settings icon
share icon
Swali

Ni namna gani mambo ambayo Yesu aliyasema na kutenda akiwa peke yake yalipata kuandikwa katika Injili?

Jibu


Kuna mara nyingi katika vitabu vya Injili ambapo meneno ya Yesu yamenukuliwa au mantendo yake akiwa peke yake yemeelezewa. Kwa mfano, wakati Yesu alikuwa katika jangwa kwa siku arobaini (Mathayo 4) au akiomba katika bustani mwa Gethsemane (Marko 14), alikuwa peke yake. Ni namna gani mtu yeyote alipata kujua chenye alisema au kufanya, jinsi hakukuwa na shahidi yeyote aliyeshuhudia kilichofanyika?

Simulizi za Injili hazikuandikiwa wakati na saa matukio yalifanyika, kama nakala yeyote ya kila siku, bali zilikusanywa pamoja baadaye, kama vile wanahistoria wengi wanaadhitia, kwa msingi wa kumbukumbu, utafiti, na mkusanyo/mtungo. Mathayo na Yohana wote walishuhudia matukio mengi katika Habari yao. Marko na Luka walipata habari ya wale walioshuhudia. Kwa hakika, Luka anataja hilo kwamba "nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo" kabla ya kuandika Injili yake (Luka 1:3). Kuna uwezekano kuwa Marko alitoa habari ya Injili yake toka kwa mtume Petro (1Petro 5:13). Faida nyingine waandishi walikuwa nayo-na hii ni kubwa sana-ni kwamba waliongozwa na Roho Mtakatifu (2Timotheo 3:16). Hakika, Yesu alikuwa amewaahidi kuwa Roho atawakumbusha "mambo yote aliyosema" (Yohana 14:26).

Na bado, ni jinsi gani wanafunzi walijua kile kilichoendelea wakati walikuwa mbali na Yesu? Elezo liwezekanalo ni kwamba Roho Mtakatifu aliwaambia kile kilichofanyika walipokuwa wakiandika hadhiti yao. Kwa kuamini kuwa Injili ni pumzi ya Mungu, kwa urahisi tunaweza kukubali elezo hilo.

Elezo lingine ni rahisi kuwa Yesu baadaye aliwaambia wanafunzi wake chenye hawakupata. Katika Mathayo 4 hakuna mwanafunzi yeyote aliyekuwa na Yesu wakati wa majaribu jangwani, lakini baadaye Yesu aliishi na wanafunzi miaka mitatu. Hakuna uwezekano kuwa Yesu aliwaambia chenye kilifanyika wakati Fulani katika miaka hiyo tatu? Vile vile, Yesu alikuwa peke yake aliposungumza na mwanamke kisimani katika Yohana 4, huku masungumzo yao yamenukuliwa kwa upana. Elezo la maana la pamoja ni kuwa Yesu aliwajaza wanafunzi wake. Au pengine Yohana alipata alipata habari kutoka kwa mwanamke, ikisingatiwa kuwa wanafunzi waliishi katika mji wake kwa siku arobaini wakifuatilia masungumzo yake (Yohana 4:40).

Baada ya ufufuko wake, Yesu aliwatokea wanafunzi wake kwa kipindi cha siku arobaini "aliongea nao juu ya ufalme wa Mungu" (Matendo 1:3). Katika siku hizo arobaini, Yesu alikuwa na nafasi mwafaka ya kuwajulisha wanafunzi mambo yote yaliyomfanyikia wakati hawakuwa karibu. Kwa vyovyote vile, matukio ya maisha ya Yesu ambayo Mungu alinuia tujue-ikiwa ni pamoja na matukio yaliyofanyika katika upweke- yalinakiliwa. Kuu ni Mungu ananuia sisi tujue. Labda matukio yalifunuliwa moja kwa moja kwa wanafunzi baadaye na Yesu au mtu mwingine, au mitume walijifunza simulizi yote kutoka kwa Roho Mtakatifu walipoandika Neno la Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni namna gani mambo ambayo Yesu aliyasema na kutenda akiwa peke yake yalipata kuandikwa katika Injili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries