settings icon
share icon
Swali

Alikuwa ni Yesu Kristo ndoa?

Jibu


Yesu Kristo ni dhahiri kwamba hakuwa na bibi. Kuna hadithi maarufu leo hii ambazo husema kwamba Kristo amemwoa Maria Magdalene. Hadithi hizi ni za uongo kabisa na hazina msingi kiteolojia, kihistoria, au kibiblia. Huku baadhi ya injili hutaja kuwa Yesu alikuwa na uhusiano wa karibu na Maria Magdalene, hakuna hata moja yao hasa inasema kwamba Yesu alikuwa amemwoa Maria Magdalene, au kuwa na uhusino wowote wa kimapenzi pamoja naye. Ukaribu unaokisiwa ni pale Yesu alimbusu Maria Magdalene, ambayo kwa urahisi inaweza kuwa “kumbukumbu ya busu ya kirafiki” Zaidi ya hayo, hata kama injili ya Aginostiki moja kwa moja ilisema kwamba Yesu alikuwa amemwoa na Maria Magdalene, hawatakua na mamlaka, kwa vile taarifa za Injili ya Agnostiki zimethibitika kuwa za udanganyifu zikinuia kujenga mtazamo Kiagnostiki kumhusu Yesu.

Kama Yesu alikuwa ameoa, Biblia ingekuwa imetuambia hivyo, au kungekuwa na baadhi ya taarifa zisizo na utata na ukweli kwa hoja hiyo. Maandiko kamwe hayawezi kimya kabisa juu ya suala hilo muhimu. Biblia inamtaja mama yake Yesu, baba mlezi, ndugu na dada zake wa kambo. Ni kwa nini iache kutaja ukweli kwamba Yesu alikuwa na mke? Wale wanaoamini / kufundisha kwamba Yesu alikuwa ameoa wanafanya hivyo katika jaribio la “kumfanya Yesu kuwa mwanadamu.” ili wamfanye kuwa kama mtu wa kawaida, hasa kama kila mtu mwingine. Watu kwa ufupi hawataki kuamini kwamba Yesu alikuwa Mungu katika mwili (Yohana 1:1, 14; 10:30). Kwa hivyo, wao hutunga na kuamini hadithi kuhusu Yesu kuwa na mke na watoto, na kuwa kama mtu wa kawaida.

Swali la pili litakuwa, “Je, Yesu Kristo angekuwa ameoa? Hakuna dhambi kwa kuoa. Hamna dhambi juu ya kuwa na uhusiano wa kingono katika ndoa. Kwa hivyo, naam, Yesu angeweza kuwa ameoa na bado kuwa mwanakondoo Mungu asiye na hatia na Mkombozi wa ulimwengu. Wakati huo huo, hakuna sababu ya kibiblia ya Yesu kuoa. Hiyo sio hoja katika mjadala huu. Wale wanaoamini Yesu alikuwa ameolewa hawaamini kwamba alikuwa na dhambi, au kwamba yeye ni Masihi. Kuoa na kupata watoto sio sababu kuu ambayo Mungu alimtuma Yesu. Marko 10:45 inatuambia ni kwa nini Yesu alikuja, “ Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Alikuwa ni Yesu Kristo ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries