settings icon
share icon
Swali

Yesu alijua wakati gani kwamba alikuwa Mungu?

Jibu


Yesu daima alikuwa Mungu. Kutoka milele yeye amekuwa Mtu wa pili wa Utatu, na wakati wote Yeye atakuwa. Swali la wakati, baada ya kutwaa mwili, Yesu mwanadamu alijua kwamba alikuwa Mungu ni jambo la kuvutia, lakini halijazungumziwa katika Maandiko. Tunajua kwamba, kama mtu mzima, Yesu alitambua kikamilifu Yeye ni nani, akijidhihirisha hivi: "Kweli nawaambieni,. . . kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko!" (Yohana 8:58). Na alipoomba, "Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla kuumbwa ulimwengu" (Yohana 17: 5).

Pia inaonekana kuwa, kama mtoto, Yesu alikwisha jua tayari asili na kazi yake. Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na mbili, Yusufu na Maria walichukua familia hiyo kwenda Yerusalemu. Wakiwa safarini kurudi nyumbani, walikuwa na wasiwasi juu Yesu alikuwa amepotea kutoka kwa msafara wao. Walirudi Yerusalemu na kumkuta Yesu "hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali" (Luka 2:46). Mama yake alimwuliza Yesu kwa nini alitoweka na kuwafanya kuhangaika hivyo. Yesu alijibu kwa kuwauliza, "Kwa nini mlinitafuta? . . . . inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?" (Mstari wa 49). Yusufu na Mariamu hawakuelewa maneno ya Yesu (mstari wa 50). Wale wote waliokuwa karibu naye hawakuelewa, inaonekana kwamba Yesu akiwa wa umri mdogo sana, alijua kwamba alikuwa Mwana wa Mungu na kwamba Baba alikuwa amekwisha tia wakufu kazi aliyopaswa kufanya.

Baada ya tukio hilo hekalu, Luka anasema, "Naye Yesu akendelea kukua kaitika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu" (Luka 2:52). Ikiwa katika wakati huu Yesu akatika uzoefu wake wa kibinadamu alijua kila kitu, hakuitajika "kukua kwa hekima." Tunasisitiza kwamba hii ilikuwa ni uzoefu wa Yesu. Yesu hakuacha kuwa Mungu, lakini katika mambo mengine alifunua uungu wake kwa mujibu wa mapenzi ya Baba. Kwa hiyo, Mwana alijishughulisha na ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii na kiroho. Mwana wa Mungu alijiweka kwa hiari katika nafasi ya haja ya kuimarisha ujuzi kama mwanadamu.

Ni wakati gani Yesu alijua kwamba alikuwa Mungu? Kutoka mtazamo wa mbinguni, Mwana alijua kutoka milele Yeye alikuwa nini na kazi Yake ya kidunia ilikuwa gani. Kutoka kwa mtazamo wa kidunia, Yesu aliyetwaa mwili alijua ufahamu huo wakati wa mapema katika Maisha yake ya utoto. Ni lini wakati huo ulikuwa, hatuwezi kujua kwa hakika.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alijua wakati gani kwamba alikuwa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries