settings icon
share icon
Swali

Kusudi la Yesu ni gani la kutuombea Mbinguni?

Jibu


Kwa kusungumzia juu ya Yesu mwandishi wa Waebrania anasema, "Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee" (Waebrania 7:25). Aya hii (na zinginezo kama hii) zinatuambia kwamba ingawa kazi ya Kristo ya kupata wokovu kwa wateule ilikamilika msalabani, na kuthibitishwa kwa kilio chake "yote yameisha" (Yohana 19:30), utunzaji wa wake kwa wana wake waliokobomolewa haungekamilika.

Yesu hakuenda mbinguni baada ya huduma yake huku duniani na "kuchukua mda wa mapumziko" kutokana na jukumu lake kama mchungaji wa watu wake. "Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake" (Warumi 5:10, msisitizo umeongezwa). Ikiwa hata baada ya wakati alinyenyekea, akadharauliwa, akiwa ana karibia kufa, n ahata akiwa mfu, bado alikuwa na uwezo wa kutimiza kazi kuu ya kutuunganisha na Mungu, ni mangapi zaidi tunaweza tarajia kuwa ataweza kutulinda sasa kuwa yuu hai, ameinuliwa, na mkombozi mshindi, alifufuliwa na anahoji kwa niapa yetu mbele za kiti cha enzi (Warumi 8:34). Ni wazi, Yesu bado anahusika katika maisha yetu na kwa niapa yetu mbinguni.

Baada ya Yesu kupaa mbinguni aliketi katika mkono wa kuume wa Mungu Baba (Matendo 1:9); Wakolosai 3:1), alirudi kwa utukufu aliokuwa nao mbeleni kabla ya kutwaa mwili (Yohana 17:5) ili kuendele na majukumu yake ya mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana-jukumu lake la milele kama mtu wa pili katika utatau. Huku dunia hii ya zamani ikiendelea kuletwa kwa Kristo, Yesu ndiye wakili wa Wakristo, kumaanisha Yeye ndiye mtetezi wetu mkuu. Hili ndilo jukumu la uombezi ambalo analitekeleza kwa sasa kwa niapa ya wale walio wake (1Yohana 2:1). Kila wakati Yesu anaombea kesi zetu mbele za Baba, kama wakili mtetezi kwa niapa yetu.

Yesu anatuombea huku Shetani (ambaye jina lake linamaanisha "mshtaki") anatutuhumia, huku akitaja dhambi zetu na udhaifu wetu mbele za Mungu, kama vile alivyofanya wakati wa Ayubu (Ayubu 1:6-12). Lakini mashataka yalianguka kwa masikio ziwi, kwa sababu kazi ya Yesu msalabani ililipa deni ya dhambi zetu kikamilifu; kwa hivyo, Mungu anaona haki kamilifu ya Yesu ndani ya wato wake. Wakati yesu alikufa msalabani, haki Yake (utakatifu kamilifu) ilihesabiwa kwetu, huku dhambi zetu zilihesabiwa kwake katika kifo chake. Huu ni ubadilisho mkuu ambao Paulo anasungumzia katika 2Wakorintho 5:21. Daima hiyo ilifutilia mbali hali yetu ya dhambi mbele za Mungu, na hivyo Mungu anaweza kutukubali bila mawaa mbele zake.

Kwa kumalizia, ni muhimu kuelewa kwamba Yesu ndiye mpatanishi wa kibinadamu kati ya Mung una mwanadamu. Hamna mtu mwingine- sio Mariamu, sio Wakristo wowote watakatifu wa kale-ana uwezo wa kutuombea mbele za kiti cha Mwenyezi. Hamna malaika aliye na nafasi hiyo. Kristo pekee ndiye Mungu-mwanadamu, na anapatanisha na kuhoji kati ya Mungu na mwanadamu. "Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu" (1Timothy 2:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kusudi la Yesu ni gani la kutuombea Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries