settings icon
share icon
Swali

Je, Upelejia na Nusu-Pelajia ni nini?

Jibu


Pelagius alikuwa mtawa ambaye aliishi katika karne ya 300 au mapema karne ya 400 AD Pelagius alifundishwa kwamba binadamu walizaliwa wasio na hatia, bila doa lolote la dhambi ya asili au ya kurithi. Yeye aliamini kuwa Mungu aliumba kila roho wa binadamu moja kwa moja na kwa hiyo kila nafsi ya mwanadamu awali ilikuwa huru kutokana na dhambi. Pelagius aliamini kwamba dhambi ya Adamu haikuweza kuathiri vizazi vijavyo ya ubinadamu. Mtazamo huu hujulikana kama Upelejia/Pelagianism.

Upelajia huitilafiana na maandiko mengi na kanuni za maandiko. Kwanza, Biblia inatuambia kwamba sisi wenye dhambi kutoka wakati wa mimba (Zaburi 51:5). Zaidi ya hayo, Biblia inafundisha kwamba binadamu wote hufa kama matokeo ya dhambi (Ezekieli 18:20; Warumi 6:23). Wakati Upelejia unasema kwamba binadamu hawazaliwi kwa mwelekeo wa asili dhidi ya dhambi, Biblia inasema kinyume (Warumi 3:10-18). Warumi 5:12 inasema wazi kuwa dhambi ya Adamu ndio sababu ya dhambi iliadhiri ubinadamu wengine. Mtu yeyote ambaye amelea watoto anaweza kushuhudia ukweli kwamba watoto wachanga lazima wafundishwe kuwa na tabia; sio lazima wafundishwe jinsi ya kutenda dhambi. Upelejia, kwa hiyo, ni wazi si wa kimaandiko na lazima ukataliwea.

Kimsingi nusu Pelajia wafundisha kwamba ubinadamu unachafuliwa na dhambi, lakini si kwa kiasi kwamba hatuwezi kushirikiana na neema ya Mungu juu yetu wenyewe. Nusu-Upelajia kwa asili, ni sehemu ya kuangamia kidogo kinyume na kuangamia kabsa. Maandiko yay ohayo hukanusha Upelejia pia hukanusha nusu Upelejia. Warumi 3:10-18 dhahiri haielezii binadamu kama kuwa sehemu tu iliochafuliwa na dhambi. Biblia inafunza wazi wazi kwamba bila Mungu "kutuvuta" kwake, sisi hatuna uwezo wa kushirikiana na neema ya Mungu. "Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba" (Yohana 6:44). Kama Upelejia, Upelejia nusu sio wa kibiblia na lazima ukataliwe.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Upelejia na Nusu-Pelajia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries