settings icon
share icon
Swali

Nini kinatokea kwa watoto wachanga na watoto wadogo wanapo kufa? Ni wapi nitapata umri wa kuwajibika katika Biblia?

Jibu


dhana ya "umri wa kuwajibika" ni kwamba watoto hawawajibiki kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zao mpaka wafike umri fulani, na kwamba kama mtoto akifa kabla ya kufikia "umri wa kuwajibika," mtoto huyo kwa mapenzi, neema na huruma za Mungu atapewa kibali cha mbinguni. Je! dhana ya umri wa kuwajibika ni ya kibiblia? Je, kuna kitu kama "umri wa kutokuwa na hatia "?

Mara kwa mara katika kuzama katika majadiliano kuhusu umri wa kuwajibika ni ukweli kuwa watoto, bila kujali jinsi walivyo wadogo, bila kuwa na "hatia " katika hali ya kuwa na dhambi. Biblia inatuambia kwamba, hata kama mtoto wachanga au mtoto hajafanya dhambi ya ya kipekee, watu wote, ikiwa ni pamoja na watoto wachanga na watoto, tuko na hatia mbele ya Mungu kwa sababu ya dhambi tuliyorithi na kuadhiriwa. Dhambi iliyorithiwa ni ile ambayo pitishwa kutoka kwa wazazi wetu. Katika Zaburi 51:5, Daudi aliandika, "Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.” Daudi alitambua kuwa hata katika mimba alikuwa mwenye dhambi. Kusikitisha sana ukweli kwamba watoto wachanga wakati mwingine hufa inaonyesha kuwa hata watoto wachanga wanashikiliwa na dhambi ya Adamu, tangu kifo cha kimwili na kiroho yalikuwa matokeo ya dhambi ya Adamu ya awali.

Kila mtu, awe mtoto mchanga au mtu mzima, anasimama na hatia mbele ya Mungu kila mtu amechukisha utakatifu wa Mungu. Njia pekee ya Mungu inaweza kuwa tu na wakati huo huo kutangaza mtu mwenye haki ni kwa kuwa mtu kuwa na kupokea msamaha kwa imani katika Kristo . Kristo ndiye njia pekee. John 14:6 imenakili kile alichokisema Yesu: "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi" vile Petro asemavyo katika Matendo 4:12, "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chin ya mbigu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa." Ukombozi ni uchaguzi wa kibinafsi.

Na je, itakuaje kuhusu watoto wachanga na watoto wadogo ambao kamwe hakuweza fikia uwezo wa kufanya uchaguzi huu wa kibinafsi? Umri wa kuwajibika ni dhana kwamba wale wanao kufa kabla ya kufikia umri wa uwajibikaji moja kwa moja huokolewa kwa neema na huruma ya Mungu. Umri wa kuwajibika ni imani kwamba Mungu anaokoa wale wote wanaokufa bila kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa au dhidi ya Kristo. Umri wa miaka kumi na tatu kwa kawaida umependekezwa kuwa umri wa kuwajibika, kwa kuzingatia desturi ya Wayahudi kwamba mtoto anakuwa mtu mzima na umri wa miaka 13. Hata hivyo, Biblia haitoi haiungi moja kwa moja na umri wa miaka 13 daima kuwa umri wa uwajibikaji. Kuna uwezekano kuwa inatofautiana kutoka mtoto hadi mtoto. Mtoto ambaye amepita umri wa kuwajibika mara tu yeye huwa na uwezo wa kufanya uamuzi wa imani wa kumfuata au kutomfuata Kristo. Maoni ya Charles Spurgeon ni kwamba "mtoto wa miaka mitano anaweza kuokolewa vile na mzima ambaye amefanywa upya."

Wazo la hapo juu likiwa katika akili, pia fikiria hili: kifo cha Kristo kimetolewa kuwa cha kutosha kwa ajili ya wanadamu wote. Yohana wa kwanza 2:2 inasema Yesu ni "naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu." Mstari huu uu wazi kwamba kifo cha Yesu kilikuwa tosha kwa ajili ya dhambi zote, siyo tu dhambi za wale pekee ambao hasa huja kwake kwa imani. Ukweli kwamba kifo cha Kristo kilikuwa cha kutosha kwa ajili ya dhambi zote kitaruhusu uwezekano wa Mungu kutumia malipo hayo kwa wale ambao kamwe hawalikuwa na wezo wa kuamini.

Baadhi ya wengi uhuzisha umri wa uwajibikaji na agano la uhusiano kati ya taifa la Israeli na Bwana ambapo hakuna mahitaji yaliyohuzishwa juu ya mtoto wa kiume kuwa ndani ya agano lingine lolote lile zaidi ya tohara, ambayo alifanywa siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake (Kutoka 12:48-5, Mambo ya Walawi 12:3).

Swali linajipusa, "Je, asili ya umoja wa Agano la Kale watumika katika kanisa hii leo?" Katika siku ya Pentekoste, Petro alisema, "Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie" (Matendo 2:38-39). Neon watoto hapa ( teknon katika Kigiriki) maana yake ni " mtoto, binti, mmwana." Matendo 2:39 inaonyesha kwamba msamaha wa dhambi unapatikana kwa moja na wote (taz. Mdo 1:8), ikiwa ni pamoja na vizazi vijavyo. Haifundishi wokovu wa kifamilia au kaya. Watoto wa wale waliotubu walihitajika pia kutubu.

Kifungu kimoja knachoonekana kutambua mada hii zaidi kuliko nyingine yoyote ni 2 Samweli 12:21-23. Mkudhata wa aya hii ni kwamba Mfalme Daudi alizini na Bathsheba, na matoke yake akashika mimba. Nabii Nathani alitumwa na Bwana kumjulisha Daudi kwamba, kwa sababu ya dhambi yake, Bwana atamchukua mtoto katika kifo. Daudi aliyaitikia haya kwa kuomboleza na kuomba kwa ajili ya mtoto. Lakini mara tu mtoto alichukuliwa, kuomboleza kwa Daudi kuliisha. Watumishi wa Daudi walishangaa kwa kuyasikia haya. Wakasema kwa mfalme Daudi, "Ni neno gani hili ulilolitenda? Umefunga na kulia kwa ajili ya mtoto, alipokuwa hai; lakini mtoto alipokuwa amekufa, uliinuka ukala chakula. Akasema, Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia; kwa maana nalisema ni nani ajuaye kwamba BWANA atanihurumia, mtotoapate kuishi? Lakin sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi."Hatua ya Daudi inaonyesha kwamba wale ambao hawawezi kuamini wako salama katika Bwana. Daudi alisema kwamba angeweza kwenda kwa mtoto lakini hangeweza kuleta mtoto hai tena. Pia, kama jambo la muhimu, David alionekana kutiwa moyo na elimu hii. Kwa maneno mengine, David alionekana kusema kuwa angeweza kumwona mtoto wake mwana (mbinguni ), ingawa hakuweza kumrudisha.

Ingawa kuna uwezekano kwamba Mungu Anatumia kifo cha Kristo kama malipo kwa ajili ya dhambi kwa wale ambao hawawezi kuamini, Biblia haisemi hasa kwamba Yeye afanya hivi. Kwa hiyo, hili ni somo ambalo sisi lazima tuwe wagumu au wenye mafunzo dhabithi. Mungu hutumia kifo cha Kristo kwa wale ambao hawawezi kuamini na wanaonekana kuwa na upendo wake na huruma zake kila wakati. Ni msimamo wetu kwamba Mungu Anatumia kifo cha Kristo kama malipo kwa ajili ya dhambi kwa watoto na wale ambao wamepungukiwa kiakili, kwa sababu wao hawana uwezo wa kiakili wa kuelewa hali yao ya dhambi na mahitaji yao kwa Mwokozi, lakini tena hatuwezi kuwa wenye idhikadi. Kwa haya tuna huhakika: Mungu ni upendo, mtakatifu, mwenye haki, na neema. Chochote Mungu daima anatenda ni haki na nzuri, na Yeye anapenda watoto hata zaidi kuliko tuwapendavyo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini kinatokea kwa watoto wachanga na watoto wadogo wanapo kufa? Ni wapi nitapata umri wa kuwajibika katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries