settings icon
share icon
Swali

Je, ni namna gani tunapaswa kuishi maisha yetu kulingana na utambulisho wetu katika Kristo?

Jibu


Utambulisho wetu katika Kristo kwanza kabisa na sana sana ni mojawapo ya upya. Sisi ni viumbe vipya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17). Utambulisho umefafanuliwa kama “sehemu ya upamoja ya kundi la sifa ambazo kwayo kitu kinaweza kutambulika au kujulikana,” kwa hivyo utambulisho wetu mpya katika Kristo unapaswa kutambulika kwetu na kwa wengine. Ikiwa tuko “ndani ya Kristo,” hilo lapaswa kuwa wazi, kama vile kuwa katika “ulimwengu” vile vile uu wazi. Fafanuzi zaidi ya utambulisho ni “kiwango au hali ya kuwa sawa kama kitu kingine kile.” Katika suala la utambulisho wetu katika Kristo, maisha yetu yanapaswa kuonyesha kwamba sisi tunafanana na Kristo. Jina “Wakristo” hasa linamaanisha “wafuasi wa Kristo.”

Katika utambulisho wetu mpya katika Kristo, sisi si watumwa wa dhambi tena (Warumi 6:6), lakini tumepatanishwa na Mungu (Warumi 5:10). Utambulisho huu mpya hubadilisha kabisa uhusiano wetu na Mungu na família zetu, kama vile unavyobadilisha jinsi tunavyouona ulimwengu. Utambulisho wety mpya katika Kristo unamaanisha kuwa tuna uhusiano sawa na Mungu ambao Kristo anao-sisi ni watoto Wake. Mungu ametufanya kuwa wana Wake. Tunaweza kumwita “Abba! Baba!” (Warumi 8:15-16). Sisi sote ni warithi pamoja naye (Wagalatia 3:29) na marafiki (Yohana 15:15) wa Kristo. Na uhusiano huu una nguvu zaidi kuliko ule tulio nao na familia zetu za kidunia (Mathayo 10:35-37). Badala ya kumwogopa Mungu kama hakimu, tuko na bahati kubwa sana ya kuja Kwake kama Baba yetu. Tunaweza kumwendea kwa ujasiri na kumwomba kile tunachohitaji (Waebrania 4:16). Tunaweza kuomba mwongozo na hekima Yake (Yakobo 1:5) na kujua kwamba hakuna kitu kitakachotuchukua kutoka kwake (Warumi 8:38-39). Pia tunapumzika katika mamlaka yake na kumjibu kwa utiivu wa tumaini, tukijua kwamba utiivu ndio sehemu kuu ya kubaki karibu naye (Yohana 14:23).

Familia ya Mungu inajumuisha kundi kubwa la waumini wanaojitahidi pamoja kukua karibu na Mungu (1 Wakorintho 12:13). Ni familia ambayo ina nguvu zaidi kwa karama za kila mtu ndani yake (Warumi 12:6-8). Washirika wa hii familia mpya hutatufa yaliyo bora zaidi kila mmoja wao (1 Wakorintho 10:24), kutiana moyo (Wagalatia 6:1-2), na kusameheana (Mathayo 18:21-22). Zaidi ya yote, tunaitikiana mmoja kwa mwingine kwa upendo-sio kwa hisia, lakini tendo la kujitolea lisilo na ubinafsi, ambalo linaakisi upendo wa agape wa Mungu ambaye alitupenda na kujitioa kwa ajili yetu (Wagalatia 2:20).

Sisi sio raia wa ulimwengu tena bali sehemu yake (2 Wakorintho 6: 14-7:1). Tunaelewa kwamba sisi ni sehemu ya ufalme wa mbinguni unaotawaliwa na Mungu. Mambo ya dunia hayatuvutii tena (Wakolosai 3:2). Hatuogopi au kusisitiza kupita kiasi mateso humu duniani au majaribu tunakumbana nayo (Wakolosai 1:24; 1 Petro 3:14; 4:12-14), wala hatuweki umuhimu kwa vitu ambavyo ulimwengu huthamini (1 Timotheo 6:9-11). Hata miili yetu na matendo yetu yanaonyesha kwamba akili zetu hazifanani tena na ulimwengu (Warumi 12:1-12). Lakini sasa ni vyombo vya haki kwa Mungu (Warumi 6:13). Na mtazamo wetu mpya wa ufalme unamaanisha tunaelewa kwamba adui yetu si watu wanaotuzunguka bali nguvu za kiroho ambazo zinajitahidi kuwazuia watu kutokana na kumjua Mungu (Waefeso 6:12).

Haya yote ni bora- tabia ya mfuasi mkomavu wa Kristo. Mojawapo ya baraka kuu kuhusu utambulisho wetu katika Kristo ni neema tunayopewa ili kukua hadi kufikia ukomavu wa kiroho unaokisi utambulisho wetu mpya (Wafilipi 1:6). Maisha yetu kwa mjibu wa utambulisho wetu katika Kristo yamejawa na Baba wetu wa mbinguni, familia kubwa yenye upendo, na kuelewa kwamba sisi ni raia wa ufalme mwingine na si wa dunia hii.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni namna gani tunapaswa kuishi maisha yetu kulingana na utambulisho wetu katika Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries