settings icon
share icon
Swali

Vibainishi vya imani ni nini?

Jibu


Vibainishi vya imani ni muhtasari wa kauli za imani za kimsingi zinazoshikiliwa na watu binafsi, makanisa, au huduma. Zinaweka wazi ukweli muhimu ambao unaongoza kila aina ya imani na utendaji. Wakati mwingine vibainishi vya imani huitwa kauli mbiu ya mafundisho, kauli ya imani. Waumini katika enzi zote wametunga kauli hizi ambazo mara nyingi zimekaririwa kwa namna ya kanuni za imani. Mojawapo ya kibainishi cha imani cha kitambo kilielezewa katika Kumbukumbu 6:4-7: “Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.” Hii inajulikana kwa Wayahudi kama “shema,” na ndiyo msingi wa amri zote za Mungu. Inathibitisha umoja wa Mungu, ukuu wa Mungu na kipaummbele katika kumtumikia Mungu. Amri kumi ni sehemu nyingine ya nakala za hapo awali za imani.

Imani ya Kikristo ya mapema inamewekwa wazi katika 1 Wakorintho 15:1-4. “Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili. Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko.” Hiki kibainishi cha mani kinatangaza vile vya msingi kwa imani iokoayo katika Kristo. Kauli kama hizi huunda kitovu ambacho kwayo watu wanaweza jumuika na kuwa na umoja katika imani (1 Wakorintho 1:10).

Katika kanisa la Kwanza, ukuzaji wa kanuni za imani na vibainishi vya imani mara nyingi ulichochewa na kuongezeka kwa waalimu wa uongo. Kauli rahisi za imani zinakosa maelezo ya kina na kwa hivyo zinaruhusu tofauti kubwa katika matumizi yake. Mafundisho na desturi za kutiliwa shaka yalipotokea, viongozi wa makanisa walikusanyika kuchunguza Maandiko na kuweka wazi imani ya kweli ya kanisa. Mchakato huu unaonekana katika Matendo 15:1-29, ambapo baadhi ya walimu wengine walisema kwamba watu wa mataifa walipaswa kutahiriwa ili kuokolewa. Mitume na wazee katika Yerusalemu walikutana na kujadili suala hilo na wakaandika barua ili kuyajulisha makanisa kwamba kufuata Sheria ya Musa haikuhitajika ili kupata wokovu. Kanuni ya imani ya Mitume, kanuni ya Nikea, na nyinginezo ziliundwa kukabilana na changamoto sawia na za imani illiyokubalika.

Leo hii vibainishi vingi vya imani vimepangwa kulingana na mada, wakiorodhesha vitengo vya msingi vya mafundisho na kufuatisha maelezo ya kufaa hapo chini. Baadhi ya mada muhimu ambazo kwa kawaida hujumuishwa katika vibainishi vya Kikristo vya imani ni: mafundisho ya Biblia, mafundisho ya Mungu, mafundisho ya tamaduni za binadamu, mafundisho ya dhambi, mafundisho ya Kristo, mafundisho ya wokovu, mafundisho ya Roho Mtakatifu, mafundisho ya kanisa, mafundisho ya nyakati za mwisho. Katika kila moja ya vitengo hivi kuna vitengo vidogo, na makanisa hutofautiana sana juu imani yao katika kila kitengo. Wakati mwingine vibainishi vya imani huandikwa kwa njia rahisi sana, na vinaruhusu wigo pana ya imani, na wakati mwingine vibainishi hivi ni vya kina sana, ili kupunguza upeo wa imani na desturi zinazokubalika.

Historia ya kanisa imetufundisha kwamba kadri vibainishi vya imani vinavyokuwa wazi na vya jumla ndivyo mafundisho ya uwongo yanavyotokea na kupata msingi. Historia imetufunza kuwa haijalishi nakala za imani zinasema nini, kimsingi hazina maana isipokuwa zinajulikana na kufuatwa na makanisa na watu binafsi. Hapo zamani ilikuwa kawaida kwa waumini kukariri mtungo wa mafundisho kwa namna ya majibizano (catechism) na kanuni za imani, zikiwapa msingi dhabiti wa kuchunguza mawazo mapya. Leo hii, mwelekeo uliopo unaonekana kuwa uwazi au ukosefu wa maarifa kuhusu maandiko. Wakristo wengi watalazimishwa kuonyesha kile wanachoamini kwa undani, na matokeo ni viraka mbalimbali vya imani ambayo wakati mwingine yanakanganya. Neno la Mungu linatuambia, “jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema” (1 Wathesalonike 5:21). Hii inamaanisha mambo na kuhakikisha yako sahihi ili ujue ikiwa utayapokea au utayakataa. Hii ndio ilisababisha kanuni za imani na vibainishi vya imani katika nyakati zilizopita, ni ndio kitu kitatusaidia kujua chenye tunaamini na ni kwa nini tunakiamini hii leo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Vibainishi vya imani ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries