settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu udanganyifu wa mtihani shuleni?

Jibu


Udanganyifu kimsingi ni kutenda kwa njia isiyo ya uaminifu au ya haki ili kupata manufaa ya kibinafsi. Udanganyifu unapuuza sheria zilizowekwa kwa ajili ya mafanikio ya kibinafsi. Wakati tamaa ya ubinafsi ya kutaka ushindi au mafanikio inapozidi ahadi ya kiadili ya ukweli na usawa, kudanganya kunaweza kuwa kishawishi. Lakini kama viumbe vipya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17), tunaweza kuchagua kukataa majaribu yenye kudhuru (Mathayo 26:41; 1 Wakorintho 10:13).

Wakristo wanapaswa kujitahidi kumtukuza Bwana kwa mawazo na matendo yao (1 Wakorintho 3:16). Kudanganya huwa kinyume na wema ambao utamtukuza. Ukosefu wa uaminifu huharibu uadilifu na sifa ya mtu binafsi (Mithali 10:9). Kutojionyesha kwa ukweli ni kusema uongo, na kusema uongo ni dhambi (Walawi 19:11; Mithali 12:22).

Hata ingawa ulimwengu unaruhusu ukosefu wa uaminifu wakati inauona kuwa jambo dogo, Mungu anawauliza wafuasi Wake wawe wasemaji ukweli kila wakati. Ikiwa mwanafunzi atafanya vibaya kwenye mtihani kwa sababu hakusoma, alama yake ya chini ni matokeo ya asili ya chaguo mbaya. Mungu ataheshimu unyoofu huo, na mwanafunzi anaweza kujifunza kutokana na makosa yake. Matokeo mabaya kwenye mtihani yanaweza kufundisha na kumtia moyo mwanafunzi kusoma kwa bidii zaidi kabla ya wakati au kupata mwalimu binafsi au kupata usingizi wa kutosha usiku uliotangulia. Matokeo shuleni yanapaswa kuonyesha yale ambayo yamefunzwa darasani na juhudi mwanafunzi amekuwa akifanya. Udanganyifu wa mtihani unanuia kukwepa mchakato wa kujifunza na kudhibiti matokeo kwa kukosa uaminifu.

Wafuasi wa Kristo wanahitaji kutembea katika nuru, na udanganyifu huzuia watu kuona utukufu wa Kristo. Ukosefu wa uaminifu huchafua wema ambao watoto wa Mungu wanapaswa kuwa nao (Wafilipi 2:15; Waefeso 5:8). Ikiwa Baba yetu wa Mbinguni analaani uongo (Mithali 6:16-19), hakuna njia ambayo muumini anaweza kuhalalisha uongo “usio na madhara” kama vile kudanganya.

Kudanganya ni tendo la ubinafsi linalotupa faida zaidi ya wengine wanaokabili changamoto hiyo. Kama Wakristo, tunapaswa kutafuta kuwasaidia wengine kwa usawa na haki tukidumisha uaminfu wa maadili na sifa ya kimungu. Kudanganya hakusaidii katika kudumisha kiwango hicho.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu udanganyifu wa mtihani shuleni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries