settings icon
share icon
Swali

Je! Ina maana gani kuwa Yesu Kristo ndiye jiwe kuu la msingi/pembeni?

Jibu


Tangu enzi za jadi, waashi/wajenzi wamekuwa wakitumia jiwe la kuu la msingi katika miradi yao ya ujenzi. Jiwe la pembeni ndilo nguzo kuu, mara nyingi linawekwa katika pembe la jumba ili kutoa mwongozo kwa wajenzi katika ujenzi. Jiwe kuu la pembeni likikuwa mojawapo ya jiwe kubwa zaidi, gumu zaidi, na jiwe lililojengwa kwa umakinifu sana kati yam awe ya jumba. Biblia inamwelezea Yesu kama jiwe kuu la pembeni ambalo kanisa lake litajengwa juu yake. Yeye ndiye msingi. Pindi jiwe kuu la pembeni lilipotiwa, lilikuwa kigezo cha kuamua kila kipimo katika jengo nzima; kila kitu kilitiwa kulingana nalo. Kima jiwe kuu la pembeni la jumba la kanisa, Yesu ndiye kigezo chetu ukadiri na usawa.

Kitabu cha Isaya kina marejeleo mengi ya Masihi atakeyekuja. Mahali kwingi Masihi anajulikana kwetu kuwa" Jiwe Kuu la pembeni," kama vile katika unabii: "Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: "Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: 'Anayeamini hatatishika.' Nitatumia haki kama kipimo changu, nitatumia uadilifu kupimia." Mvua ya mawe itaufagilia mbali uongo mnaoutegemea, na mafuriko yataharibu kinga yenu'" (Isaya 28:16-17). Kwa muktadha, Mungu anasungumza na wadhihaki na majivuno wa Yuda, na anaahidi kutuma Jiwe kuu la pembeni Mwanawe mpenzi-ambaye atatoa msingi dhabiti kwa maisha yao, ikiwa watamwamini Yeye.

Katika Agano Jipya jiwe kuu la pembeni linaendelzwa kama mithali. Mtume Paulo alitamani sana Wakristo wa Efeso kumjua Kristo vyema: "Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana (Waefeso 2:19-21). Zaidi ya hayo, katika 1 Petro 2:6, chenye Isaya alisema karne zilizopita kinathibitishwa kwa maneno yale yale.

Petro anasema kwamba, Yesu kama jiwe letu kuu la pembeni "mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa" (1Petro 2:4). Jiwe kuu la pembeni ni la kutegemwa pia, na "Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa" (aya 6).

Kwa bahati mbaya, sio kila mtu anajiweka kwa jiwe kuu la Pembeni. Baadhi humkubali Kristo; na baadhi humkataa. Yesu ndiye "Jiwe walilokataa waashi" (Marko 12:10; ona pia Zaburi 118:22). Wakati habari ya ujio wa Masihi iliwafikia mamajusi kutoka Mashariki, waliamua kumletea dhaabu, tunu na uvumba na manemane. Lakini wakati Habari hiyo hiyo ilimfikia Mfalme Herode kule Yerusalemu, itikio lake lilikuwa la kujaribu kumuua. Kutoka mwanzo, Yesu alikuwa "Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu" (1Petro 2:8).

Je! watu wanawezaje kulikataa jiwe kuu teule la msingi la Mungu? Kwa ufupi, wanataka kujenga kitu tofauti kutoka na kile Mungu anakijenga. Kame vile watu walioujenga mnara wa Babeli waliasi dhidi ya Mungu na wakakimbilia mradi wao wenye, wale wanaomkataa Kristo hukataa mpango wa Mungu kwa minajili ya mpango wao wenyewe. Hukumu imeahidiwa kwa wale wote wanaomkataa Kristo: "Atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda" (Mathayo 21:44).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ina maana gani kuwa Yesu Kristo ndiye jiwe kuu la msingi/pembeni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries