settings icon
share icon
Swali

Agano Jipya linasema nini kuhusu ushoga?

Jibu


Biblia inathibitisha katika Agano la Kale na Jipya kwamba ushoga ni dhambi (Mwanzo 19:1–13; Walawi 18:22; 20:13; Warumi 1:26–27; 1 Wakorintho 6:9; Yuda 1:7). Katika suala hili, Agano Jipya linasisitiza kile ambacho Agano la Kale lilitangaza tangu Sheria iliyotolewa kwa Musa (Walawi 20:13). Tofauti kati ya Agano la Kale na Jipya ni kwamba Agano Jipya linatoa tumaini na urejesho kwa wale walionaswa katika dhambi ya ushoga kupitia nguvu ya ukombozi ya Yesu. Ni tumaini lile lile linalotolewa kwa yeyote anayechagua kukubali (Yohana 1:12; 3:16–18).

Viwango vya utakatifu vya Mungu havikuweza kubadilika kwa kuja kwa Yesu, kwa sababu Mungu habadiliki (Malaki 3:6; Waebrania 13:8). Agano Jipya linaendelea kufunua mwingiliano wa Mungu na wanadamu. Mungu alichukia ibada ya sanamu katika Agano la Kale (Kumbukumbu la Torati 5:8), naye bado anaichukia katika Agano Jipya (1 Yohana 5:21). Kile kilichokuwa kibaya katika Agano la Kale bado ni kibaya katika Agano Jipya.

Agano Jipya linasema kwamba ushoga ni “tamaa ya aibu” (Warumi 1:26), “tendo la aibu,” kuachana na “mahusiano ya asili” (Warumi 1:27), “kosa” (1 Wakorintho 6:9), na “uasherati na upotovu wa kijinsia” (Yuda 1:7). Ushoga una “adhabu inayostahili” (Warumi 1:27), “ni kinyume cha mafundisho yenye uzima” (1 Timotheo 1:10), na umeorodheshwa miongoni mwa dhambi zinazowazuia watu kuingia katika ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9). Licha ya majaribio ya wengine kupunguza aya hizi, Biblia haiwezi kuwa wazi zaidi kwamba ushoga ni dhambi dhidi ya Mungu.

Ushoga sio sababu ya kuanguka kwa jamii, lakini ni dalili yake; ni matokeo ya watu kujifanya mamlaka ya mwisho. Warumi 1 inatoa mwendo wa asili wa jamii ambayo imechagua ibada ya sanamu na raha ya dhambi badala ya utii kwa Mungu. Kuanguka huanza kwa kukana kwamba Mungu ana mamlaka kamili juu ya uumbaji wake (Warumi 1:21-23).

Matokeo ya jamii kukataa utawala wa Mungu katika maisha yao ni kwamba Mungu “aliwaacha katika tamaa zao za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao, kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele” (Warumi 1:24-25). Mistari ya 26 na 27 inasema, “Kwa sababu hiyo, Mungu aliwaacha tamaa za aibu. Hata wanawake wao walibadilisha mahusiano ya kawaida ya kijinsia na yasiyo ya kawaida. Vivyo hivyo wanaume pia waliacha mahusiano ya kawaida na wanawake na kuwaka na tamaa kwa wengine. Wanaume walifanya matendo ya aibu na wanaume wengine, na wakapokea ndani yao adhabu inayostahili kwa kosa lao.” Maneno “Mungu aliwaacha” inamaanisha kwamba, tunaposisitiza kutikisa ngumi zetu kwa Mungu, hatimaye anaturuhusu kuwa na upotovu tunaodai. Na hiyo ni hukumu yenyewe. Tabia ya ushoga ni matokeo ya kumpuuza Mungu na kujaribu kuunda ukweli wetu wenyewe.Tunapopinga maagizo ya Mungu yaliyo wazi, tunavuna “adhabu stahiki” ya kutotii kwetu (2 Wathesalonike 1:8–9; Ufunuo 21:8).

Habari njema ni kwamba ushoga sio dhambi isiyosameheka. Inaweza kusamehewa kama vile uchoyo, wizi, na mauaji yanaweza kusamehewa tunapojuta na kumgeukia Yesu (Matendo 2:38). Anatupa utambulisho mpya (1 Petro 1:14; Wakolosai 2:13). 2 Wakorintho 5:17 inasema kwamba “mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya!” Mambo hayo ya “zamani” yanajumuisha dhambi za zamani ambazo ziliwahi kutufunga. Ingawa hapo awali tulifafanuliwa na dhambi zetu, kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:3) kunamaanisha kwamba sasa tumefafanuliwa na Yesu na haki yake (Wakolosai 3:3). Mwizi haitaji tena kujiita mwizi. Amesafishwa kutoka kwa njia zake za zamani na kufanywa mpya katika Kristo. Muuaji—kama vile Sauli kabla ya kuwa mtume Paulo—amesamehewa na kufanywa mfano wa Kristo (Wagalatia 1:13; 1 Wakorintho 15:9; Warumi 8:29). Na mtu yeyote aliyenaswa katika ushoga anaweza kuwekwa huru kutembea katika usafi wakati yeye anakubaliana na Mungu kuhusu dhambi na anaamini uwezo Wake wa kusamehe na kurejesha.

Kama ilivyoelezwa, 1 Wakorintho 6:9-10 inajumuisha mashoga katika orodha ya wale ambao hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini mstari wa 11 unaendelea kusema, “Na watu kama hao ndivyo mlivyokuwa baadhi yenu; lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.” Ukweli ni kwamba baadhi ya watakatifu katika kanisa la Korintho walikuwa mashoga wa zamani. Ufalme wa Mungu umejaa watenda dhambi. Hakuna anayekuja kwa Mungu kwa sifa za kibinafsi. Sote tunakuja kwa njia ile ile: kupitia toba, kukataa dhambi ambayo Yesu alikufa kwa ajili yake, na kukubali haki ya Kristo mahali pake (2 Wakorintho 5:21).

Agano Jipya linatoa habari njema kwa kila mtu anayepambana na utambulisho wa kijinsia. Yesu anataka kuchukua nafasi ya mitindo yetu ya maisha ya dhambi na haki yake mwenyewe ili tuweze kuwa kama yeye zaidi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Agano Jipya linasema nini kuhusu ushoga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries