settings icon
share icon
Swali

Jinsi gani Mkristo anapaswa kushughulikia utasa?

Jibu


Tatizo la utasa linaweza kuwa mojawapo ngumu sana, hasa kwa wanandoa ambao wametafuta watoto katika maisha yao yote. Wanandoa Wakristo wanaweza kujikuta wakiuliza "Kwa nini ni sisi, Bwana?" Kwa kweli Mungu anataka Wakristo kubarikiwa na watoto kwa upendo na malezi. Kwa wapenzi wenye afya kimwili, moja ya masuala yanayoumiza moyo ni kukosa kujua kama utasa ni hali ya muda mfupi au wa kudumu. Kama ni muda, ni kwa muda gani wanapaswa kusubiri? Kama ni wa kudumu, ni jinsi gani wao hujua hilo na ni hatua gani wanapaswa kuchukua?

Biblia inaonyesha tatizo la utasa wa muda katika hadithi kadhaa:

Mungu aliwahidi Abramu na Sara mtoto, lakini yeye hakuzaa mtoto Isaka, mpaka umri wa 90 (Mwanzo 11:30).

Isaka, mume wa Rebeka, alisali kwa bidii, na Mungu akamjibu, iliopelekea kuzaliwa kwa Yakobo na Esau (Mwanzo 25:21).

Raheli aliomba, na hatimaye Mungu "akafungua tumbo yake." Alizaa wana wawili wa kiume, Yusufu na Benyamini (Mwanzo 30:1; 35:18).

Mkewe Manoa, aliyekuwa tasa kwa wakati, akajifungua Samsoni (Waamuzi 13:2).

Elizabeti katika umri wake wa miaka akajifungua Yohana Mbatizaji, mtangulizi wa Kristo (Luka 1:7, 36).

Utasa wa Sara, Rebeka, na Raheli (wamama wa taifa la Israeli) ni wa umuhimu kuwa na uwezo hatimaye wa kuzaa watoto ilikuwa ni ishara ya neema na kibali cha Mungu. Hata hivyo, wanandoa tasa wasidhani kwamba Mungu anazuia neema yake na kibali, wala wao kudhani kuwa wanaadhibiwa kwa namna fulani. Wanandoa Wakristo lazima wayashike maarifa kwamba dhambi zao zimesamehewa katika Kristo na kwamba kukosa uwezo wa kuwa na watoto si adhabu kutoka kwa Mungu.

Hivyo basi ni nini mwanandoa Mkristo ambaye ni tasa anastahili kufanya? Ni vizuri kutafuta ushauri kutoka kwa madaktari na wataalamu wengine wa uzazi. Wanaume na wanawake wanapaswa kuishi maisha bora kujiandaa kwa ajili ya mimba. Wamama wa taifa la Israeli waliomba bila kukoma kwa ajili ya mimba, hivyo kuendelea kuomba kwa ajili ya mtoto hakika hakuko nje ya mstari. Kimsingi, ingawa, tunapaswa kuomba kwa ajili ya mapenzi ya Mungu kwa maisha yetu. Kama mapenzi yake ni tuzae watot wetu wa asili, tutazaa. Kama mapenzi yake ni kwamba tuasili, kuwa mzazi wa kambo, au kuwa bila mtoto, basi hicho ndicho tunapaswa kukubali na kujitoa kwa furaha kufanya. Tunajua kwamba Mungu ana mpango wa uungu kwa kila mpendwa wake. Mungu ndiye mwanzilishi wa maisha. Yeye anaruhusu mimba na kuzulia mimba. Mungu ndiye mwenye mamlaka na ana hekima yote na maarifa (Warumi 11:33-36). "Kila kipaji chema na kamilifu hutoka juu ..." (Yakobo 1:17). Kujua na kukubali ukweli huu kutaenda hadi kujaza mioyo ya wanandoa tasa iliyo na machungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Jinsi gani Mkristo anapaswa kushughulikia utasa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries