settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anahitaji Wakristo waitunze Sabato?

Jibu


Katika Wakolosai 2:16-17, mtume Paulo anatangaza, "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo" Vile vile, Warumi 14:5 yasema, "Mtu mmoja afanya tafauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe." Maandiko haya huiweka wazi kwamba, kwa Mkristo, Sabato ni suala la uhuru wa kiroho, si amri kutoka kwa Mungu. Sabato ni suala ambalo neno la Mungu linatufundisha tusihukumu kila mmoja. utunzaji sabato ni jambo ambalo kila Mkristo anahitaji kushawishiwa kikamilifu katika akili yake mwenyewe.

Katika sura za mwanzo wa kitabu cha Matendo, Wakristo wa kwanza wengi walikuwa Wayahudi. Watu wa mataifa mengine walianza kupokea zawadi ya wokovu kwa njia ya Yesu Kristo, Wakristo wa Kiyahudi walikuwa na tatizo. Ni mambo gani ya Sheria ya Musa na desturi za Wayahudi Wakristo wa Mataifa wanaelekezwa kutii? Mitume walipokutana na kujadili suala katika baraza la Yerusalemu (Matendo 15). Uamuzi ulikuwa, "Kwa sababu hiyo mimi naamua hiv; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika mataifa; bali twaandikie kwam wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu" (Matendo 15:19-20). Kutunza Sabato ilikuwa mmojawapo ya amri mitume waliona kuwa si muhimu kuwalazimshia watu wa Mataifa waamini. Haidhaniwi kwamba mitume, wangeacha kujumlisha utunzaji sabato kama ilikua amri ya Mungu kwa ajili ya Wakristo kuitunza siku ya Sabato.

Makosa ya kawaida katika mjadala wa kutunza sabato ni dhana kuwa Sabato ilikuwa siku ya ibada. Makundi kama vile Wasabato hushikilia kwamba Mungu anahitaji ibada ya kanisa kufanyika siku ya Jumamosi, siku ya Sabato. Hiyo sio kile amri ya Sabato ilikuwa. Amri ya Sabato ilikuwa bila kufanya kazi siku ya Sabato (Kutoka 20:8-1). Hakuna mahali popote katika maandiko siku ya Sabato aliagizwa kuwa siku ya ibada. Ndio, Wayahudi katika Agano la Kale, Agano Jipya, na nyakati za kisasa hutumia Jumamosi kama siku ya ibada, lakini hiyo siyo kiini cha amri ya Sabato. Katika kitabu cha Matendo, wakati wowote mkutano alisemakana kuwa siku ya Sabato, ni mkutano wa Wayahudi, si Wakristo.

ni lini Wakristo wa kwanza walikutana? Matendo 2:46-47 inatupa jibu, "Na siku zote kwa moy mmoja walidumu dnani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyma, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moy wmeupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana aklizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa" Kama kuna siku wakristo walikuwa wakikutana mara kwa mara, ilikuwa ni siku ya kwanza ya wiki (Jumapili yetu), si siku ya Sabato (Jumamosi yetu) (Matendo 20: 7, 1 Wakorintho 16:2). Kwa heshima ya ufufuo wa Kristo siku ya Jumapili, Wakristo wa kwanza waliitunza Jumapili si kama "Sabato ya Kikristo" lakini kama siku ya ibada hasa ya Yesu Kristo.

Je, kuna ubaya wowote wa kuabudu siku ya Jumamosi, Sabato ya Wayahudi? La hasha! Tunapaswa kumwabudu Mungu kila siku, si tu Jumamosi au Jumapili! Makanisa mengi leo hii yana ibada ya Jumamosi na Jumapili. Kuna uhuru katika Kristo (Warumi 8:21; 2 Wakorintho 3:17, Wagalatia 5:1). Je, Mkristo anafaa kutunza Sabato, yaani, hafanyi kazi Jumamosi? Kama Mkristo anahisi kuongozwa kufanya hivyo, naam na afanye hivyo (Warumi 14:5). Hata hivyo, wale huchagua kutunza Sabato haiwapaswi kuwahukumu wale ambao hawatunzi siku ya Sabato (Wakolosai 2:16). Zaidi ya hayo, wale ambao hawatunzi Sabato lazima waepuke kuwa kikwazo (1 Wakorintho 8:9) kwa wale ambao wanaitunza Sabato. Wagalatia 5:13-15 yatoa muhtasari wa suala zima: "Maana nyinyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anahitaji Wakristo waitunze Sabato?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries