settings icon
share icon
Swali

Ni mpangilio gani unapaswa kuwa wa vipaumbele katika familia zetu?

Jibu


Biblia haiweki utaratibu wa hatua kwa hatua kwa ajili ya uhusiano vipaumbele vya familia. Hata hivyo, sisi bado tunaweza kuangalia kwa maandiko na kuwa kanuni kwa jumla ya kipaumbele kwa uhusiano katika familia zetu. Mungu yuu wazi anakuja kwanza: Kumbukumbu 6:5, "Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote." Zote kwa moyo wa mtu, roho, na nguvu ni kuwa na bidii kwa kumpenda Mungu, na kufanya kuwa kipaumbele.

Kama wewe ni ndoa, mke/bwana wako anakuja baadaye. Mume aliyeoa anapaswa kumpenda mke wake kama Kristo alivyolipenda kanisa (Waefeso 5:25). Kipaumbele cha kwanza cha Kristo baada ya kutii na kumtukuza Baba ilikuwa ni kanisa. Huu ndio mfano mume anapaswa kufuata: Mungu kwanza, kwa njia sawia mke anapaswa kumheshim mume wake” kama vile kwa Bwana (Waefeso 5:22). Kanuni hii ni kwamba mume wa mwanamke ni wa pili kwa Mungu katika vipaumbele vyake.

Kama waume na wake ni wa pili kwa Mungu katika vipaumbele vyetu, na tangu mume na mke ni mwili mmoja (Waefeso 5:31), indhihiri ikisema kuwa matokeo ya uhusiano wa ndoa kwa ajili ya watoto unapaswa kuwa pili. Wazazi wanapaswa kulea watoto wamchao Mungu ambao watakuwa kizazi kijacho cha wale wamwitao Bwana kwa mioyo yao yote (Mithali 22:06, Waefeso 6:04), kuonyesha kwa mara nyingine tena kwamba Mungu anakuja wa kwanza. Mahusiano mengine yote ya familia lazima yaonyeshe hayo.

Kumbukumbu la Torati 5:16 inatuambia tuheshima wazazi wetu ili tupate kuishi kwa muda mrefu na hivyo mambo kutwendea vizuri. Hakuna kikomo maalum cha umri kimetajwa hapa ambayo itatufanya kuamini kwamba ili muradi tu wazazi wetu wako hai, lazima tuwaheshimu. Bila shaka, mara tu mtoto afikapo utu uzima, yeye hawajibiki tena kuwatii ("Watoto, watiini wazazi wenu ..."), lakini hakuna kikomo kwa umri wa kuwaheshimu. Tunaweza kuhitimisha kutokana na hili kwamba wazazi ni wa pili katika orodha ya vipaumbele baada ya Mungu, mume na mke wetu, na watoto wetu. Baada ya wazazi ndio wanakuja wengine wa familia moja (1 Timotheo 5:8).

Wa kufuatia katika orodha ya vipaumbele ni wanafamilia ya waamini wenzetu. Warumi 14 inatuambia tusihukumu au kuwadharau ndugu zetu (v. 10) au kufanya chochote kumsababisha Mkristo mwenzetu "kukwzwa" au kuanguka kiroho. Mengi ya kitabu cha 1 Wakorinto ni maagizo ya Paulo juu ya jinsi kanisa linatakiwa kuishi pamoja kwa amani, na kupendana. Mawaidha mengine yanayohuzisha ndugu na dada zetu katika Kristo ni "kuhudumiana kwa upendo" (Wagalatia 5:13); "Tena iweni wafadhili ninnyi kwa nyinyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasemehe ninyi" (Waefeso 4:32); "Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya" (1 Wathesalonike 5:11); na "tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri (Waebrania 10:24). Hatimaye wengine wote wa dunia wanakuja baadaye (Mathayo 28:19), ambao tutawaletea habari njema, na kuwafanya wanafunzi wa Kristo.

Kwa kumalizia, utaratibu wa maandiko matakatifu wa vipaumbele ni Mungu, mume/mke, watoto, wazazi, ndugu na jamaa, ndugu na dada katika Kristo, na kisha wengine wa dunia. Wakati mwingine maamuzi ni lazima yafanyike kuzingatia mtu mmoja baada ya mwingine, lengo ni kutopuuza uhusiano wetu wowote. Usawa wa Kibiblia ni kumruhusu Mungu kutujaza nguvu ili kutimiza vipaumbele vya uhusiano wetu, ndani na nje ya familia zetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni mpangilio gani unapaswa kuwa wa vipaumbele katika familia zetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries