settings icon
share icon
Swali

Yusufu alikuwa wapi wakati Yesu alikuwa mtu mzima?

Jibu


Wakati wa mwisho Yusufu ametajwa katika Biblia ni wakati Yesu alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili. Kurudi kutoka safari kwenda Yerusalemu, Yesu alitenganishwa na wazazi Wake, ambao hatimaye walimpata Hekaluni akizungumza na walimu. Kwa kushangaza, ilikuwa wakati huo-wakati Yesu alitangaza kwamba alikuwa lazima awe katika biashara ya Baba yake wa mbinguni-kwamba kutaja yoyote juu ya baba wake duniani hukoma (Luka 2: 41-50).

Kwa sababu Yusufu hajatajwa tena, wasomi wengi wanafikiri alikufa kabla ya Yesu kuanza huduma yake ya umma. Wakati tunapofika kwenye harusi huko Cana (Yohana 2), Yusufu ni wazi kabisa hakua. Tunamwona Maria huko, lakini hakuna kutajwa kwa Yusufu. Pengine sehemu ya sababu Yesu alibaki nyumbani hadi alipofikia miaka 30 ni kwamba alikuwa na jukumu la kutunza familia.

Nadharia ya kwamba Yusufu alikuwa amefariki wakati Yesu alikuwa mtu mzima imepewa uaminifu zaidi kwa ukweli kwamba Yesu, wakati alipokuwa msalabani, alifanya mipangilio ya mama yake kutunzwa na mtume Yohana (Yohana 19: 26-27) ). Yusufu lazima alikua amekufa wakati wa kusulubiwa, au Yesu hangempeana Maria kwa Yohana. Kama Yusufu alikuwa bado yu hai, Yesu hangesema, "Sasa, Mama, nitakuacha kwa Yohana." Yusufu angeweza kujibu kwa hakika, "Subiri kwa dakika; ni wajibu wangu kumtunza. "Mjane tu ndo anaweza kupeanwa hakika katika utunzi wa mtu aliye nje ya familia ya karibu.

Inafikiriwa na wengine kuwa labda Yusufu alikufa baada ya Yesu kuanza huduma yake ya umma. Hii haiwezekani, kwa sababu, ikiwa Yusufu alikuwa amekufa wakati wa huduma ya miaka mitatu ya Kristo, hiyo ingekuwa tukio kubwa; Yesu bila shaka angeenda kwa mazishi pamoja na wanafunzi Wake, na angalau mmoja wa waandishi wa Injili angeandika. Ingawa hatujui kwa hakika, hali ya uwezekano ni kwamba Yusufu alikufa wakati kabla ya Yesu kuanza huduma yake duniani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yusufu alikuwa wapi wakati Yesu alikuwa mtu mzima?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries