settings icon
share icon
Swali

Ni nini baadhi ya vikwazo kwa maisha ya nguvu kimaombi?

Jibu


kizuizi cha wazi zaidi kwa ufanisi wa sala ni kuwepo na dhambi katika moyo wa mtu anayeomba ambayo haijaungamwa. Kwa sababu Mungu wetu ni Mtakatifu, kuna kizuizi huwapo baina yake na sisi wakati sisi huja kwake bila kuungama dhambi katika maisha yetu. "Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu; na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia" (Isaya 59:2) . Daudi alikubaliana, kwa kujua kutokana na uzoefu kwamba Mungu yu mbali na wale ambao hujaribu kuficha dhambi zao: "Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia" ( Zaburi 66:18 ).

Biblia inataja maeneo kadhaa ya dhambi ambazo ni kikwazo kwa ufanisi wa sala. Kwanza, wakati tunaishi kulingana na mwili, badala ya Roho, nia yetu ya kuomba na uwezo wetu wa kuwasiliana kwa ufanisi na Mungu huzuiliwa. Ingawa sisi hupokea asili mpya tunapozaliwa mara ya pili, kwamba asili hiyo mpya bado inaishi ndani ya mili yetu ya zamani, na kuwa katika "hema" ya zamani yenye uharibifu na ya dhambi. Mwili unaweza kupata udhibiti wa matendo yetu, mitazamo na nia ikiwa tutakuwa makini "kwa kuyafisha matendo ya mwili" (Warumi 8:13) na kuongozwa na Roho katika uhusiano sahihi na Mungu . Hapo ndipo sisi tutakuwa na uwezo wa kuomba kwa ushirika pamoja naye.

Moja ya njia ya kuishi katika mwili, inajidhihirisha katika ubinafsi, kizuizi kingine cha ufanisi wasala. Wakati maombi yetu ni ya msukumo wa ubinafsi, wakati tunamwomba Mungu chenye tunataka badala ya kile anataka, nia yetu huzuia sala zetu. "Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawaswa na mapenzi yake, atusikia" (1 Yohana 5:14). Kuuliza kulingana na mapenzi ya Mungu ni sawa na kuuliza katika kunyenyekea kwa kila mapenzi yake yanaweza kuwa, hata kama ikiwa tunajua au hatujui mapenzi ni gani. Katika mambo yote, Yesu anafaa kuwa mfano wetu katika maombi. Yeye daima huomba katika mapenzi ya Baba yake: "Walakini si mapenzi yangu bali yako yatendeke" (Luka 22:42). Sala za ubinafsi daima ni zile ambazo lengo lake ni kutosheleza matamanio yetu ya kibinafsi, na tusitarajie Mungu kujibu maombi hayo. "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu" (Yakobo 4:3).

Kuishi kulingana na ubinafsi, tamaa za mwili pia huzuia maombi yetu kwa sababu inazalisha ugumu wa moyo kwa wengine. Kama hatujali mahitaji ya wengine, tusitarajia Mungu kujali mahitaji yetu. Wakati tunaenda kwa Mungu katika maombi, haja yetu ya kwanza lazima iwe ni mapenzi yake. Pili lazima iwe ni mahitaji ya wengine. Hii inatokana na kuelewa kwamba tunawachukilia wengine kuwa bora kutuliko na kujali maslahi yao zaidi mbele yetu wenyewe (Wafilipi 2:3-4).

Kikwazo kikuu kwa ufanisi wa sala ni roho ya kutosamehe wengine. Wakati sisi hukataa kusamehe wengine, mzizi wa uchungu hukua katika mioyo yetu na kunyonga maombi yetu. Jinsi gani tunaweza kutarajia Mungu kutunyunyizia baraka zake tusisostahili sisi wenye dhambi tunapowe chuki na uchungu kwa wengine? Kanuni hii ni mfano mzuri katika mfano wa mtumishi asiye samehe katika Mathayo 18:23-35. Hadithi hii inafundisha kwamba Mungu ametusamehe madeni ambayo ni zaidi ya kipimo (dhambi zetu), na anatutarajia sisi kuwasamehe wengine vile tumekwisha samehewa. Kukataa kufanya hivyo huzuia sala zetu.

Kizuizi kingine kikubwa kwa ufanisi wa sala ni kutoamini na shaka. Hii haimaanishi vile wengine wanapendekeza kwamba kwa sababu sisi huja kwa Mungu tukiwa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu atajibu maombi yetu, Yeye kwa namna fulani anawajibika kufanya hivyo. Kuomba bila shaka ina maana kuwa kuomba katika imani salama na uelewefu wa tabia ya Mungu, asili, na nia. "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana mtu amwendaaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao " (Waebrania 11:6). Wakati tunakuja kwa Mungu katika maombi tukitia shaka tabia yake, kusudi, na ahadi, sisi tunamchukiza sana. Ujasiri wetu lazima uwe katika uwezo wake wa kujibu ombi lolote ambalo ni kwa mujibu wa mapenzi yake na madhumuni kwa maisha yetu. Tunapaswa kuomba kwa kuelewa kwamba chochote adhaminio ndio bora. "Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liliolochukuliwa na upeopo, na kupeperushwa huku n huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana"( Yakobo 1:6-7).

Hatimaye, ugomvi katika jamii ndio kikwazo kikuu kwa maombi. Petro hasa anataja hiki kama kizuizi kwa maombi ya mume ambaye mtazamo wake kwa mke wake sio wa uungu. "Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe" (1 Petro 3: 7). Wakati kuna mgogoro mkubwa katika mahusiano ya familia na kichwa cha boma haonyeshi nia Petro anataja, sala ya mawasiliano ya huyo mume na Mungu yanazuiliwa. Vile vile, wake wanapaswa kufuata kanuni za kibiblia za utii kwa uongozi wa waume zao ndio maombi yao yasizuiwe (Waefeso 5:22-24).

Kwa bahati nzuri, hizi kero zote za maombi zinaweza kushughulikiwa mara moja kwa kuja kwa Mungu katika maombi ya kukiri na toba. Tunahakikishiwa katika 1 Yohana 1:9 kwamba "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Pinid tu tumefanya hivyo, tunafurahia uwazi wa njia ya mawasiliano na Mungu, na maombi yetu hatasikika tu na kajibiwa, bali sisi pia tutajazwa na hisia za furaha.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Vikwazo vya sala ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries