settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu alikuwa mweusi?

Jibu


Kuna baadhi ya makundi ambayo yanajihusisha na fugufugu/wanaharakati wa "Waibrania Weusi", ambao hubishi kwa dhati kwamba Yesu alikuwa mweusi/Mwafrika katika rangi yake ya Ngozi/sura. Huku hili likienda moja kwa moja na kinyume na Biblia ambayo inatangaza Uyahudi waYesu, kumaanisha kuna uwezekano alikuwa na rangi ya ngozi ya udhurungi weupe, na hatimaye mjadala/hoja hiyo inakosea. Je! inajalisha kwetu kujua rangi ya ngozi ya Yesu-iwe alikuwa mweusi, kinjano, samawati au mweupe? Ingawa hii inaweza kuwa suala tatanishi kwa wengine, ukweli ni kwamba hatujui rangi ngozi ya Yesu ilikuwa. Huku kukiwa na marejeleo kadha wa kadha ya Yesu kuwa na uridhi wa Kiyahudi, biblia inatoa elezo dogo sana kama kunalo la jinsi Yesu angeonekana.

Ni nabii Isaya ambaye anatupa elezo nzuri sana la jinsi Yesus alionekana: "Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani" (Isaya 53:2). Ikiwa rangi ya ngozi ya Yesu na sura vilikuwa muhimu, basi Mungu angetuambia juu yake. Fauka ya hayo, kudhania kuwa Yesu ni wa rangi moja au nyingine ni kukisia Habari ambayo haipatikani katika Maandiko. Dhanio kama hilo ni ubatili usio na maana kabisa (1Timotheo 1:4; Tito 3:9). Jambo ni kuwa haijalishi katika mpango wote wa ukombozi ni rangi gani Yesu alikuwa nayo (Waefeso 1:7; Wakolosai 1:14).

Kwa hiyo, tunapaswa kujishughulisha na nini tunaposungumzia juu ya Yesu? Petro anatuambia, "Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe" (1 Petro 1:3). Kwa maneno mengine, Kristo ametuitia maisha ya utukufu na maadili bora, hapa duniani na mbinguni. Tunapaswa kuishi maisha safi na ya haki kwa utukufu wake. Ujumbe wa kifungu hiki uu wazi: ni kwa utukufu wake na wema ambao utavutia mwanadamu maisha na wema ndani Yake. Hii haina uhusiano wowote na jinsi anavyoonekana au rangi ya ngozi yake.

Petro pia anatuambia kuwa Mungu "Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye" (Matendo 10:34-35). Wakati Yesu anatuita twenende kwa kila taifa na kufundisha injili (Mathayo 28:18-20), anatuambia kwamba hakuna tamaduni au vizuizi vya kirangi, kwamba sisi wote tu kitu kimoja katika Kristo Yesu. Paulo anakariri hili katika barua yake kwa makanisa ya Galatia: "Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:28). Rangi ya ngozi ya Mwokozi wetu haina haina athari yoyote katika usimulizi wetu wa injili yake (Warumi 1:16). mitume wa kanisa ya karne ya kwanza walibadili ili kufaa tamaduni za nchi za kigeni, lakini hawakufanya hivyo kwa gharama ya uaminifu wao kwa sheria ya Kristo (1Wakorintho 9:19-23).

Huenda Paulo alibadilisha mtindo wake wa kufundisha pindi aliingia utamaduni mpya au nchi ya kigeni, kamwe hakuwai badilisha ujumbe wake. Aliendelea kuhubiri mambo yale yale alikuwa amekwisha fundisha, mbali na rangi ya ngozi ya wasikizi wake. Cha muhimu ni kwamba waliipokea habari njema ya Kristo. Ukweli ni kwamba ujumbe wa injili ya Krist ulifanya kazi enzi hizo na injili hiyo itafanya kazi siku hizi! Bado unafikia zile roho za wale walio na shauku ya kumjua Mungu, hata kama wao ni weusi, weupe, wa rangi ya njano, au samawati. Sio rangi ya ngozi ya Yesu au rangi ya ngozi ya jirani yetu yenye inaamua mile yetu. Lakini chenye hujalisha ni "hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu alikuwa mweusi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries