settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu alikuwa nabii?

Jibu


Manabii wameoneshwa wakiwa na majukumu mengi katika Biblia. Kwanza, manabii ni wasemaji wa Mungu. Wakati watu wa Israeli walimuuliza Samueli mfalme, Mungu alimwambia Samueli, "Sikiliza kila kitu ambacho watu wanakuambia; maana hawajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme juu yao" (1Samueli 8:7). Samueli aliwajibika katika kupeana Neno la Mungu kwa watu wa Israeli, na na Mungu anakauli kuwa, Yeye ndiye chanzo cha mamlaka na maneno ya Samueli. Kwa hivyo, nabii alikuwa mwakilishi wa Mungu.

Vifungu vingi katika Agano la Kale vina taarifa kama vile "neno la Mungu lilimjia," ikionyesha kwamba chanzo cha ujumbe ilikuwa ni Mungu na sio nabii (kwa mfano 2 Samueli 7:4; 2 Wafalme 20:4; Yeremia 1:4; Ezekieli 3:16; na aya funguzi za Hosea, Yoeli, Mika, Yona, na Zefania). Vile vile, Yesu alifunza ujumbe wa mbinguni: "Mafundisho ninayofundisha is yangu, bali ni yake yeye aliyenituma" (Yohana 7:16). Pia alisema kwamba "ninasema yale tu Baba alinifundisha" (Yohana 8:28). Katika ombi la Yesu la Hukuani, anasema, "nimewapa ule ujumbe ulionipa" (Yohana 17:8). Kwa hivyo, kwa wazi Yesu alitimiza jukumu la nabii, kwa kuwa alikuwa msemaji wa Mungu.

Jukumu la pili la msingi la nabii katika Biblia ni kile kwa kawaida watu wanafikiria juu yake wakati wanaposikia neno unabii, na hiyo ni kutabiri au ubashiri wa matukio yajayo kwa ufunuo wa kiungu. Utabiri, ingiwa sio kazi ya kawaida ya manabii, ni aina nyingine ya jukumu la kimsingi la manabii. Katika kuonge kwa niaba ya Mungu, wakati mwingine ujumbe utakuwa ubashiri wa yatakayo kuja. Yesu alitabiri yatakoyotokea wakati aliwaambia wanafunzi wake "imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka" (Mathayo 16:21). Unabii huu umerekodiwa ukiwa umetimilika katika simulizi ya vitabu vyote vinne vya Injili (Mathayo 27-28; Marko 15-16; Luka 22-24; na Yohana 18-20). Yesu pia alitabiri kuwa, muda mfupi baada yake kupaa mbinguni, wanafunzi watopekea nguvu baada ya Roho Mtakatifu kuwashukia (Matendo 1:8). Matendo 2 imerekodi kutimia kwa unabii: mitume walipokea Roho Mtakatifu na wakanena katika lugha ambazo hawakuzijua kwa kiutangaza injili takribani katika lugha kumi na tano za makundi tofauti yaliyowakilishwa kule Yerusalem siku ya Pentekote. Kwa hiyo, ni wazi Yesu alitimiza jukumu la nabii, kwa kuwa alisungumza kiunabii.

Kazi ya tatu ya baadhi ya manabii ikuwa kuponya na miujiza. Musa alifanya ishara nyingi, ikiwa ni pamoja na kutawanya Bhari ya Shamu (Kutoka 14:21-22). Elia alifanya muujiza wakati aliomba moto kutoka mbinguni kuichoma dhabihu (1 Wafalme 18:36-38). Elisha alifanya muujiza wakati alikifanya kichwa cha shoka kuelea juu maji (2Wafalme 6:6). Simulizi zote nne za Injili zimemrekodi Yesu akifanya ishara na uponyaji (mfano, Mathayo 8:14-15; Marko 1:40-45; Luka 8:42-48; na Yohana 6:16-21).

Cheo "nabii" limetumika mara nyingi sana katika vitabu vya Injili wakati watu wengine wanamrejelea Yesu (Mathayo 21:11; Luka 7:16; Yohana 4:19).

Mungu alikuwa amemwambia Musa kwamba siku moja atamtuma nabii mwingine kwa Israeli, "nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru" (Kumbukumbu 18:18). Yesu alikuwa nabii ambaye alitimiza unabii huo (ona Matendo 3:22; 7:37). Yesu anatimiza masharti yote ya kuwa nabii katika cheo, maneno na matendo. Yeye ndiye nabii wa mwisho kwa sababu Yeye ndiye Neno la Mungu (Yohana 1:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu alikuwa nabii?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries