settings icon
share icon
Swali

Wakristo wanapaswa kujibuje wakati mtu anadai kuwa Yesu amezaliwa tena?

Jibu


Kila mara nyingi, mtu anadai kuwa amefanyika kuwa kama Yesu. Baadhi ya watu hawa hata wanaonekana sawa na tafsiri maarufu za kisanii za Yesu. Kwa muda mwingine, hawa "wafinyika Yesu" wanapata wafuasi wengi sana. Kwa sababu mbalimbali, wao wote hatimaye huonyeshwa jinsi walivyo wadanganyifu na waharibifu. Ni ngumu kudumisha mwonekano wa maisha kamilifu. Wakristo, na wasio Wakristo, wanapaswa kuitikiaje wakati mtu anadai kuwa Yesu ambaye amezaliwa tena?

Jambo la kwanza kumbuka ni kuzaliwa tena sio dhana ya Kibiblia. Biblia inafundisha kwamba kila mtu hufa na kisha anafikishwa katika hukumu (Waebrania 9:27). Wazo la mzunguko ambalo watu wamefungwa nalo linahusisha kifo na kuzaliwa upya hutoka kwa Uhindu na Ubuddha. Sio, wala halijawahi kuwa mafundisho ya Kikristo / ya kibiblia. Ujio wa pili wa Yesu Kristo hautakuwa usaliwa upya wa Yesu tena.

Ujio wa pili wa Yesu Kristo umeelezwa kwa undani sana katika Ufunuo 19: 11-16. Sio kuzaliwa tena kwa Yesu. Ni Yesu Mwenyewe atarudi katika utukufu wake wote. Katika ujio wa pili, Yesu "hazaliwi tena" ulimwenguni; Haji kama mtoto kama alivyofanya wakati wa kuja kwake kwa kwanza. Badala yake, Yesu anarudi katika mwili ule ule wa utukufu ambaye aliondoka nao (Matendo 1:11). Biblia pia inafundisha kwamba kurudi kwa Yesu kutatokea wakati wa mshtuko mkubwa ulimwenguni pote. Kuja kwake kwa pili kutatokea mwishoni mwa dhiki kuu. Kurudi kwa Yesu kutakuwa kama kwa shujaa mwenye ushindi, si kama Mfalme wa Amani.

Yesu alituonya kwamba kutakuwa na mesihi wengi wa uongo. Hiyo ni mtu yeyote anayedai kuwa Yesu ambaye amezaliwa tena-masihi wa uwongo. Katika Luka 17: 23-24, Yesu alisema, " Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate; kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake." Ona pia Mathayo 24: 23-25. Yesu anasema kwamba kurudi kwake kwa pili kutakuwa dhahiri. Hakutakuwa na shaka. Kutakuwa dhahiri kama mpigo wa radi katika giza la usiku.

Mtu yeyote anayesema kuwa yeye ni Yesu ambaye amefufuliwa tena ni, mchoraji, nabii wa uongo, na masi wa uwongo. Msisikilize na msiwape pesa. Kuzaliwa upya ni dhana isiyo ya kibiblia kabisa. Kuja kwa pili kwa Yesu, kama ilivyoelezwa katika Biblia, kwa namna yoyote hakuna vile kunafanana na kuzaliwa upya. Yesu alizaliwa mara moja; Alikufa mara moja; na sasa Yeye ndiye Mfufuo ambaye "yu hai milele na milele!" (Ufunuo 1:18).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wakristo wanapaswa kujibuje wakati mtu anadai kuwa Yesu amezaliwa tena?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries