settings icon
share icon
Swali

Yesu yuko katika Agano la Kale?

Jibu


Yesu anaonekana mara nyingi katika Agano la Kale-sio kwa jina lake, na sio katika mfano ule ule vile tunamwona katika Agano Jipya, bali fauka ya hayo yupo. Mada kuu ya Biblia nzima ni Kristo.

Yesu mwenyewe alithibitisha hoja kuwa Yeye alikuwa katika Agano la Kale. Katika Yohana 5:46 aliwaeleza baadhi ya viongozi wa dini ambao walikuwa wamemuuliza swali kwamba Agano la Kale lilikuwa linamsungumzia: "Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamimi mimi, kwa sababu yeye aliandika habari zangu." Kulingana na Yesu, kazi ya Mungu kwa mwanadamu tangu wakati uanze yote iliwaelekeza Kwake. Wakati mwingine ambao Yesu alionyesha kuwa alikuwepo wakati wa Agano la Kale ilikuwa wakati wa ufufuo wake. Yesu alikuwa anatembea na wanafunzi wake wawili, na "Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Musa hadi manabii wote" (Luka 24:27). Awali, kabla ya ufufuo wake, Yesu alikuwa ameonyesha kutoka Isaya 53:12 na kusema, "Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake" (Luka 22:37).

Kwa hesabu kidogo, zaidi ya nabii 300 ya Agano la Kale inalenga Yesu Kristo na zilitimizwa kwa maisha yake ulimwenguni. Hii ni pamoja na unabii wa kuzaliwa kwake wa kipekee (Isaya 7:14), huduma yake duniani (Isaya 61:1), na hata njia atakayo kufa (Zaburi 22). Yesu aliihangaza dini ambayo ilikuwa imeanzishwa wakati alisimama katika sinagogi ya Nazarethi na kusoma kutoka Isaya 61, akihitimiza na maelezo haya: "Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu" (Luka 4:18-21).

Namna nyingine Yesu kuwepo katika Agano la Kale ni kwa njia ya maono-kutwaa mwili kwa Mwana wa Mungu mbeleni. Agano la Kale hutumia neno malaika wa Bwana sawia na Bwana katika kurejelea ziara hizi. Mwonekano wa kwanza wa Kristo unaonekana katika Mwanzo 18:1-33 wakati Bwana alimwonekania Ibrahimu katika mfano wa binadamu. Mkutano huo wa wazi na uungu umetapakaa katika Agano la Kale (Mwanzo 16:7-14; 22:11-18; Waamuzi 5:23; 2 Wafalme 19:35; Danieli 3:25).

Lakini kunazo njia zingine za ndani ambazo kwazo Yesu anapatika katika Agano la Kale. Hizi zinaonekana kwa zile tunaita "mifano." Mfano ni mtu au kitu katika Agano la Kale ambacho kinaashiria mtu au kitu katika Agano Jipya. Kwa mfano, Musa anaweza kuonwa kama mfano wa Kristo. Kama Yesu, kuzaliwa kwake Musa kulikuwa kwa maana, alikabiliana na nguvu za giza za siku hizo alivyowaongoza watu wake kupata uhuru kupitia ukombozi wa kimiujiza. Maisha ya Yusufu ni kielezo kingine cha maisha ya Kristo.

Matukio mengi ya kihistoria ya Agano la Kale huwa na kauli mbili ya ishara ya kile ambacho Mungu atatenda siku za usoni, kupitia kwa Kristo. Kwa mfano, Mungu alimwita Ibrahimu akamtoe mwanawe Isaka kama dhabihu. Ibrahimu aliyasema maneno haya ya kiunabii kwa mjibu wa swali la Isaka kuhusu kondoo wa dhabihu: "Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu" (Mwanzo 22:8). Mungu akapeana kondoo wa kuchinjwa badala ya Isaka, ikiashiria chenye atafanya maelfu ya miaka baadaye juu ya mlima huo huo wakati Mwanawe alitolewa kama dhabihu kwa niapa yetu (Mathayo 27:33). Matukio yanayoisunguka kutolewa dhabihu kwa Isaka basi huwa mfano kwetu wa dhabihu ya Kristo.

Yesu alireelea tukio lingine katika historia ya Waisraeli kama kivuli cha kusulubiwa kwake. Katika jangwa, watu waliomfuata Musa walifanya dhambi, na Mungu akamtuma nyoka kwao kuwauma. Watu walikuwa wanakufa, na wakamsihi Musa kuwasaidia. Mungu akwamwambia Musa kutengeza nyoka ya shaba na kuipachika mtini. Wale wote waliomtizama yule nyoka wa shaba walipona (Hesabu 21:4-19). Yesu alitaja tukio hili katika Yohana 3:14-15: "Kama vile Mose alivyomwinua juu nyoka wa shaba kule jangwani, naye Mwana wa Mtu atainuliwa juu vivyo hivyo, 15ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele."

Ubunifu wa Mungu wa hema ya ibada ni njia nyingine ambayo Yesu anaonekena katika Agano la Kale. Madhabahu katika katika ua la ndani inaashiria haja ya dhabihu ya Yesu kwa ondoleo la dhambi zetu. Birikia linamweka Yesu kuonekana kuwa mtoa maji ya uzima (Yohana 4:14). Ndani mwa patakatifu pa patakatifu, taa iliashiria Yesu kama mwangaza wa dunia (Yohana 9:5). Meza ya mikate inaashiria Yesu kama mkate wa uzima (Yohana 6:35). Katika madhabahu ya ufumba yanaonekena kama Yesu mwombezi wetu mbinguni, anayeendelea kamwe kutuombea (Warumi 8:34; Waebrania 7:25). Kulinga na Waebrania 10:20, pasia ya sanduku la agano ni taswira ya mwili wa nyama wa Yesu.

Mwana wa Mungu huyoko katika Agano Jipya pekee; Yesu ako pia katika Agano la Kale. Yesu ndiye Masiaha ambaye Mungu alituahidi. Toka kwa kuzaliwa kwake kwa ubikra katika Bethlehemu (Isaya 7:14; Luka 1:35; Mika 5:2), ingawa safari kwenda Mistri (Hosea 11:1; Mathayo 2:14-15), hadi kwa huduma yake uponyaji na tumaini (Mwanzo 3:15; 1Yohana 3:8), hadi kufufuka kwake (Zaburi 16:9-11; Matendo 2:31), Yesu Kristo ndiye mada kuu ya Agano la Kale na Jipya. Inaweza semekana kuwa Yesu ndiye sababu ya Biblia kuwepo. Yeye ni Neno lilo hai. Biblia yote ni nguzo ambayo hutelekezea kwa na fasi ya Mungu ya upatanishi, tumaini la kusamehe na maisha ya miele kupitia kwa Yesu Kristo aliye Bwana wetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu yuko katika Agano la Kale?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries