settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu alikuwa mweupe?

Jibu


Katika sanaa nyingi za Magharibi, Yesu anaoneshwa kuwa na ngozi nyeupe na nywele iliyo na ueupe. Hivo ndivyo Yesu alionekana? Kama sivyo, ni kwa nini mara nying hudhihirishwa hivyo?

Kwanza, ni vyema kukumbuka kwamba hakuna mahali Biblia inapeana maelezo ya jinsi Yesu anaonekana. Biblia haisemi lolote kuhusu urefu wa Yesu, uzito, rangi ya ngozi, rangi ya nywele au macho. Mambo kama hayo siyo ya maana kwa kuelewa Yesu ni nani. Biblia inayokaribi kwa kuelezea jinsi Yesu anaonekana ni mchoro usio na simulizi yote ya jinsi Yesu anaonekana ni Isaya 53:2: "Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani" (Isaya 53:2). Kwa kweli Isaray 53:2 inasema kuwa Yesu alikuwa anaonekana kikawaida. Maelezo ya Yesu aliyetukuka kuwa na nywele nyeupe na ngozi ya shaba nyeusi katika Ufunuo 1:14-15 haifai kueleweka kihalisi isipokuwa wewe unaamini kuwa Yesu ana nyota saba katika mkono wake wa kulia, kisu mdomoni mwake, na uso ungaao kama jua (Ufunuo 1:16).

Kulingana na Biblia Yesu alikuwa Myahudi ambaye pia anajulikana kama Mwibrania au Mwisraeli. Yesu aliishi Mashariki ya Kati na alikuwa wa asili ya taifa la Shem. Kwa sababu ya hiyo, huenda rangi ya Ngozi yake ilikuwa na samawati epesi, anayolinganishwa na ile ya Ulaya/uzunguni, ngozi kama hizo ni chache katika sehemu hiyo ya ulimwengu. Je! Yesu alikuwa mzungu? Jibu ni kwamba kuna uwezekano hakuwa mzungu.

Kwa hivyo, ikiwa kuna uwezeano kuwa Yesu hakuwa mzungu/mweupe, ni kwa nini mara nyingi anaonyeshwa kuwa mzungu? Ukichunguza michoro ya usanii ya Yesu kutoka nchi nyingi, utapata kuwa, mara nyingi inamwonyesha Yesu njia mkabala na jinsi watu wanavyoonekana katika utamaduni huo. Uzunguni/Ulaya humwonyesha Yesu kama mzungu. Waafrika wanamchora Yesu na asili ya Kiafrika. Wa Asia wanamwelezea Yesu kwa namna ya Kiasia. Watu hupendelea kumwonyesha Yesu jinsi na namna wanavyoonekana, au hasa kama watu wanaowajua.

Ni makosa kufanya hivyo. Haina haja. Maadamu vile tusiporuhusu mfano wa Yesu tunaoupenda kuwa sanamu, hakuna kitatika Biblia kinachozungumzia dhidi ya kumwonesha Yesu kuonekana namna fulani. Yesu ndiye Mwokozi wa "mataifa yote" (Mathayo 28:19; Wagalatia 3:8). haijalishi rangi ya ngozi mtu, uraia, kabila, na utaifa, anaweza kupokea msamha wa dhambi na upatanisho na Mungu kupitia kwa Kristo aliyesulubiwa na kufufuka. Upendo wa Yesu unapita rangi ya ngozi. Kwa kutokuwa na maelezo ya mwili ya Yesu, watu kwa kawaida hufikiria Mwana wa Adamu kuwa kama wao.

Kwa hivyo, hatupaswi kuifanya kuwa kanuni taswira ya Yesu tunayoipendelea. Ukweli kwamba hamna mahali Biblia inatoa maelezo ya kimwili inafaa kuwa onyo dhidi ya ufidhuli na majivuno juu ya suala hili. Jinsi Yesu anavyoonekana haijalishi. Mwonekano wake wa kimwili hauna umuhimu wowote wa Yeyd kuwa Mwokozi wa ulimwengu (Yohana 3:16).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu alikuwa mweupe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries