settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje kuhusu subira?

Jibu


Wakati kila kitu kinaenda njia yetu, uvumilivu ni rahisi kuonyesha. Mjarabu wa kweli wa uvumilivu unakuja wakati haki zetu zimekiukwa - wakati gari limetupita kwenye trafiki; wakati tunapofanyiwa isivyo haki; wakati wafanyakazi wenzetu wanakejeli imani yetu, tena. Baadhi ya watu wanadhani wana haki ya kutamauka katika uso wa kukasirika na majaribu.kutovumilia kunaonekana kama hasira takatifu. Lakini tunda la roho ni upendo, furaha ,amani ,uvumilivu ,utu wema ,fadhili ,uaminifu (Wagalatia 5:22) ambayo inapaswa kuzalishwa kwa ajili ya wafuasi wote wa Kristo (1 Wathesalonike 5:14).Uvumilifu unaonyesha imani yetu kwa majira ya Mwenyezi Mungu , na upendo.

Ingawa watu wengi wanachukulia uvumilivu kuwa kusubiri kimyakimya au stahamala pole, zaidi ya maneno ya Kigiriki yaliyotafsiri "uvumilivu" katika Agano Jipya ni tendaji, maneno imara.Chukulia kwa mfano Waebrania 12: 1: "Basi na sisi pia,kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii,na tuweke kando kila mzigo mzito ,na dhambi ile ituzingayo kwa upesi ; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu "(NKJV). Je, mtu hukimbia kwa shindano kwa kusubiri kimyakimya msukumo wa polepole au waongo wavumilifu?Kwa hakika sivyo! Neno lililotafsiriwa "uvumilivu" katika mstari huu linamaanisha "ustahimilifu." Mkiristo anakimbia kwa shindano akiwa mvumilifu kwa kusitahimili kwa matatizo. Katika Biblia, uvumilivu ni kudumu kuelekea kwa lengo, kuvumilia majaribu, au kwa kutarajia ahadi kutimizwa.

Uvumilivu haukui kwa usiku mmoja. Nguvu za Mungu na wema ni muhimu kwa ukuaji wa uvumilivu. Wakolosai 1:11 inatuambia kwamba tunatiwa nguvu na Yeye kwa "uvumilivu mkubwa na subira, "ilhali Yakobo 1: 3-4 inatutia moyo ili tujue kwamba majaribio ni njia yake ya kukamilisha uvumilivu wetu. Uvumilivu wetu unaendelezwa zaidi na kutiwa nguvu kwa kutulia katika mapenzi kamili ya Mungu, hata katika uso wa watu waovu ambao "Ukae kimya mbele za Bwana, nawe umngojee kwa saburi; usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake ,wala afanyaye hila." (Zaburi 37: 7). Uvumilivu wetu utalipiwa mwisho "kwa sababu kuja kwa Bwana kuko karibu" (Yakobo 5: 7-8). "Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtfutayoa" (Maombolezo 3:25).

Tunaona katika Biblia mifano mingi ya wale ambao uvumilivu wao ulitambulisha kutembea kwao na Mungu.Yakobo anatuelekeza kwa manabii. Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya,na wa uvumilivu. (James 5:10). "Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana mwingi wa rehema ,mwenye huruma." (Yakobo 5:11 ). Ibrahimu, pia, alisubiri kwa uvumilivu na "kupokea kile kilichoahidiwa" (Waebrania 6:15). Yesu ni mfano wetu wa kuiga katika mambo yote, na alionyesha uvumilivu wa kudumu: "tukimtazama yesu , mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu ;ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu ,naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” (Waebrania 12: 2).

Ni kwa jinsi gani sisi huonyesha uvumilivu utokanao na tabia ya Kristo? Kwanza, tunamshukuru Mungu. Kwa kawaida marudio ya kwanza ya mtu huwa ni "mbona mimi?", Lakini Biblia inasema tufurahi katika mapenzi ya Mungu (Wafilipi 4: 4; 1 Petro 1: 6). Pili, tunatafuta kusudi lake. Wakati mwingine Mungu anatuweka katika hali ngumu ili tuweze kuwa shahidi. Mara nyingine, aweza kuruhusu jaribio kwa ajili ya kutakaza tabia. Tukikumbuka kwamba kusudi lake ni kwa ukuaji wetu na utukufu wake utatusaidia katika jaribio hilo. Tatu,tunakumbuka ahadi zake kama vile Warumi 8:28, ambayo inatuambia kwamba "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake." "Katika mambo yote" ni pamoja na mambo ambayo hujaribu uvumilivu wetu.

Wakati utakaokuwa kwenye msongamano wa magari, kusalitiwa na rafiki, au dhihaka kwa ushuhuda wako, ni jinsi gani utaweza kujibu?Jibu la kawaida ni kutokuwa na uvumilivu ambao utapelekea kuwa na mawazo , hasira na kukatisha tamaa. Sifu Mungu kwamba, kama Wakristo,hatushirikishwi kamwe na "mwitikio wa asili" kwa sababu sisi ni viumbe vipya katika Kristo mwenyewe (2 Wakorintho 5:17). Badala yake, tuna nguvu za Bwana ya kujibu kwa uvumilivu na katika imani kamili katika nguvu na lengo Baba. Wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima nakutokuharibika ,watapewa uzima wa milele;" (Warumi 2: 7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje kuhusu subira?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries