settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini kuna Wakristo bandia wengi?

Jibu


Mkristo anaweza kufafanuliwa kama mtu ambaye, kwa imani amempokea na kumwamini Yesu Kristo kikamilifu kama Mwokozi kutoka kwa dhambi (Yohana 3:16; Matendo 16:31; Waefeso 2:8-9). Na ndani ya moyo wa Mkristo Roho wa Kristo anaishi (Waefeso 3:17; 1 Wakorintho 6:19; Warumi 8:11). Na sasa, “ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo” (Warumi 8:9), na mtu huyu, basi, si Mkristo. Kwa hiyo, neno “Mkristo bandia” ni jina litakuwa limetumika visivyo. Wewe ni Mkristo au si Mkristo; mtu yuko pamoja na Mungu au hayuko pamoja na Mungu (Mathayo 12:30).

Baada ya hayo kusemwa, swali hili hakika ni halali katika akili za watu wengi. Na kuna uwezekano hili hutokana na tabia za baadhi ya Wakristo; hata hivyo, inawezekana pia kwa sababu ya tabia ya wengi wanaofikiri wao ni Wakristo au wanaodai kuwa Wakristo, lakini wao sio Wakristo. Sababu za wengi kuamini kuwa wao ni Wakristo wa kweli wakati wao sio Wakristo ni nyingi mno na ni tofauti. Mafundisho ya uwongo bila shaka ni sababu moja. Wakati makanisa yanapoepuka mafundisho yenye uzima, matokeo yatakuwa makutaniko yasiojua kweli ya Neno la Mungu. Wanawezaje kushikana na Roho, wakati Kweli haimo ndani yao?

Pia, wengine wanaamini kukariri sala au kuitikia ”wito wa madhabahuni” pekee kunaweza kuwafanya kuwa Mkristo. Wengi wanaamini mapokeo yao ya kidini, kama vile kubatizwa wakiwa watoto wachanga, yaliwatengenezea nafasi Mbinguni, au kwamba matendo yao mengi mazuri pekee ndiyo yamewaweka katika msimamo mzuri mbele za Mungu. Na bila shaka wengine wanaamini kuhudhuria kanisa pekee kunawahakikishia wokovu. Jambo ni kwamba wengi wanaodai kuwa Wakristo si Wakristo hata kidogo. Bado wanasalia kuamini kwamba kila kitu kiko sawa na nafsi zao. Cha kusikitisha ni kwamba, wengi wataishi maisha yao yote wakiamini walikuwa Wakristo hadi siku moja watakaposikia maneno haya kutoka kwa Yesu: “Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!” (Mathayo 7:23).

Fundisho la wazi la Biblia ni kwamba mtu anapookolewa maisha yake yatabadilika kwa hakika kwani yeye “amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17). Mkristo ambaye kwa kweli amaezaliwa mara ya pili atajitahidi kuleta utukufu na heshima kwa Kristo kwa kuishi maisha yanayompendeza Mungu (1 Petro 1:15-16, 4:1-4). Imani ya kweli iokayo itazaa matendo au “matunda” katika maisha ya muumini (Yakobo 2:17, 26). Kwa hivyo ikiwa hakuna matendo ya upendo katika maisha ya mtu, kujichunguza kwa uangalifu kunahitajika. Mtume Paulo aliwaagiza wale waliokuwa Korintho wafanye jambo lili hili: “Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Yesu Kristo yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho!” (2 Wakorintho 13:5). Hakika, ukiri wa aina yeyote wa imani ambayo haileti mabadiliko ya maisha na matendo mema ni taaluma ya uongo na mtu kama huyo si Mkristo.

Sasa, ingawa mtindo wa maisha ya Wakristo wa kweli unaonyesha kuwapo kwa Kristo ndani ya mioyo yao, tunajua kuwa sisi sio wakamilifu. Wakristo hutenda dhambi na mtume Yohana anaiweka wazi kwamba tunajidanganya ikiwa tunafikiri vingenevyo (1 Yohana 1:8). Na wakati Wakristo wanatenda dhambi, kunao wale ambao hutamani kutumia “kuteleza” kwao ili kudhalilisha kundi lote la waumini. Ndio maana Paulo alilionya kanaisa la Thesalonike kujiepusha na hata uovu unaonekana (1 Wathesalonike 5:22) ni kuishi katika njia ambayo “wajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote (1 Wathesalonike 4:12).

Kile ambacho Wakristo hawapaswi kufanya ni kushiriki katika dhambi ya mara kwa mara au ya mazoea (1 Yohana 3:6). Mtu anayejihusisha na dhambi kimakusudi na kimazoea anathibitisha tu kwamba hamjui Kristo na kwa hiyo hawezi kukaa ndani Yake ingawa anaweza kuishi maisha yake chini ya mwavuli wa dini na kwa hivyo atafikiriwa na wengi kuwa yeye ni Mkristo.

Waumini wanapokomaa katika imani yao, wataonyesha ushahidi zaidi na zaidi wa asili yao ya kweli ya Kikristo, kama vile upendo wao kwa Mungu, toba kutoka kwa dhambi, kutengwa na ulimwengu, kukua kiroho, na kuishi kwa utiifu. Kama Paulo alivyowaambia Warumi, mtoto halisi wa Mungu amewekwa huru kutoka kwa dhambi na amekuwa mtumwa wa Mungu, na matokeo yake ni uzima wa milele (Warumi 6:22).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini kuna Wakristo bandia wengi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries