settings icon
share icon
Swali

Uchumba ilikua nini wakati wa kibiblia?

Jibu


“Nyakati za Kibiblia” inashughulikia sehemu pana ya ratiba ya matukio ya historia, kwa sababu historia ya Biblia inahusisha maelfu ya miaka na tamaduni kadhaa. Katika miaka hiyo na tamaduni hizo, mila za uchumba zilitofautiana. Hata hivyo, baadhi ya vipengele vya uchumba vilikuwa dhabiti wakato wote.

“Uchumba” katika nyakati za Biblia, kama vile ilivyo katika nchi za kisasa za Magharibi, ulikua uhusiano wa watu wa jinsia tofauti kabla ya ndoa. Wakati huo na kama ilivyo sasa, wakati wa kuchumbiana ulimpa bi-arusi fursa ya kujiandaa kwa ajili ya wajibu wake mpya, kukusanya vitu vya kibinafsi, kuweka sawa uhusiano na wazazi, ndugu na dada, marafiki, na kufahamiana zaidi na mchumba wake. Bwana harusi alitumia wakati wa uchumba kwa shughuli sawa, ikiwa ni pamoja na kukamilisha nyumba ya kulelea familia yake.

Ndoa za kupangwa zilikuwa ni jambo la kawaida katika nyakati za Biblia, na inawezekana kwamba bi-arusi na bwana arusi hawakujuana hadi wakati walipokutana kwa sherehe ya harusi. Ikiwa wazazi walipanga arusi wakati bi-arusi, bwana harusi au wote wawili walikuwa wachanga kufanya ndoa, uchumba wa muda mrefu zaidi ungefanyika. Kinachoonekana kuwa cha ajabu kwa watu wa kisasa wa Magharibi ni kwamba mvuto wa ngono wala upendo hakuwa wa muhimu kutanguliza uchumba au ndoa. Wazaazi waliopanga ndoa ya watoto wao walidhani upendo na shauku ingekua kutokana na kufahamiana kwa karibu na uhusiano wa kingono ambao kawaida hutokea katika ndoa. Mawazo haya yanasaidia kuelewa ni kwa nini Waefeso 5:25-33 inawaamuru waume kupenda wake zao na wake Wakristo kuwaheshimu waume zao. Upendo na heshima hiyo ilikua baada ya harusi na haikuihitajika hapo awali.

Katika utamaduni wa kisasa wa Magharibi, kuna tofauti ya wazi kati ya uchumba na ndoa. Katika tamadudi za nyakati za Biblia, tofauti hiyo haikuwa wazi kabisa. Katika nyakati za Biblia, uchumba ulihusisha familia mbili katika mkataba rasmi, na mkataba huo ulikuwa makubaliano ya kubana kama ndoa yenyewe. Uchumba basi ulikuwa kama vile shughuli ya kibiashara kati ya familia mbili na sio chaguo la kibinafsi la kimapenzi. Makubaliano ya mahari yalihusishwa, hivyo kwamba uchumba uliovunjika ulihitaji kulipa ile mahari. Baada ya uchumba, yaliyobaki yalikuwa mambo matatu: sherehe ya harusi, bi-arusi kuhamia kwa nyumba ya bwana arusi, na utimilifu wa ndoa.

Mfano unaojulikana sana wa uchumba ni ule wa mamake Yesu, Maria, na mchumba wake, Yosefu. Yosefu alipojua kwamba Maria alikuwa mjamzito , na kabla kuelewa asili ya kimuujiza ya mimba hiyo, alifikiri kwamba alikiuka uchumba wake, ambao ulikuwa makubaliano ya kubana kama vile mkataba wa ndoa. Hapo mwanzo, Yosefu aliamini kwamba suluhisho pekee ilikuwa kumtaliki Maria au “kuachana naye.” Mathayo anaandika simulizi hiyo: “ Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri ” (Mathayo 1:18–19). Mathayo anasema kwamba Maria alikuwa “ameposwa,” lakini pia anamwita Yosefu “mume wake.” Ukweli kwamba “talaka” ilihitajika ili kuvunja uchumba inaonyesha kwamba mkataba kabla ya ndoa ulikuwa wa lazima kisheria. Ikiwa, hata katika muda wa uchumba, Maria angekuwa amefanya ngono na mtu mwingine isipokuwa Yosefu, angekuwa na hatia ya uzinzi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uchumba ilikua nini wakati wa kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries