settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu alitupatia vitabu vinne vya Injili?

Jibu


Hapa kuna baadhi ya sababu Mungu alitoa Injili nne badala ya moja tu:

1) Kwa kutoa picha kamili ya Kristo. Wakati Biblia nzima ni pumzi ya Mungu (2 Timotheo 3:16), Alitumia binadamu kuwa waandishi na misingi tofauti na hadhi ya kutimiza malengo yake kwa njia ya maandishi yao. Kila waandishi wa injili alikuwa na kusudi tofauti nyuma ya injili yake na katika kutekeleza malengo hayo, kila mmoja alisisitiza masuala mbalimbali ya huduma ya Yesu Kristo.

Mathayo aliwaandikia watazamaji Kiebrania, na moja ya makusudi yake ilikuwa kuonyesha kutoka ukoo wa Yesu na kutimia kwa unabii wa Agano la Kale kwamba alikuwa Masihi iliyetarajiwa kwa muda, na kwa hivyo unapaswa uaminiwe. Mathayo mkazo wake ni kwamba Yesu ni mfalme wa ahadi, "Mwana wa Daudi," ambaye milele atakaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli (Mathayo 9:27; 21:9).

Marko, binamu yake Barnaba (Wakolosai 4:10), alikuwa mshahidi wa matukio katika maisha ya Kristo pamoja na kuwa na rafiki wa mtume Petro. Marko aliandika kwa ajili ya watu wa Mataifa, kama vile inavyoelezwa naye kwa kukosa mambo mhimu (Ukoo, mgongano wa Kristo na viongozi wa Kiyahudi wa wakati wake, kurejelea kwake katika Agano la Kale mara kwa mara) kwa Wayahudi wasomi wa nakala yake. Marko anasisitiza Kristo kama mtumishi mteswa, aliyekuja si kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kama fidia ya watu wengi (Marko 10:45).

Luka, "daktari mpendwa" (Wakolosai 4:14), mwinjilisti, na rafiki wa mtume Paulo, aliandika Injili ya Luka na matendo yote ya mitume. Luka ndie mwandishi pekee wa Mataif tu wa Agano Jipya. Yeye mwenyewe kwa muda mrefu amekuwa akikubalika kama mwana historia na wale ambao wametumia maandiko yake katika masomo ya nasaba na ya kihistoria. Kama mwanahistoria, anaeleza kwamba ni nia yake kuandika akaunti ya utaratibu ya maisha ya Kristo kutokana na ripoti ya wale ambao walikuwa mashahidi (Luka 1:1-4). Kwa sababu yeye hasa aliandika kwa ajili ya faida ya Theofilo, inaonekana baadhi ya watu wa Mataifa wa kimo, injili yake ilikuwa linatungwa na watu wa mataifa mengine watazamaji katika akili, na dhamira yake ni kuonyesha kuwa imani ya Kikristo ni msingi juu ya matukio ya kihistoria ya kuaminika na kuthibitishwa. Luka mara nyingi anamrejelea Kristo kama "Mwana wa Adamu," na kusisitiza ubinadamu wake, anashiriki maelezo mengi ambayo hayapatikani katika akaunti nyingine ya injili.

Injili ya Yohana , iliyoandikwa na Yohana mtume, ni tofauti na injili zingine tatu na ina maudhui mengi ya kitheolojia katika suala la utu wa Kristo na maana ya imani. Mathayo, Marko, na Luka zinajulikana kama "muhtasari wa Injili" kwa sababu ya mitindo wao sawa na maudhui na kwa sababu wanatoa muhtasari/vidokezo vya maisha ya Kristo. Injili ya Yohana haianzi na kuzaliwa kwa Yesu au huduma Yake ya kidunia bali kwa shughuli na tabia ya Mwana wa Mungu kabla afanyike mwanadamu (Yohana 1:14). Injili ya Yohana inasisitiza uungu wa Kristo, kama inavyoonekana katika matumizi yake ya maneno kama vile "Neno lilikuwa Mungu" (Yohana 1:1 ), "mkombozi wa ulimwengu" (Yohana 4:42), Mwana "wa Mungu " (hutumika mara kwa mara ), na " Bwana na ... Mungu"(Yohana 20:28). Katika injili ya Yohana, Yesu pia anathibitisha uungu wake na kadha wa "Mimi ni" Taarifa; mashuhuri zaidi miongoni mwao ni Yohana 8:58, ambayo Anaeleza kwamba "... Ibrahimu asijakuwako, mimi niko" (linganisha na Kutoka 3:13 -14). Lakini Yohana pia anasisitiza ukweli wa ubinadamu wa Yesu, wanataka kuonyesha makosa ya madhehebu ya dini ya siku zake, Agnostiki, ambao hawakuamini katika ubinadamu wa Kristo. Injili ya Yohana inaelezea kusudi lake kwa ujumla kwa ajili ya kuandika: "Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele ya wanafunzi wake, ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa jina lake" (Yohana 20:30-31).

Hivyo, kwa kuwa na nne tofauti na bado akaunti sawa na sahihi ya Kristo, masuala mbalimbali ya nafsi yake na huduma ni wazi. Kila akaunti inakuwa kama uzi wa rangi mbalimbali katika kitambaa kilichofumbwa pamoja na kuunda picha kamili zaidi ya huyu mmoja ambaye ni zaidi ya maelezo. Na wakati sisi kamwe sisi hatuwezi elewa kila kitu kuhusu Yesu Kristo (Yohana 20:30), kwa njia ya Injili nne tunaweza kumfahamu ya kutosha kuwa yeye ni nani na amefanya nini kwa ajili yetu ili tuweze kuwa na uzima kwa njia ya imani katika Yeye.

2) Kutuwezesha kuthibitisha ukweli wa lengo la akaunti zao. Biblia, kutoka nyakati za mwanzo, inasema kwamba hukumu katika mahakama ya sheria haikuwa ifanywe dhidi ya mtu kwa msingi ya ushahidi wa ushuhuda mtu mmoja bali wawili watatu kama idadi ya chini ya waliotakiwa (Kumbukumbu 19:15). Hata hivyo, baada ya kuwa na akaunti tofauti ya utu na huduma ya kidunia ya Yesu Kristo inatuwezesha kupima usahihi wa taarifa tunayo kumhusu Yeye.

Simioni Greenleaf, maarufu sana na amekubalika na mamlaka kwa maana ya ushahidi wa kuaminika katika mahakama ya sheria, alichunguza Injili nne kwa mtazamo wa kisheria. Alibainisha kuwa aina ya maelezo ya mashahidi imetolewa katika Injili zote nne – ni akaunti ambayo inaweza kutegemewa, yakujizimamia na inaweza kubalika katika mahakama ya sheria kwa ushahidi mkali. Vitabu vyote vine vingekua na ujumbe mmoja na maelezo sawa ya kina zote zimeandikwa kutoka kwa mtazamo mmoja, hiyo itaonyesha mgongano, kwa mfano kuwepo na muda wakati waandishi wote walikutana kabla ili “wapate hadithi zao moja kwa moja” ili wafanye uandishi wao kuwa wa sifa. Tofauti kati ya injili, hata utata dhahiri wa maelezo kwa uchunguzi wa kwanza, zungumza kwa asili huru ya maandishi. Hivyo, asili huru ya rekodi ya vitabu vine vya injili, zikikubaliana katika taarifa zao lakini tofauti katika mtazamo, kiasi ya undani, na ambayo matukio yalikuwa kumbukumbu, zinaonyesha kwamba rekodi tuliyo nayo ya maisha ya Kristo na huduma kama vile zimewasilishwa katika Injili ni sahihi na ya kuaminika.

3) Kuwazawadi wale wanaotafuta kwa bidii. Mengi yanaweza kupatwa kwa utafiti wa binafsi wa kila injili. Lakini bado mengi zaidi yanaweza kupatwa kwa kulinganisha akaunti tofauti tofauti ya matukio maalum ya huduma ya Yesu. Kwa mfano, katika Mathayo 14 tumepewa sababu ya kulisha watu 5000 na Yesu akitembea juu ya maji. Katika Mathayo 14:22 tunaambiwa kwamba "Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua na kwenda ngambo ya upande mwingine, wakati Yeye anauaga umati wa watu. "Mtu anaweza kuuliza, kwa nini hivyo? Hakuna sababu dhahiri iliotolewa katika Mathayo ya akaunti. Lakini wakati sisi tunaziweka pamoja na akaunti katika Marko 6, tunaona kwamba wanafunzi wamerudi kutoka kukemea mapepo na kuponya watu kupitia mamlaka Yeye alikuwa amewapa wakati aliwatuma wawili-kwa- wawili. Lakini wakarudi na "vichwa kubwa," wakisahau nafasi zao na akiwa tayari sasa kuwafundisha (Mathayo 14:15). Hivyo, katika kuwatuma nje majira ya jioni kwenda ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, Yesu anaonyesha mambo mawili kwao. Wanapo pambana na upepo na mawimbi, kwa kujitegemea wao wenyewe hadi masaa ya asubuhi na mapema ( Marko 6:48-50 ), wanaanza kuona kwamba 1) hawawezi kufikia kitu kwa Mungu katika uwezo wao wenyewe na 2) hakuna kitu chochote kigumu ikiwa wao watamwita na kuishi katika kutegemea nguvu zake. Kuna sura nyingi ziko na "vyombo" sawa zitakazo patikana na mwanafunzi makini wa neno la Mungu ambaye atachukua muda wake na kulinganisha maandiko kwa maandiko.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu alitupatia vitabu vinne vya Injili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries