settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu mtu wa aina gani?

Jibu


Ingawa "hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza…" (Isaya 53:2), ni tabia yake Yesu ambayo ilivutia watu kwake. Yeye alikuwa mtu wa tabia nzuri.

Yesu alijawa na rehema. Alihurumia umati wa watu "kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji" (Mathayo 9:36). Kwa sababu ya rehema zake kwao, yeye aliponya magonjwa yao (Mathayo 14:14; 20:34), na kwa sababu ya njaa yao, kwa rehema zake aliunda chakula cha kutosha kulisha umati wa watu angalau mara mbili (Mathayo 14:13-21; 15:29-39).

Yesu alikuwa mwenye umakinifu. Alikuwa na utume maishani na hakupotoshwa, alijua uzani wa utume wake na kwamba wakati ulikuwa mfupi. Nia yake ilikuwa ile ya MUHUDUMU. "Hakuja kutumikiwa, bali kutumika" (Marko 10:45). Tabia yake ilkuwa ya UKARIMU na KUTOJIPENDA yeye mwenyewe.

Yesu alikuwa MYENYEKEVU kwa mapenzi ya Baba yake alipokuja duniani na vilevile msalabani. Alijua kuwa kufa msalabani ndio malipo pekee Baba yake angeweza kukubali kwa wokovu wetu. Aliomba usiku wa kusalitiwa kwake na Yudasi, "Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe" (Mathayo 26:39). Pia aikuwa Mwana mtiifu kwa Mariamu na Yosefu. Alikua katika mazingira ya kawaida yenye dhambi, lakini yeye alikuwa "mtiifu" kwa wazazi wake (Luka 2:51). Alikuwa MTIIFU kwa mapenzi ya Baba yake. "Alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyo mpata" (Waebrania 5:8). "Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15).

Yesu alikuwa na moyo wa REHEMA na MSAMAHA. Pale msalabani aliomba, "Baba, uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo" (Luka 23:34). Yesu alikuwa MWENYE KUPENDA katika mahusiano yake. Kwa mfano, Yohana 11:5 inasema, "Yesu aliwapenda Martha, na dada yake na Lazaro" (Yohana 11:5). Yohana alijitambulisha kama mwanafunzi "ambaye Yesu alimpenda" (Yohana 13:23).

Yesu alikuwa na sifa ya kuwa MWEMA na KUJALI. Aliponya mara nyingi ili watu wapate kumjua. Kweli alidhibitisha kuwa Mwana wa Mungu aliye hai kwa miujiza yote aliyotenda, wakati wote akionyesha kujali wengine kwa mateso waliyopitia.

Yesu alikuwa MWAMINIFU na MSEMA UKWELI. Kamwe hakukiuka Neno lake mwenyewe. Alinena ukweli popote alipoenda. Aliishi maisha tunayoweza kuiga kwa wazi. Yesu alisema, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima." (Yohana 14:6). Wakati huo huo, alikuwa mwenye AMANI. Hakuwa na mahojiano, au kujilazimisha katika mioyo ya watu.

Yesu alikuwa na UHUSIANO WA KARIBU na wafuasi wake. Alitumia wakati mwingi pamoja nao. Alitamani ushirika wao, aliwafunza na kuwasaidia kuzingatia kile ambacho ni cha milele. Pia alikuwa ba uhusiano wa karibu na Baba yake wa mbinguni. Alimuomba mara kwa mara, kumsikiza, kumtii, na kujali sifa njema ya Mungu. Yesu alipowaona wabadilishaji pesa ambao walikuwa wanawatumia vibaya waabudu, aliwafukuza. Alisema, "Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi" (Luka 19:46). Yesu alikuwa KIONGOZI mwenye NGUVU na mpole. Kila mahali alipoenda watu walimfuata, wakitamani kusikiliza mafundisho yake. Watu walishangaa kwa kuwa aliongea kwa MAMLAKA (Marko 1:27-28; Mathayo 7:28-29).

Yesu alikuwa MVUMILIVU, akijua na kuelewa udhaifu wetu. Mara kadhaa katika vitabu vya Injili, Yesu alidhibitisha uvumilivu wake mbele ya maudhi yetu yasiyokuwa na Imani (Mathayo 8:26; Marko 9:19; Yohana 14:9, tazama 2Petro 3:9).

Waumini wote wanapaswa kutamani kuiga tabia ya Yesu kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu. Vitu vilivyowavutia watu kwa Yesu vinapaswa kuwa vitu ambavyo vinawavutia watu kwetu. Tunahitaji kusoma Neno la Mungu (Biblia) ili kujua na kuelewa haswa ni nani mungu na kujua mapenzi Yake kwetu. Tunapaswa kufanya kila jambo kwa utukufu wa Bwana (1 Wakorintho 10:31), kuishi kama chumvi na nuru duniani na kuwaelekeza wengine katika ukweli wa kushangaza wa Mungu na wokovu ndani yake (Mathayo 5:13–16; 28:18–20).

Wafilipi 2:1-2 ni mukhutasari mzuri wa jinsi Yesu alivyokuwa na vile tunapaswa kumuiga:

Basi ikiwako faraja yoyote katika Kristo, yakiwako matulizo yoyote ya mapenzi, ukiwako ushirika wowote wa Roho, ikiwako huruma yoyote na rehema, ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristi ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu mtu wa aina gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries