settings icon
share icon
Swali

Je, Ukanaji Mungu mpya ni nini?

Jibu


Mwanzoni mwa karne ya 21 kumekua na moni kuwa dini isiwe msingi wa elimu na maadili, na ukanaji Mungu ukikuzwa katika dunia ya Magharibi yote kwa nguvu thabiti inayozidi kuongezeka na kwa kijeshi. Hii imesababisha kuibuka kwa “wakanamungu wapya,” wanachama mashuhuri ambao wanajumuhisha waandishi wanaouza ujapishaji wao sana kama vile Sam Harris, Daniel Dennett, Richard Dawkins, na Christopher Hitchens.

Ubishi wa wakanamungu wapya ni, kwa Dhahiri, kwamba hakuna Mungu. Wafuasi wa falsafa ya ukanaji Mungu mpya wanaamini kwamba upovu, nguvu za asili, ndizo zinawajibika kwa uhakika wote tunaojua. Wakanamungu wapya hawajiwekei vikwazo kwa kutoamini batili. Badala yake, wanashiriki kikamilifu katika kuonya wengine kufuata nyayo, kutangaza kutokuamini kwao katika Mungu, na kuchukua hatua muhimu ya kuondoa ulimwengu wa imani na desturi ya kikristo. Kama vile mkanamungu anayesema kwa wazi Richard Dawkins anaiweka katika kitabu cha Udanganyifu wa Mungu, “Nafanya kila kitu kwa nguvu zangu kuwaonya watu dhidi ya imani yenyewe.”

Sifa ya dhihaka ya ukanaji Mungu mpya ni imani yake kali katika uduni wa kuwa na imani. Wakanamungu wapya wanafafanua upya kimakosa “imani” kama “Imani isiyo na akili katika kutokuwako na ushahidi.” Huu upotoshaji wa asili ya imani ni upuuzi, kwa Imani kimsingi sio Imani kali katika kitu, lakini badala yake msingi wa Imani ya Mkristo ni kuamini katika mtu—Mungu. A.W. Tozer alisema, “Imani inapumzika juu ya tabia ya Mungu, sio juu ya maonyesho yamaabara au mantiki.” Wakati mtu ana imani katika tabia ya mtu, kwa mfano, mama au rubani wa ndege, mtu haitaji kuwa na shaka au kuhitaji ushahidi dhabiti ili kuwa na heshima kwa huduma ambayo anatoa.

Wakati inahuzisha vitu, Wakristo wanalishughulikia suala hili kwa kutafuta ushahidi dhabiti, wakati wanakubali kwamba mambo mengine yanaweza kuwa zaidi ya ufahamu wetu wa sasa. Kweli, wanasayansi wengi waliojawa na imani wamekuwa katika mashirika ya kisayansi ya kisasa na kujaribu ushahidi wakitumia mbinu na ujuzi kali. Wakanamungu wapya wanaamini kwamba majaribio ya sayansi ni njia ya pekee ya kufahamu uhakika. Hata hivyo, haya makosa, tangu wazo la “sayansi” (mtazamo kwamba sayansi ni njia pekee ya kupata elimu) yenyewe sio somo kwa jaribio lolote la kisayansi na hatimaye kusafisha imani. Imani, mbali na kuwa “Imani isiyo na akili katika kutokuweko kwa ushahidi,” ni uamuzi wa kufikiri kama kweli kitu ambacho kisichoonekana. Sayansi ni wazo la kimetafizikia. Basi, wakanamungu wapya wanahitaji imani ya maelezo fulani, ata kama sio kwa Mungu. Sayansi inajikanusha yenyewe, na basi haistitahili kuaminiwa. Sayansi inaweza wekwa kwa muhtasari kama imani amabayo, “majaribio ya sayansi ni njia pekee ya kuwa hakika kuhusu chochote.” Bila shaka, tunaweza kuuliza basi, “Ni jaribio gani la kisayansi ambalo lilidokeza kwamba majaribio ya sayansi ndio njia pekee ya hakika kuhusu chochote?”

kiulinganisho, ukanaji Mungu unajifungamanisha na ukweli kwamba Mungu anapita uwezo wa binadamu. Ukanamungu wa kibiblia unatemea seti ya dhana za busara, mojawapo ni kwamba hakuna kitu kama asiyeamini Mungu. Ni kweli kwamba wasioamini Mungu wana imani ya namna Fulani, ikiwa tu katika uwezo wao wakushawishi wengine wajiunge na njia zao ukanaji mungu. Warumi 1:19-20 inatangaza wazi kwamba watu wote wanajua Mungu yupo kwa sababu Mungu amejifunua kwa wazi busara hiyo kwao kupitia kwa ushahidi wa uumbaji. Wale wanaomkataa Mungu wanafanya hivyo kwa sababu ya uasi wa moyo ulio gizani (Warumi1:21). Mkanamungu aliyejitangaza mwenyewe anaweza fikiria kuwa msomi, lakini Mungu ametamka, “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu” (Zaburi 14:1; 53:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Ukanaji Mungu mpya ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries