settings icon
share icon
Swali

Kama wokovu wetu uu salama milele, ni kwa nini Biblia inatuonya kwa nguvu dhidi ya uasi?

Jibu


Sababu hasa Biblia inatuonya kwa nguvu dhidi ya uasi ni kwamba mabadiliko ya kweli ya kipimo kwa matunda yanayoonekana. Wakati Yohana Mbatizaji alikuwa akibatiza watu katika mto Yorodani, aliwaonya wale ambao walidhani wao walikuwa na haki na " kuzaa matunda katika kutunza toba" ( Mathayo 3:7). Yesu aliwaonya wale ambao walikuwa wakimsikiliza alipokuwa akitoa Hotuba ya Mlimani, kila mti unaweza kujulikana kwa matunda yake (Mathayo 7:16) na kwamba kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni (Mathayo 7:19).

Nia ya maonyo haya ni kukabiliana na kile baadhi ya watu huita ni "rahisi kuamini." Kwa maneno mengine, kumfuata Yesu ni zaidi ya kusema wewe ni Mkristo. Mtu yeyote anaweza kudai Kristo kama Mwokozi, lakini wale ambao kweli wameokolewa huzaa matunda yanayoonekana. Sasa, mtu anaweza kuuliza swali, "Ni nini maana ya matunda?" Mfano ulio wazi wa matunda ya Mkristo unaweza kupatikana katika Wagalatia 5:22-23 ambapo Paulo anayaelezea matunda ya Roho Mtakatifu: upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole, na kujizuia. Kuna aina nyingine ya matunda Mkristo (kama vile sifa, kushinda nafsi kwa Kristo), lakini orodha hii inatupa sisi muhtasari mzuri wa mitazamo ya Kikristo. Waumini wa kweli waonyesha wazi tabia hizi katika maisha yao kwa kiwango cha kuongezeka wanapoendelea katika safari yao ya Kikristo (2 Petro 1:5-8).

Ni hawa wanafunzi wanao zaa matunda ambao wako na dhamana ya usalama wa milele, na wao watavumilia hadi mwisho. Kuna maandiko mengi ambayo yamebeba haya. Warumi 8:29-30 inaelezea "mzululo wa maadili ya kidhahabu" wa wokovu kwa kusema kwamba wale waliokwisha julikana na Mungu walikuwa tangu asili, waliitwa, mwadilifu, na utukufu kwa sababu hakuna hasara njiani. Wafilipi 1:6 inatuambia kwamba kazi ambayo Mungu ameianza ndani yetu, Yeye pia ataikamilisha. Waefeso 1:13-14 inafundisha kuwa Mungu ametutia muhuri juu ya yetu kwa Roho Mtakatifu kama dhamana ya urithi wetu hadi pale tutakao umiliki. Yohana 10:29 inathibitisha kwamba hakuna mtu ana uwezo wa kumchukua kondoo wa Mungu mikononi mwake. Kuna maandiko mengine mengi ambayo husema kitu kimoja - kweli waumini ni salama milele katika wokovu wao.

Vifungu vinavyoonya dhidi ya uasi hutumika kimsingi kwa madhumuni mawili. Kwanza, kuwahimiza waumini wa kweli kuhakikisha "wito na uchaguzi." Wao. Paulo anatuambia katika 2 Wakorintho 13:5 tujichunguze wenyewe ili tuone kama sisi tuko katika imani. Kama waumini wa kweli na wafuasi wa Yesu Kristo wanaozaa matunda, basi tuwe na uwezo wa kuona ushahidi wa wokovu. Wakristo huzaa matunda katika viwango na misingi mbali mbali vya utii na vipawa vyao vya kiroho, lakini Wakristo wote huzaa matunda; na tunapaswa kuona ushahidi wa hayo tunapo jioji sisi wenyewe.

Kutakuwa na vipindi katika maisha ya Mkristo ambapo hakutakuwa na matunda yanayoonekana. Huu utakuwa wakati wa dhambi na uasi. Kinachotokea nyakati hizi za uasi wa muda mrefu ni kwamba Mungu huondoa ndani yetu uhakika wa wokovu wetu. Hiyo ndio sababu ni kwa nini Daudi aliomba katika Zaburi ya 51 arejeshewe "furaha ya wokovu" (Zaburi 51:12). Tunapoteza furaha ya wokovu wetu wakati sisi huishi katika dhambi. Hiyo ndio sababu Biblia inatuambia na "Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe" (2 Wakorintho 13:5). Mkristo wa kweli wakati anajioji mwenyewe na aone hakuna mafanikio ya hivi karibuni, ni lazima imwongoze kwenye toba kubwa na kugeuka kwa Mungu .

Sababu ya pili ya vifungu juu ya uasi ni kuwaonyesha wazi waasi ili tuweze kuwatambua. Mpotofu ni mtu ambaye anaacha imani yake ya kidini. Ni wazi kutokana kwa Biblia kwamba waasi ni watu ambao walifanya maarufu wa imani katika Yesu Kristo, lakini kamwe hawakumpokea kama Mwokozi wao. Mathayo 13:1-9 (Mfano wa Mpanzi) unaeleza hatua hii kikamilifu. Katika mfano huo, mpanzi alipanda mbegu, mfano wa neno la Mungu, kwenye aina nne za udongo: udongo ngumu, udongo wa mawe, udongo wa miba, na udongo wenye rutuba ya faida kwa mkulima. Dongo hizi zinawakilisha aina nne ya majibu kwa injili. Wa kwanza ni kukataa wazi kabisa, ambapo zingine tatu huwakilisha ngazi mbalimbali za kukubalika. Udongo wa mawe na ule wa miba unawakilisha watu ambao awali waliitikia injili vizuri, lakini wakati udhalimu unapotokea (udongo wa magugu) au wasiwasi wa ulimwengu unawaangusha chini. Yesu anaziweka wazi aina hizi mbili za majibu kwamba, ingawa awali "waliikubali" injili, wao hawakupata kuzaa matunda yoyote kwa sababu mbegu ya (injili) haikupenya udongo wa moyo wao. Ni udongo wa nne pekee, ambao ulikuwa "umetayarishwa" na Mungu na ulikuwa na uwezo wa kupokea mbegu na kuzaa matunda. Tena, Yesu anasema katika mahubiri ya Mlimani, "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, ataingia katika Ufalme wa mbinguni"(Mathayo 7:21).

Inaweza kuonekana kuwa si jambo la kawaida Biblia kuonya dhidi ya uasi na wakati huo huo iseme kwamba muumini wa kweli kamwe hawezi kuasi. Hata hivyo, hiki ni kile maandiko yanasema. Yohana wa Kwanza 2:19 hasa inaeleza kwamba wale ambao huasi wanaonyesha kwamba hawakuwa waumini wa kweli. Onyo la kibiblia dhidi ya uasi, kwa hivyo, ni lazima huwa onyo kwa wale walio katika "imani" bila kuipokea kwa kweli. Maandiko kama vile Waebrania 6:4-6 na Waebrania 10:26-29 ni onyo kwa "kujifanya" Muumini kwamba wanahitaji kujichunguza wenyewe na kuona kama ikiwa wao hunuia kuasi, basi wao hawajaokolewa kwa kweli. Mathayo 7:22-23 inaonyesha kwamba wale " waumini wa kujipandika" ambao Mungu amewakataa si kwa sababu wameipoteza imani, bali ni kwa sababu ya kuwa Mungu kamwe hakuwajua wao.

Kunao watu wengi ambao wako tayari kutajimbulisha na Yesu. Ambao hawataki uzima wa milele na baraka? Hata hivyo, Yesu anatuonya kuhesabu gharama ya uanafunzi (Luka 9:23-26, 14:25-33). Waumini wa kweli huhesabiwa gharama hizo, bali waasi hawajahesabu. Waasi ni watu ambao, wakati wanaiacha imani, hutoa ushahidi kuwa wao kamwe hawakuwa wameokoka katika nafasi ya kwanza (1 Yohana 2:19). Uasi si kuupoteza wokovu, bali ni dhihirisho kwamba wokovu kamwe haumilikiwi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kama wokovu wetu uu salama milele, ni kwa nini Biblia inatuonya kwa nguvu dhidi ya uasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries