settings icon
share icon
Swali

Je, ni makosa kwa wanaume kuwa na tabia za kike au kwa wanawake kuwa na tabia za kiume?

Jibu


Ili tuweze kujibu swali hili, tunahitaji kufafanua baadhi ya maneno. Watu ni tofauti. Sisi sio vipandikizi vya biskuti vilivyogawanywa tu kwa jinsia. Mwanaume ambaye sio mnene na ambaye akona sauti nyororo anaweza kuonekana kuwa ana tabia za kike na watu wengine, lakini anaweza kuwa anakubali jinsia yake kwa furaha kama vile kikaragosi chenye misuli ya kiume. Jinsi mwanaume ameumbwa na sifa zake za asili ni zawadi kutoka kwa Mungu na hazipaswi kudhikakiwa. Na ndivyo ilivyo kwa wanawake pia. Wanawake wengine wana sifa zaidi za kike kuliko wengine. Matamanio na maslahi yao yanalingana na wazo linalokubalika la maana ya kuwa mwanamke. Mtoto wa kike mwenye mwenendo wa mtoto wa kiume anaweza kumheshimu Mungu kama vile msichana yeyote ikiwa atakubali mpango wa Mungu kwa ajili yake na kumtukuza kwa karama zake.

Kwa hivyo kwa madhumuni ya nakala hili, tutafafanua tabia za kike (kwa wanaume) na tabia za kiume (kwa wanawake) kama chaguo la mtindo wa maisha ambao ni kinyume na na jinsia ya mtu aliyopewa na Mungu. Katika Agano la Kale, neno linalotafsiriwa kama “kike” pia linatumika kurejelea mahanithi wa wa kiume (Kumbukumbu 23:17; 1 Mfalme 22:46). Katika Agano Jipya, neno la Kigiriki linalotafsiriwa kuwa “kike” linamaanisha “mpole na dhaifu.” Katika Wakorintho wa Kwanza 6:9, neno hili limeorodheshwa tofauti na ushoga, kuonyesha kwamba sio visawe. Mwanaume mwenye tabia za kike katika mstari huu ni yule ambaye amekataa uume wake na kujitambulisha kuwa ni mwanamke. Anaweza kuwa anajihusisha au pia hajihusishi na shughuli za ngono, lakini ameamua kuishi kimakusudi kama mtu “mpole na mdhaifu” badala ya kukubali utambulisho wake aliopewa na Mungu. Anachukua sifa za mwanamke na kuhusiana na wanaume wengine jinsi vile wanawake wanavyofanya.

Wakati Mungu aliumba mwanaume na mwanamke (Mwanzo 5:2), aliumba zaidi ya tofauti za kimwili. Wanaume na wanawake waliumbwa kutimiza majukumu tofauti katika uumbaji na katika uhusiano wetu na Mungu. Kukataa majukumu waliyopewa na Mungu ni dalili ya kuasi Mungu Muumba. Wetu. Wakati watu wanamkaidi Mungu na kuamua kuishi kwa nji yoyote wanayochagua, Mungu anawaruhusu kufuata tamaa zao potovu na matokeo yake ya asili. Warumi 1:26-27 inasema, “Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao wakabadili matumizi ya asili ya miili yao wakaitumia isivyokusudiwa. Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao.”

Upotovu unaongezeka wakati wanawake na wanaume wanaacha utambulisho waliopewa na Mungu na kuiga sifa za jinsia tofauti. Wanaume huwa kama wanawake na wanawake huwa kama wanaume. Dhambi iko katika chaguo letu, sio tofauti zetu za kiasili. Tunapaswa kuwa waangalifu tusije tukazipatia jinsia sifa fulani kulingana kanuni zetu za kitamaduni. Katika tamaduni zingine, wanaume kushikana mikono au kubusu shavuni ni ishara ya urafiki, wala sio ishara ya kike au ushoga. Katika wakati wa Yesu, wanaume walivaa kanzu na kuketi mezani, wakiegemea katika vifua vya wenzao ( Yohana 21:20). Lakini tofauti za tamaduni hizi hazionyeshi kwa vyovyote kukataliwa kwa uanaume.

Hali ya mabadiliko ya jinsia inaongezeka siku hizi huku kukiwa na upasuaji wa kubadilisha jinsia na kudai kwamba waliobadilisha jinsia wakubaliwe. Watu wanaacha utambulisho wao wa asili na kujitambulisha kiakili kama jinsia yoyote watakayochagua. Jamii imejiingiza katika upumbavu huu unaoleta mkanganyiko zaidi. Kwa wale wanaokabiliana na mkanganyiko wa kijinsia, suluhu yake sio kubadilisha miili yao, lakini kuruhusu Roho Mtakatifu kubadilisha mioyo yao (1 Petro 4:2). Tunaponyenyekea kikamilifu kwa Bwana Yesu tunatamani kufuata mpango wake kwa ajili yetu, badala ya kuchagua mpango wetu wenyewe (Wagalatia 2:20).

Ni makosa kwa mwanamume kuchukia jinsia yake na kujitambulisha kama mwanamke au mwanamke kuacha jinsia yake na kujitambulisha kama mwanamume. Ni kukaidi mpango wa Mungu alipoumba mwanamume na mwanamke. Kumbukubu 22:5 inasema, “Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana Bwana Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.” Amri hii haikuwa kuhusu mavazi haswa bali ilihusu kulinda utakatifu wa maana ya kuwa mwanamume au mwanamke. Warumi 1 inaonyesha kwamba mkanganyiko wa jinsia ni dalili tu ya tatizo zaidi. Wakati watu wanakaidi mamlaka ya Mungu na kujifanya miungu wao wenyewe basi machafuko hutokea. Mistari ya 21 na 22 yaonyesha tatizo hilo: “Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga.”

Kufikiri kwamba tunajua zaidi kuliko Mungu ni chazo cha kuwa mpumbavu. Wakati mwanamume anapinga uume wake au mwanamke anakataa jinsia yake ya kike, hii huwa ni dalili ya dhambi wazi: kukataa mamlaka ya Mungu. Kadri tunavyomkaribia Mungu ndivyo tunaweza kukumbatia utambulisho wetu wa jinsia. Jinsia zote mbili zinaonyesha vipengele fulani vya tabia ya Mungu kwa njia ya kipekee. Tunavyokaidi chaguo lake kwa ajili yetu, tunapunguza nafasi anazotupa kuonyesha utukufu wa kuumbwa kwa mfano wake (Mwanzo 1:27).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makosa kwa wanaume kuwa na tabia za kike au kwa wanawake kuwa na tabia za kiume?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries