settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kwamba kutakuwa na watu wenye kudhihaka katika siku za mwisho?

Jibu


Vifungu viwili katika Biblia vinasema kwamba “katika siku za mwisho watakuja watu wenye dhihaka”. Waraka wa pili wa Petro 3:3 na Yuda 1:18 zote zinaelezea maana ya mdhihaki. Mtu mwenye kudhihaka katika muktadha huu, ni mtu ambaye anamdhihaki Kristo, anadharau mambo ya Mungu na kupinga Injili.Petro na Yuda wote walikuwa wanaandika onyo dhidi ya waalimu wa uongo ambao walikuwa na nia ya kuwapotosha wengine. Neno ‘mdhihaki’ linarejelea mtu ambaye anaukataa ukweli wa maandiko na kuwashawishi wengine ili wakubali uongo zake.

Watu wenye kudhihaki wamekuweko tangu bustani mwa Edeni. Jaribu la kwanza la shetani kwa mwanadamu lilikuwa kwa mfano wa kudhihaks kwa amri za Mungu: “Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu-?” (Mwanzo 3:1). Watu wenye dhihaka walitawala siku za Nuhu (Mwanzo 6:5-8; Waebrania 11:7), hii ilimwacha Mungu bila chaguo ila kuwaangamiza wote na kuanza upya na Nuhu, ambaye alikuwa mtu mwadilifu pekee duniani. Wenye dhihaka hukataa kuamini maandiko ya Bwana na kujitengenezea miungu yao (2Mambo ya Nyakati 36:16). Mwandishi wa zaburi anaonya dhidi ya mtengano unaotokana na uhusiano na watu waovu hadi kuketi “barazani pa wenye mizaha” ( Zaburi 1:1), kukumbatia mtazamo wao wa kiulimwengu na kushiriki katika hatima yao.

Ingawa wenye dhihaka wamekuwa sehemu ya ulimwengu huu ulioanguka, maandiko yanaonekana kuashiria kwamba, siku ya Bwana inapokaribia, kudhihaki kunaongezeka. Petro anawaeleza wenye dhihaka hawa kama “wafuatao tamaa zao wenyewe” (2 Petro3:3) na kuhoji ujio wa pili wa Bwana Yesu (2Petro 3:4). Maelfu ya miaka yamepita tangu Yesu aende mbinguni,akiahidi kwamba atawakujia waaminifu wake (Yohana 14:1-4; Ufunuo 22:12). Wenye dhihaka huonyesha upotevu wa wakati na kuwadhihaki wale ambao bado wanatamani na kungoja kurudi Kwake (2 Timotheo 4:8; 2 Wathesalonike 1:7).

Yuda anaeleza wenye dhihaka wa siku za mwisho kama watu wanaofuata tamaa mbaya na kuleta mgawanyiko katika kanisa (Yuda 1:18). Wanaweza jionyesha kama viongonzi wa kanisa, lakini “hawana roho” (Yuda 1:19). Paulo anaeleza kwa upana kuhusu hali ya ulimwengu itakavyo kuwa kabla ya kurudi kwa Yesu. “Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu: wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo” (2 Timotheo 3:1-5). Wadhihaki wataingiana na umati kama huo.

Tayari tunaona ongezeko la wadhihaki katika ulimwengu wetu wa leo, na sababu kadhaa zinaweza kuchangia ongezeko hilo. Upatikanaji wa vyombo vya habari kila wakati, mtandao, na aina nyinginezo za teknolojia hutoa jukwaa wazi kwa mtu yeyote aliye na maoni, na kukejeli kila kitu ambacho kilidhaniwa kuwa cha heshima ni mchezo wa kujiburudisha. Watu wenye dhihaka hutiwa moyo kwenye mitandao ya kijamii na wengine ambao wako tayari kuidhinisha kejeli zao mara moja. Watu wengi wamesoma zaidi ya uwezo wa akili zao, na ulimwengu huu wa sasa usio na mipaka ya kimaadili unazalisha watu wenye dhihaka badala ya wenye kufikiria. Wengi hujaribu kutumia mafunzo ya kisayansi kusema kwamba, kwa kuwa ukweli wa Mungu muumba hauwezi kuthibitishwa na ufahamu wa mwanadamu, Mungu hayupo. Kwa kukataa maandiko, wanadamu wamepoteza mwelekeo wa maadili, na kutuacha bila njia ya kuamua haki au baya, nzuri au mbaya, ukweli au uongo.Katika hali hii, yeyote anayedai kujua ukweli analengwa na wenye dhihaka.

Majivuno husababisha dhihaka, kama ilivyokuwa kabla ya mnara wa Babeli (Mwanzo 11:1-4). Wakati watu hujawa na kiburi vile wao wenyewe ni muhimu, wanaanza kupinga chochote kile kinachotishia kujipenda kwao. Mara tu tunapoacha kumzingatia Mungu, basi chochote hutokea. Wadhihaki wamejaribu kuelezea ndoa upya, kufuta dhana ya jinsia mbili, na kuunda ulimwengu wa njozi ambamo ukweli huwa chochote tunachohisi. Si kitambo sana, mawazo kama hayo yalikuwa ufafanuzi wa wazimu.Sasa tunaambiwa ni hekima ya mwisho. Warumi 1:21-22 haijawahi kuwa muhimu vile; “Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga .”

Kuongezeka kwa wenye kudhihaka ni ishara ya siku za mwisho. Wanajidai kuwa wenye hekima, lakini ni wapumbavu kwelikweli (Zaburi 14:1). Haijalishi ni matukio ya eskatolojia ambayo mtu anapendelea, sote tunaweza kukubaliana kwamba idadi ya wenye dhihaka na wadanganyifu inaongezeka kwa kasi, kama vile Maandiko yalivyotuonya ingekuwa (2 Yohana 1:7). Ni muhimu kwa kila Mkiristo azingatie kwa uzito amri za kusoma na kuchambua Neno la Mungu (2 Timotheo 2;15;Yoshua 1:8) ili tusije tukapotoshwa na mawazo ya kiburi yanayotolewa kwetu na wenye dhihaka ( 2 Wakorintho 10:5)

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kwamba kutakuwa na watu wenye kudhihaka katika siku za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries