Swali
Biblia inasemaje juu ya umuhimu wa uwajibikaji?
Jibu
Pamoja na majaribu mengi tayari katika dunia ya leo, Shetani anafanya kazi kwa muda wa ziada kwa kuyaunda hata zaidi. Lazima tuwe na ndugu au dada tunaweza kuwajibikia wakati tunakabiliwa na majaribu ambayo yanatishia maisha yetu ya kiroho. Mfalme Daudi alikuwa peke yake jioni ile alijaribiwa katika uzinzi na shetani. Na inaweza onekana kuwa Bathsheba ndiye alimjaribu (2 Samweli 11), lakini Biblia inatuambia sisi kupigana vita visivy vya kimwili bali vya kiroho, dhidi ya nguvu na vikosi vya kiroho ambavyo hututishia (Waefeso 6:12).
Kwa kujua kwamba tuko katika vita dhidi ya nguvu za giza, tunapaswa kuhitaji msaada vile tuwezavyo kukusanyika karibu nasi. Katika Waefeso, Paulo anatueleza kwamba ni lazima tujikinge kwa vifaa vya nguvu zote ambazo Mungu hutoa, vifaa vya kupigana vita hivi. "Kwa sabau hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama" (Waefeso 6:13). Paulo alitambua kwamba hata kama sisi hujikinga wenyewe na kila kitu Mungu anatoa katika ulinzi wa uovu, sisi bado ni binadamu na huenda daima hatuna uwezo wa kupinga na majaribu ya Shetani. Tunajua bila shaka kwamba majaribu yatakuja.
Shetani anajua udhaifu wetu, na yeye anajua wakati tuko hatarini. Yeye anajua wakati wanandoa wanapigana na labda kuhisi kwamba mtu mwingine anaweza kuwaelewa vizuri. Yeye anajua wakati mtoto ameadhibiwa na wazazi wake na anaweza kuwa na hisia ya chuki. Yeye anajua wakati mambo yameenda mrama kazini na anajua jinsi hiyo inatukumbusha kiwanga kwamba kiko juu katika njia ya kwenda nyumbani. Ni wapi sisi tutapata msaada kama tumefanya yote tunaweza kufanya kupigana vita? Tunataka kufanya kilicho jema mbele za Mungu, lakini sisi tu wadhaifu. Tufanye nini?
Mithali 27:17 inasema, "Chuma hunoa chuma; ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake." uso wa rafiki ni mtazamo au usemi wa kutia moyo au msaada wa maadili.Ni wakati gani wa mwisho rafiki yako alikupigia simu kukujulia tu hali yako? Ni wakati gani wa mwisho ulimpigia rafiki wako mwanamke na ukamuuliza iwapo alitaka kuongea? Kutia moyo na msaada wa maadili kutoka kwa rafiki ndizo nyenzo zikosapo katika kubambana vita dhidi ya shetani.
Mwandishi wa Waebrania aliijumulisha wakati alisema, "Tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia...." (Waebrania 10: 24-25). Uwajibikaji ni muhimu sana katika vita ya kushinda dhambi. Mpenzi muwajibikaji anaweza kuwepo kukutia moyo, kukemea wewe, kufundisha, kwa kushangilia pamoja nawe, na kulia nawe. Kila Mkristo anapaswa kuwa na mpenzi muwajibikaji ambaye pamoja naye anaweza kuomba,kuongea,kuambia siri, na kukiri.
English
Biblia inasemaje juu ya umuhimu wa uwajibikaji?