settings icon
share icon
Swali

Je! Akika Yesu aliishi? Kunao ushahidi wa kale/historia kuwa Yesu aliishi?

Jibu


Kawaida wakati swali hili linapoulizwa, mtu anayeuliza anahitimisha swali la “nche ya Bibilia” hatulikubalini na hili wazo kuwa Bibilia haiwezi chukuliwa kuwa na ushahidi wa kutosha kuwa Yesu aliishi. Agano Jipya liko na ma mia ya marejeo ya Yesu Kristo. Kunao wale wanaiweka kuwa Injili katika karne ya pili baada yaYesu kuzaliwa, zaidi ya miaka 100 baada ya kifo cha Yesu. Hata kama ilikuwa hivi (wazo ambalo twalipinga), kwa ushahidi wa kale, uandishi chini ya miaka 200 baada ya matukio kutokea inachukuliwa kuwa ushahidi wa kutosha kuaminika. Zaidi ya hayo wengi wa wachanganusi wa Bibilia wa mbeleni (wakristo na wasio wakristo) unaipa barua za Paulo (baadhi yao si zote) kwa kweli ziliandikwa katikati mwaka wa karne ya kwanza baada ya Yesu kuzaliwa (A.D)., chini ya miaka 40 baada ya kifo cha Yesu. Kulingana na uandishi wa kale, huu ni utibitisho wa wa kutosha wa kuwepo kwa mtu anayeitwa Yesu katika Israeli katika karne ya kwanza baada ya Yesu kuzaliwa (A.D).

Ni vizuri pia kutambua kwamba mwaka wa 70 baada ya Yesu kazaliwa (A.D) Warumi walifamia na kuiharibu Yerusalemu na sehemu nyingi za Israeli, wakiwachinja wenyeji. Mji wote ulichomwa kabisa. Tusishangashwe kama ushaidi wa kuwepo kwa Yesu uliharibiwa. Wengi wa waliomshuhudia Yesu pengine waliuwawa. Hali hii ilidunisha wingi wa shuhuda zinazoishi za waliomshuhudia Yesu.

Kwa kuangalia huduma ya Yesu ambayo ilikuwa kwa maeneo madogo sana yasiyo na maana sana katika sehemu ya ufalme wa Rumi, cha kushangasha kiwango cha habari kuhusu Yesu chaweza kutolewa kutoka kwa historia za kawaida. Baadhi ya ushahidi wa kihistoria za ulimwengu wa kale, umetajwa kutokuwa na dhana ya Mungu “Wakristo” (kutoka kwa Christus, ambalo ni neno la kilatini kumaanisha Kristo), ambaye alitezeka chini ya Pilato wakati wa kiongozi Teberius. Suetonius , kama kinara mkuu wa mfalme Hadriana (Hadrian), aliandika kwamba, kulikuwa na mtu aliyeitwa Kristo (christus) ambaye aliishi wakati wa karne ya kwanza (Annals 15:44).

Flavius Josephus (Yosefasi) ni mwanahistoria maarufu wa Kiyahudi. Katika uandishi wake unamrejelea Yakobo “ndugu yake Yesu, aliyeitwa Kristo” Kuna aya ya kutatanisha aya (18:3) ambayo yasema, “Sasa kulikuwa na huu wakati Yesu, mtu wa hekima, kama itakuwa kisheria kumwita mtu. Ni yeye alifanya maajabu, alikuwa Kristo, alitokea kwao akiwa hai tena siku ya tatu, vile unabii wa kweli ulikwishasema juu yake na vitu vingine elfu kumi vilisema kuhusu juu yake. “Tafsiri moja yasoma, “kwa wakati huu kulikuwa na mtu wa hekima aitwaye Yesu. Tabia yake ilikuwa nzuri, alijulikana kwa maadili mema. Na watu wengi kutoka kwa Wayahudi na mataifa mengine wakawa wanafunzi wake na hawakuacha huanafunzi wao. Waliripoti kwamba aliwatokea siku tatu baada ya kusulubiwa kwake; kwa hivyo alikuwa Masia, ambae manabii walisema makuu yake.”

Julius Africans anamnukuu Thallus mwanahistoria kwa mjadala juu ya giza lilokuja baada ya kusulubiwa kwa Yesu (Extant writings, 18).

Pliny mudogo, kwa barua 10:96 anakili wakristo wa kwanza wakiabudu na kuongezea kuwa wakristo walimwabudu Yesu kama Mungu na walikua na heshima na walikuwa wakishiriki mesa ya bwana.

Mdhuluma wa Kibabeli (Sunhedrin 43a) anatibitisha kwamba kusulubiwa kwa Yesu siku ya pasaka na makisio kwamba Yesu alifanya uchawi na kuipa moyo fundisho potovu la Kiyahudi.

Luciana (Lucian) wa Samosata alikuwa mgiriki mwandishi katika karne ya pili anayekubali kwamba wakristo walimwabudu Yesu, na kuleta mafundisho mapya na alisulibiwa kwa ajili yao. Alisema kwamba mafundisho ya Yesu yalijumlisha undugu wa wakristo, umuimu wa kuokoka, na umuimu wa kukataa miungu. Wakristo waliishi kulingana na sheria ya Yesu, waliamini kuwa mili yao haiharabiki na walikuwa wakijulikana kwa kutoogopa kifo, na kutolea nafsi zao kwa hiari yao na kukataa utajili wa dunia.

Mara Bar-seapion anatibitisha kwamba Yesu alifunzwa kuwa mtu wa hekima na maadili mema, alichukuliwa na wengi kuwa mfalme wa Israeli. Alisulubiwa na Wayahudi, na aliishi njia wanafunzi wake wanafundisha.

Pia tuko na maandishi ya Wayunani (Injili ya kweli/The Gospel of Truth, Kitabu kingine cha Yohana/Apocryphon of John, Injili ya Thomasi/ The Gospel of Thomas, Makubaliano juu ya ufufuo/The Treaties on Resurrection na mengine) yote yanamtaja Yesu.

Kwa kweli tunaweza kujenga injili kutoka kwa maandishi yasiyo ya kikristo. Yesu aliitwa Kristo (Josephus), alitenda “miujiza” aliwaongoza waisraeli kwa mafunzo mapya na aliangikwa siku ya pasaka kwa ajili yao (Ubebari wa kibabeli/ Babylonian Tulmud), katika Yuda (Tacticus), lakini alisema kuwa Mungu na atarudi (Eliezar), ambacho wanafunzi wake waliamini na kumwabudu kyeye kama Mungu (Pliny mdogo).

Kuna ushaidi wa kufurahisha wa kuwepo kwa Yesu, zote katika historia za kawaida na historia ya kibilia. Ingawa ushaidi mkubwa ya kwamba Yesu alikuepo ni ule kwamba maelfu ya Wakristo katika karne ya kwanza baada ya Yesu kuzaliwa (A.D), wanafunzi kumi na wawili wakiwemo, walikuwa karibu kuyatoa maisha yao hata kufa kwa sababu ya Yesu Kristo. Watu walikufa kwa ajili ya walichokiamini kuwa kweli, lakini hakuna aliyekufa kwa ajili alichokijua kuwa uongo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Akika Yesu aliishi? Kunao ushahidi wa kale/historia kuwa Yesu aliishi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries