settings icon
share icon
Swali

Kwa nini usingizi au kulala ni muhimu? Kwa nini Mungu alituumba tukiwa na hitaji ya kulala?

Jibu


Kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu, alituumba pia na hitaji ya kulala. Biblia inataja usingizi kwa mara ya kwanza katiaka Mwanzo 2:21 wakati Mungu alimfanya Adamu kulala usingizi mzito na kumuumba Hawa kutoka kwa ubavu wake. Mungu aliumba dhana ya kupumzika katika uumbaji wake (Mwanzo 2:2). Aliweka utaratibu wa kupumzika wakati alitenga siku ya Sabato kwa ajili ya Wayahudi (Kutoka 31:16; Walawi 23:3).

Biblia inazungumza kuhusu usingizi kwa njia nzuri na mbaya pia. Wakati mwingine usingizi unaelezewa kuwa zawadi kutoka kwa Mungu katika vifungu kama vile Mithali 3:24 na Zaburi 4:8. Tunajua kwamba kulala ni sehemu ya kuwa mtu mwenye afya nzuri kwa sababu Yesu alilala kama tunavyolala (Luka 8:23; Marko 1:35). Wakati mwingine Yesu alizungumza na watu kupitia kwa ndoto na maono walipokuwa wanalala (Mwanzo 20:3; 31:24; 1 Wafalme 3:5; Danieli 7:1). Hata hivyo, usingizi unaweza kutumiwa vibaya, kama vile zawadi zingine kutoka kwa mungu. Mistari kama Mithali 6:9, 19:15, 20:13, na 24:33 inaashiria uvivu kuwa usingizi.

Kuna nadharia nyingi za kisayansi na za ajabu zinazoeleza kwa nini sisi hulala. Utafiti unaonyesha mabadiliko ya tabia yanayotokea wakati tonakosa usingizi, lakini sayansi haiwezi kujibu swali “ni kwa nini?” Inawezekana kuwa sababu moja ya kuhitaji kwetu kwa usingizi ni kwamba usingizi hutukumbusha kwamba sisi ni viumbe wala sio Muumba. Miili yetu lazima ijazwe mara kwa mara na chakula, maji, oksijeni, na usingizi ndiposa iendelee kufanya kazi. Kukidhi mahitaji haya inachukuwa mud ana nguvu zetu nyingi. Tunahitaji kukumbushwa daima kuhusu upungufu wetu na kwamba tunamtegemea Mungu maishani. Hitaji la kimwili ni ukumbusho kama huo.

Usingizi pia huruhusu akili zetu kupumzika ili tuweze kuwa waangalifu tunapoamka. Akili zetu ni sawa na tarakilishi, zenye uwezo wa kuhifadhi, kumbukumbu, na uwezo ambao hajatumika bado. Lakini zinaweza kukosa kufanya kazi vizuri ikiwa hazijatunzwa vizuri. Kama vile tarakilishi inahitaji kuwashwa upya mara kwa mara inavyotumika sana, akili zetu pia zinahitaji kuwashwa upya kwa kulala vizuri. Mara nyingi Maandiko yanarejelea kukutana na Mungu asubuhi (Isaya 50:4, Kutoka 34:2; Zaburi 5:3). Mungu pia anatuahidi kuwa huruma zake ni mpya kila asubuhi (Maombolezo 3:23), maana kuwa baada ya usingizi mzuri usiku tunahitaji kumwita Mungu atupe uwezo kwa ajili ya siku hiyo.

Usingizi mzuri mara nyingi umetajwa kuwa zawazi kutoka kwa Mungu (Walawi 26:6; Zaburi 4:8), huku kuzungukazunguka kwa kitanda inaonekana kwamba ni dhamiri yenye hatia au woga (Zaburi 6:6; 77:4). Haijalishi ni kwa nini Mungu alituumba tukiwa na hitaji ya kulala lakini tunamshukuru kwamba yeye hukidhi hitaji yoyote tulilo nalo (Wafilipi 4:19). Alituumba na mahitaji na upungufu ili tukumbuke mara kwa mara jinsi tunavyomhitaji. Ukumbusho huo unatufanya tuwe na shukrani na wanyenyekevu, sifa mbili zinazohitajika kabla kuishi katika uwepo wa Mungu ( Yakobo 4:6; Zaburi 95:2).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini usingizi au kulala ni muhimu? Kwa nini Mungu alituumba tukiwa na hitaji ya kulala?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries