settings icon
share icon
Swali

Yesu alikuwa wa taifa gani?

Jibu


Ijapokuwa Bibilia haijaelezea maumbile yake Yesu kama mwanadamu, tunajua kwamba Yeye alizaliwa katika Bethlehemu na alilelewa katika mji wa Nazareti huko Galilaya kaskazini mwa Israeli (Mathayo 2:1; Luka 2:4-7; 4:16; Yohana 7:42). Kwa hivyo, Yesu Kristo alikuwa mtu wa Mashariki ya kati, Myahudi wa Kiebrania.

Tunapofuata ukoo wa Kristo tunagundua kwamba Yesu alikuwa Myahudi wa kabila nyingi. Ukoo wake una silika kutoka kwa taifa na tamaduni tofauti ikiwepo Wamoabu kupitia Ruthu na Mkanaani kupitia Rahabu.

Picha za zamani za Yesu zinaonyesha wazi kuwa Yeye alikuwa na rangi nyeusi. Lakini kufikia mapema Zama za Kati, wasanii walianza kumchora kwa maumbile ya uzungu kama vile Ngozi nyeupe, ndevu, na nywele ndefu zenye hudhurungi. Walakini, kama mtu wa Mahariki ya Kati, hakika Yesu angekuwa na nywele nyeusi, na ngozi ya mzeituni mweusi na silika za Kiyahudi. Na kama mwana wa seremala, pengine ngozi yake ilikuwa imegeuka nyekundu kwa sababu ya jua.

Katika historia na katika kila tamaduni, watu wamekuwa na mazoea ya kumuelezea Yesu kama mtu wa kabila lao. Labda hii ni mojawapo ya sababu kwa nini Mungu hakutaja rangi ya ngozi ya Yesu katika Neno lake. Biblia inafundisha kwamba Mungu aliumba mataifa mbali mbali ya ulimwengu na akafanya kila moja kuwa ya kipekee (Matendo ya Mitume 17:26-27). Bwana wetu, Yesu Kristo, alikuja ili ahusiane na watu wa kila taifa (Mathayo 28:19). Mungu Baba anapenda watu wote na alituma Mwanaye kuokoa ulimwengu (Yohana 3:16-17; Ufunuo 5:9).

La muhimu zaidi kuliko kubaini kabila la Kristo ni kuelewa utume Wake- ambao ulijumuisha kufanyika sehemu ya wanadamu (Yohana 1:14; Wafilipi 2:6-7). Yesu alikuja kuwaunganisha watu katika imani na upendo (Yohana 13:34; Wakolosai 1:4) katika ulimwengu ambapo rangi ya ngozi mara nyingi hutenganisha watu. Mungu anataka tukubaliane katika tofauti zetu (Wagalatia 5:22).

Rangi ya ngozi na urithi wa kitaifa huwekwa pembeni wakati washiriki wa mwili wa Kristo hujitambulisha kama watoto wa Mungu ambao wana uraia wa mbinguni (Wafilipi 3:20). Basi tunaweza kukubaliana na mtume Paulo, ambaye alisema, "Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:28; pia tazama Waefeso 2).

Pengine swali bora la kuuliza kuliko kuuliza "Yesu alikuwa wa taifa gani?" ni "Yesu alikuja kwa ajili ya taifa gani?" Jibu ni kwamba yeye alikuja kwa ajili ya mataifa yote.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alikuwa wa taifa gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries