settings icon
share icon
Swali

Uwazi wa Uungu ni nini?

Jibu


"Uwazi wa Uungu," pia inajulikana kama "theolojia wazi " na "uwazi wa Mungu," ni jaribio la kuelezea maarifa ya Mungu katika uhusiano na hiari ya mtu. Hoja ya dhana ya uwazi wa Mungu kimsingi ni hii: binadamu kwa kweli wako huru; kama Mungu alijua kabisa baadaye, kuwa binadamu hangeweza kweli kuwa huru. Kwa hivyo, Mungu hajui kabisa kila kitu kuhusu hali ya baadaye. Uwazi wa Uungu unashikilia kwamba baadaye haijulikani. Kwa hiyo, Mungu anajua kila kitu ambacho kinaweza kujulikana, lakini Yeye hajui siku zijazo.

Uwazi wa Uungu waweka imani hizi juu ya vifungu vya maandiko ambayo huelezea Mungu "akibadilisha mawazo yake" au "kushangazwa" au "akionekana kupata elimu" (Mwanzo 6:6; 22:12, Kutoka 32:14; Yona 3:10). Katika mwanga wa wengi maandiko mengine kwamba hutangaza maarifa ya Mungu ya baadaye, maandiko haya lazima yaeleweke kama Mungu kujielezea mwenyewe katika njia ambazo tunaweza kuelewa. Mungu anajua matendo yetu na maamuzi yatakuaje, lakini Yeye "hubadilisha akili yake" kuhusiana na matendo yake ya msingi juu ya matendo yetu. Chukizo laa Mungu katika uovu wa binadamu haumaniishi Yeye hakuwa na ufahamu kuwa itatokea.

Kinyume na uwazi wa Uungu, Zaburi 139:4, 16 yasema, "Maana hamna neon ulimini mwangu, usilolijua kabisa, Bwana ... siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado." Ni jinsi gani Mungu anaweza kutabiri maelezo kwa kina katika Agano la Kale juu ya Yesu Kristo kama yeye hajui siku za baadaye? Jinsi gani Mungu kwa namna yoyote angeweza kuhakikisha wokovu wetu kama Yeye hajui chenye kitakachokuwa wakati ujao?

Hatimaye, uwazi wa Uungu unashindwa katika majaribio ya kuelezea yasiyoelezeka-uhusiano kati ya maarifa ya Mungu na mapenzi huru ya mwanadamu. Kama vile tu aina ya Ukalvini unashindwa, kiwango wanafanya binadamu kama muigizo uliotegwa kabla, hivyo uwazi wa Uungu unashindwa kwa kuwa unakataa utu wa kweli na uhuru wa Mungu. Mungu lazima aeleweke kwa njia ya imani, kwa kuwa "bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu" (Waebrania 11:6 a). Uwazi wa Uungu hivyo, si wa maandiko. Ni njia nyingine kwa mwanadamu aliye na mwisho kujaribu kuelewa Mungu asiye na mwisho. Uwazi wa Uungu lazima ukataliwe na wafuasi wa Kristo. Wakati uwazi wa Uungu ni maelezo ya uhusiano kati ya maarifa ya Mungu na uhuru wa binadamu, si maelezo ya Biblia.


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uwazi wa Uungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries