anakuja na mawingu." Inamaanisha tu kwamba Yesu atawatokea watu wote anapokuja duniani kutoka mbinguni.

Baada ya Yesu kuwapa mitume wake Utume Mkuu, "akachukuliwa juu mbinguni mbele ya macho yao na wingu likampokea wasimwone tena" (Matendo 1:9). Wanafunzi walipokuwa wakisimama hapo, wakimwangalia Bwana, malaika wawili walitokea na kuwaambia, "Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni (

Matendo 1:11). Maweingu yametajwa katika kupaa kwake, ni pia mawingu yametajwa katika kurudi kwake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu atakuja mawinguni (Ufunuo 1:7)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries