settings icon
share icon
Swali

Inamaanisha nini kuwa Yesu Kristo alishinda kifo?

Jibu


Ni dhahiri kuwa, kauli kuwa Kristo ameshinda kifo hurejelea ufufuo wake. Alikufa na sasa yu hai (ona Ufunuo 1:18). Maneno haya matatu-Kristo alishinda kifo-hufafanua tofauti maalum kati ya Ukristo na dini zingine zote. Hamna kiongozi yeyote wa dini amewahi tabiri kifo chake mwenyewe na ufufuo (Mathayo 16:21), madai yake yakiungwa na yeye mwenyewe pamoja na mafundisho yake kuhusu utabiri huo (Yohana 2:18-22; Mathayo 27:40), na kisha akatunza ahadi hiyo (Luka 24:6).

Ufufuo wa Yesu unatia alama katika historia kuwa mtu alifufuka kutoka wafu na hatakufa tena. Wengine wote waliofufuliwa hatimaye walikufa tena (ona 1Wafalme 17:17-24; 2Wafalme 4:32-37; Marko 5:39-42; Yohana 11:38-44). Ufufuo wa Yesu ulikuwa ushindi wa kweli na kamili kwa kifo. Kama vile Mwana Mtakatifu wa Mungu, Yesu alishinda kifo mara moja vile Petro anaelezea: "Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, akamwokoa katika maumivu ya kifo kwa maana haingewezekana kabisa kifo kimfunge" (Matendo 2:24). Shangwe ya Kristo aliyefufuka ilisema, "Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwa nimekufa, lakini, tazama, sasa ni hai milele na milele. Ninazo funguo za kifo na kuzimu" (Ufunuo 1:18). Funguo ni ishara ya mamlaka. Yesu ni mkuu juu ya kifo. Ushindi wa Kristo kwa kifo ulikuwa wa kudumu na wa milele.

Kristo alishinda kifo kwa sababu hakuwa na dhambi. Laana juu ya mwanadamu katika bustani mwa Edeni, ililetwa na dhambi yao, na hii ilesemwa wazi: "hakika utakufa" (Mwanzo 2:17). Tangu wakati huo tumeona ukweli wa Warumi 6:23, "Mshahara wa dhambi ni kifo." Lakini Yesu Kristo hakuwa na dhambi (1Petro 2:22); kwa hivyo, kifo hakikuwa na mamlaka juu yake. Kifo cha Yesu kilikuwa dhabihu ya hiari kwa dhambi zetu, na kwa mjibu wa ukamilifu wake usio na dhambi, ufufuo Wake kimantiki ulifuata. "nautoa uhai wangu," Yesu alisema, "ili nipate kuupokea tena" (Yohana 10:17).

Ukweli kwamba Kristo ameshinda kifo ina matokeo hadhari za milele. Habari njema ni-Injili-msingi wake uu katika ushindi wa Kristo juu ya kifo. Bila ufufuo, hakuna injili; hakika, kamwe hakuna tumaini kwetu: "Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu" (1Wakorintho 15:17). Lakini Kristo amefufuka, na kama washindi wenzi pamoja naye, Wakristo "tumekwisha pita kutoka katika kifo" (1Yohana 3:14). Kristo "amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo" (2Timothy 1:10).

Ukweli kwamba Kristo ameshinda kifo yamaanisha kuwa waumini pia wamepewa ushindi juu ya kifo. Sisi tu "katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda" (Warumi 8:37). Kristo ndiye "wa kwanza wa wale waliolala katika kifo" (1Wakorintho 15:20), ambayo yamaanisha kuwa ufufuo wa Kristo ndio wa kwanza kati ya wengi: waumini ambao "wamelala" (kufa) vile vile watafufuliwa. Yesu aliwahidi wanafunzi wake, "kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai" (Yohana 14:19).

Ukweli kwamba Kristo ameshinda kifo ni utimizo wa unabii. Mtunga zaburi alitabiri kuwa Masihi atashinda kifo: "Naam wewe hutaiacha nafsi yangu kuzimu, hutaniacha mimi mwaminifu wako nipate kuoza" (Zaburi 16:10). Manabii wengine walitia watu wa Mungu tumaini kuwa Bwana siku moja ataondoa kifo: "Bwana Mungu atakiangamiza kifo milele! Atayafuta machozi katika nyuso za watu wote na kuwaondolea watu wake aibu duniani kote" (Isaya 25:8), na "Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma! (Hosea 13:14; rejelea na 1 Wakorintho 15:54-55).

Kifo ndio silaha ya nguvu sana ya Shetani, na ya kututisha. Katiak msalaba Kristo alimshinda Shetani kwa niapa yetu sisi wenye dhambi wanyonge: "Sasa ndio wakati wa ulimwengu huu kuhukumiwa; sasa mtawala wa ulimwengu huu atapinduliwa" (Yohana 12:31; angalia Wakolosai 2:15). Kwa kaburi lililo tupu, Kristo aliangamiza silaha kali ya Shetani, kifo. Shetani, mshtaki, sasa hana nguvu ya kuwahukumu Wakristo. Hatutashiriki hatima yake (Ufunuo 12:9-11; 20:10,14).

Wkati Kristo alishinda kifo kwa ajili yetu, aliutoa ule "uchungu wa kifo," dhambi (1Wakorintho 15:56)-hivyo, hatutahukumiwa na Mungu kulingana na dhambi zetu; ili hali, tutasimama mbele za Mungu tukiwa tumevikwa haki kamilifu ya Kristo. Hii ndio sababu waumini katika Kristo "Mshindi hataumizwa na kifo cha pili" (Ufunuo 2:11), na "Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao" (Ufunuo 20:6). Kristo amepokea adhabu yetu ya dhambi na kupitia kifo chake, ameshinda kifo (Ufunuo 20:14).

Waumini "katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda" (Warumi 8:37). Ni kitu gani kitatutenganisha na upendo wa Mungu katika Kristo? "wala mauti, wala uzima" (aya 38). Kristo ameshinda kifo, na waumini wanasiama wima kwa neno Yesu: "Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi; 26na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe" (Yohana 11:25-26).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inamaanisha nini kuwa Yesu Kristo alishinda kifo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries