settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu uraibu wa ngono?

Jibu


Dhana ya uraibu wa ngono kuwa ugonjwa wa kisaikolojia sawa na matatizo mengine ya kulazimishwa, au sawa na uraibu mwingine, kama vile ulevi au matumizi haramu ya dawa za kulevya, na maendeleo ya hivi punde. Hapo awali, mwanamume (au mwanamke) ambaye alikuwa mzinzi alisemekana kuwa msherati na kujawa na tamaa. Suala sasa ni kwamba kitu ambacho Biblia inasema ni dhambi, ngono ya uasherati nje ya ndoa, inaitwa ugonjwa wa kisaikolojia. Kwa wengine huu ni udhuru, na kubainisha dhambi iliyo wazi. Kwa hivyo, je! kuna kitu kama uraibu wa ngono, na ikiwa ndivyo, Biblia inasema nini juu yake?

Kwanza, wacha isemwe kwamba kufanya mapenzi nje ya ndoa siku zote ni dhambi (Matendo 15:20; 1 Wakorintho 5:1; 6:13, 18; 10:8; 2 Wakorintho 12:21; Wagalatia 5:19; Waefeso 5:3; Wakolosai 3:5; 1 Wathesalonike 4:3; Yuda 7). Hakuna wakati ambapo ni sawa kufanya mapenzi nje ya ndoa. Baada ya kusema hayo, ni muhimu kutambua kwamba ngono kwa kweli ni ya uzoevu. Mtu anayeshiriki tendo la ndoa mara kwa mara karibu kila mara atakuwa mraibu wake kisaikolojia na kimwili. Ngono kati ya mume na mke katika ndoa ni “safi” Waebrania 13:4) na ni njia iliyowekwa na Mungu ya kupunguza hisia kali za “uraibu wa ngono.” Je! wenzi wa ndoa wanapaswa kujiruhusu kuwa waraibu hadi ngono iwe mvuto, na kizuizi kwa sehemu zingine za maisha? La sivyo kabisa. Ngono katika ndoa sio dhambi. Mume na mkewe wanaruhusiwa kibiblia kufanya ngono mara nyingi wapendavyo, katika roho ya maridhiano (1 Wakorintho 7:5).

Dhambi yenye ni uzoevu. Mara nyingi, na sio nyakati zote, dhambi huwa zoevu ikiwa inatendwa mara kwa mara. Kusema uongo, kunywa kupita kiasi, kuvuta sigara, ulafi, hasira, ponografia, n.k., yote yanaweza kuwa mazoea. Hatimaye, sisi sote, katika miili yetu iliyoanguka, tuna uraibu wa dhambi. Ngono isiyo ya adili, kame dhambi nyinginezo, inaweza kusababisha “kuongezeka kwa uovu” (Warumi 6:19). Kama vile matumizi haramu ya dawa husababisha kuongezeka kwa viwango vya dawa inayohitajika ili kufikia “ushawishi,” vivyo hivyo ngono isiyo ya maadili inaweza kusababisha kujamiiana mara kwa mara ili kupata uridhisho. Naama, kunao kitu kama uraibu wa ngono. Mtu anaweza kuwa mraibu wa kisaikolojia na kimwili wa kufanya ngono za mara kwa mara, zisizo za kawaida, za majaribio, na hata ukosefu wa maadili.

Ukweli kwamba ngoni inaweza kuwa na uraibu, na ukweli wa kibiblia kwamba dhambi inashawishi, ikiunganishwa, inaongoza kwenye hitimisho kwamba uraibu wa ngono upo kweli. Ukweli kwamba uraibu wa ngono upo, inagawa haubadili ukweli kwamba ni dhambi. Ni muhimu sana kutambua uraibu wa ngono kama dhambi, na sio kuiruhusu kama udhaifu wa kisaikolojia. Wakati huo huo, hatupaswi kupuuza ule ushawishi wa nguvu ngono inaweza kuwa nayo kwa mtu. Kama vile ilivyo kwa uraibu wa dhambi zingine, tiba pekee ya kweli ya uraibu wa ngono ni Yesu Kristo. Sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiw ana utukufu wa Mungu (Warumi 3:23). Kwa sababu ya dhabi zetu, sote tunastahili hukumu ya kifo cha milele (Warumi 6:23). Yesu, ambaye alikuwa Mungu katika umbo la mwanadamu, alilipa adhabu ya milele/isiyo na mwisho kwa ajili yetu (2 Wakorintho 5:21). Ikiwa tunaamini kikamilifu dhabihu yake kwa niaba yetu kama dhamana kamili ya dhambi zetu, tukimpokea kama Mwokozi kwa imani, anaahidi kwamba dhambi zetu zote zitasamehewa. Kisha, Mungu anatufanya kuwa viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17) na kuanza mchakao wa kutupatanisha na mapenzi yake (Warumi 12:1-2), ikiwa ni pamoja na kutuwezesha kushidna dhambi na kuacha mazoea yoyote ya dhambi tuliyo nayo. “Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu” (Warumi 7:24-25).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu uraibu wa ngono?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries