settings icon
share icon
Swali

Je! Kila mtu atakuwa umri gani mbinguni?

Jibu


Biblia haijibu swali hili moja kwa moja. Je! Watoto wachanga na watoto wanaokufa bado watakuwa watoto mbinguni? Na je, wakongwe wanaokufa- wanabaki wakongwe mbinguni? Wengine wamekisia kwamba watoto wachanga wanapewa mwili wa ufufuo (1 Wakorintho 15:35-49) ambao kwa “upesi unasukumwa mbele” katika “umri unaofaa,” kama vile wale wanaokufa wakiwa wazee “wanabadilishwa” kwa umri bora. Hii inaweza kuonyesha kwamba hakutakuwa na watoto au wazee mbinguni.

Umri unaofaa ni upi? Tena, dhana hii sio ya kibiblia haswa. Wengine wanaamini kuwa ni mika 30. wengine wanakisia kuwa miaka 33 kwa kuwa hiyo ni takribani na umri ambao Yeus alikuwa alipokufa. 1 Yohana 3:2 inatangaza hivi: “Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo.”

Kuna jambo moja ni hakika. Umri wowote tunaoonekana kuwa nao, tutakuwa wakamilifu kwa utukufu. Tutafanywa upya bila upungufu, kamilifu na kuwa kama Kristo. Tuwacha chembe zote za anguko la kibinadamu, tukivaa mavazi meupe ya usafi, utakatifu na ukamilifu kabisa. Kwa hivyo umri wowote tulio nao, utakuwa ni umri kamilifu kabisa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kila mtu atakuwa umri gani mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries