settings icon
share icon
Swali

Yesu alikuwa na umri wa miaka ngapi wakati alikufa?

Jibu


Biblia haisemi umri wa Yesu wakati alikufa. Fauka ya hayo, Biblia haitoi tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu au tarehe ya kufa kwake. Hii huifanya ngumu kuainisha umuri halisi wa Yesu wakati alikufa.

Kwa kufuatisha historia iliyonakiliwa katika Agano Jipya, hasa Injili ya Luka, na kuilinganisha na historia ya Kirumi, tunahitimisha kuwa Yesu alizaliwa kati ya karne ya 6 na 4 BC. Ulinganisho mwingine hutuelekeza kuamini kuwa Yesu huendea alisulubiwa mwaka wa AD 30, ingawa pia kuna uwezekano kuwa Yesu alisulubiwa mwaka wa AD 33. Kwa mjibu wa tarehe hizo za kuzaliwa na kufa kwa Yesu, Yesu alikuwa na umri wa miaka ya thelathini-pengine kati ya 33 na 39- wakati alikufa.

Wengi wa wachanganuzi wa Biblia na wanahistoria huegemea ukadri wa miaka ya chini. Kwa hivyo, huku ikiwa ni ngumu kuhalisi au kununisha jibu kwa swali "Yesu alikuwa na umri gani wakati alikufa?" alikuwa "takribani miaka 34."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alikuwa na umri wa miaka ngapi wakati alikufa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries