settings icon
share icon
Swali

Je! Ni namna gani Wakatoliki wanaweza punga mapepo ikiwa wingi wa imani zao sio za kibiblia?

Jibu


Katika filamu kama vile Upungaji mapepo (The Exorcist) na Upungaji mapepo wa Emily Rose (The Exorcism of Emily Rose- misingi yao ikiwa ni ya tukio halisi- mapepo yanapungwa na makasisi wa Katoliki. Hii imewafanya wengi kustaajabu, ikiwa upungaji huo wa mapepo ni wa kweli, ni namna gani unaweza kutekelezwa na Wakatoliki, ili hali Wakatoliki sio Wakristo.

Kwanza kabisa, kauli kwamba “Wakatoliki sio Wakristo” ni kauli pana sana. Dini ya Kikatoliki inafunza mengi ambayo ni kinyume na Neno la Mungu, lakini bado kuna waumini wa kweli katika Kanisa la Katoliki na wanatenda mema katika ulimwengu. Kuwa Mkatoliki haimfanyi mtu kuwa Mkristo, wala haimzui mtu kuwa Mkristo. Tafadhali soma nakala ifuatayo: Je! Ukatoliki ni dini ya uongo? Je! “Wakatoliki wanaokolewa?” na lile la “Mimi ni Mkatoliki. Je! Ni kwa nini nifikirie kuwa Mkristo?”.

Pili, miuzija inaweza kuwa ghushiwa (2 Wathesalonike 2:9). Yesu alisema kwamba baadhi ya wale ambao sio Wake waneza fanya ishara za miujiza- hii ikiwa ni pamoja na upungaji mapepo- katika jina Lake. Katika Mathayo 7:22-23, Yesu alionya, “Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’ Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’” Katika siku ya Hukumu, kutakuwa na wale ambao walipunga mapepo na walidhani walikuwa wameokolewa kwa sababu ya kazi yao njema. Walikuwa wamechukua tabia za Ukristo na kuyakubali akilini mwao baadhi ya mafundisho yake, lakini walikuwa Wakristo kwa jina tu. Hawakuwa wameyatoa maisha yao kwa Kristo. Katika hukumu hawa waliojiita Wakristo watagundua kwamba ule mwonekano wao wa nje wa kiroho hautoshi kuwawezesha kuingia mbinguni; miujiza yoyote waliyofanya iliwezeshwa na kitu kingine na sio Roho Mtakatifu. Kwa bahati mbaya, watu wengi hii leo wanashikilia falsafa mbaya kuwa matendo mema yanaweza kumpa mtu wokovu.

Shetani ako na kiasi fulani cha nguvu ambacho anatumia kuwadanganya na kuvuruga. Wachawi katika makao ya Farao weliweza kuiga miujiza mingi ya kile ambacho Musa alifanya (Kutoka 7:22;8:7). Ingawa, kulikuwa na kiwango ambacho uchawi wao ungeweza kutimiza, na nguvu za Mungu zilizidi ujanja wao (Kutoka 7:11-12). Inaweza kuwa kwamba upungaji mapepo wa Kikatoliki ni “miujiza,” namna hiyo ambayo inanuia kuipa utambulisho kanuni ya Kikatoliki na “kuthibitisha” nguvu za hirizi na matambiko.

Matendo 19:13-16 inatoa mfano wa watoa mapepo ambao hawakumjua Bwana Yesu na bado walijaribu kutumia nguvu Zake kuondoa mapepo: “Basi baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga huku na huko wakitoa pepo wachafu wakajaribu kutumia jina la Bwana Yesu wale wenye pepo wakisema, ‘Kwa jina la Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo, nakuamuru utoke.’ Wana saba wa Skewa, Myahudi aliyekuwa kiongozi wa makuhani, walikuwa wanafanya hivyo. Lakini pepo mchafu akawajibu, ‘Yesu namjua na Paulo pia namjua, lakini ninyi ni nani?’ Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.” Nguvu ya kweli haimo katika kutaja jina la Yesu, kunyunyizia maji matakatifu, au katika kuguza vazi, bali ni katika kumjua Yesu kibinafsi.

Mapepo yapo. Shetani yupo. Hata hivyo Shetani ni mlaghai mkuu na baba wa uwongo (Yohana 8:44; 2 Wakorintho 11:14). Uwezo wa pepo wa kuwavuta wanadamu wenye kudanganyika kwa mitego yake mara nyingi inazidi uwezo wetu wa kigundua mitego hiyo (2 Wakorintho 2:11; 1 Petro 5:8). Ikiwa litatimiza makusudi yake kwa kujificha kwa mwili wa mtu, pepo litafanya hivyo. Au ikiwa litatimiza makusudi yake kwa kujifanya kukuja kwa kuamrishwa, linaweza kufanya hivyo pia. Shetani pia anaweza kushiriki pamoja na anayepunga mapepo na ambaye hajaokoka ili aweze kuzidisha kiburi cha mpunga mapepo na kujivuna kwa nguvu zake mwenyewe juu ya mapepo. Kwa hivyo kusudi la “kuandaa” utoaji wa pepo unaweza kuwa ni wa kuwanasa wale wanaokuja kwa viongozi wa Katoliki ili kupata msaada.

Nguvu pekee ambayo tumehakikishwa itamshinda Shetani kila wakati ni nguvu ya Roho Mtakatifu inayokaa ndani ya muumini ambaye amejikinga na silaha zote za Mungu (Waefeso 6:11-17; 2 Wakorintho 10:4). Tunaponyenyekea kwa Mungu, tunaweza “kumpinga Ibilisi naye atawakimbia” (Yakobo 4:7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni namna gani Wakatoliki wanaweza punga mapepo ikiwa wingi wa imani zao sio za kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries