settings icon
share icon
Swali

Uchaguzi wa masharti ni nini?

Jibu


Ingawa Biblia inafundisha wazi kwamba Mungu huchagua watu kwa wokovu, kuna kutokubalina kuhusu msingi wa uchaguzi huo. Uchaguzi wa masharti ni imani kwamba Mungu huwachagua watu kwa ajili ya wokovu kulingana na fahamu Yake ya mbeleni ya ni nani ataweka imani yake katika Kristo. Uchaguzi wa masharti unasema kwamba Mungu ajuaye mambo yote anatizamia wakati ujao na anaamua kuwachagua watu kulingana na uamuzi wao wa siku zijazo wa kuja kwa Kristo. Unachukuliwa kuwa uchaguzi wa “masharti kwa sababu unategemea hali ya mwanadamu kufanya jambo kwa hiari yake mwenyewe. Kulingana na uchaguzi wa masharti, wale ambao Mungu anawajua kuwa watakuja kwa imani katika Kristo wamechaguliwa na Mungu, na wale ambao Mungu anajua hawatamkubali Kristo hawajachaguliwa.

Uchaguzi wa masharti ni mojawapo ya Nakala za Upingamizi unaofafanua theolojia ya Waararati na kiini msingi cha mtazamo huo na mfumo wakitheolojia. Kwa hivyo, ni pingamizi kwa imani ya wale wanaoshikilia theolojia ya Mageuzi, ambayo inaamini kwamba Biblia inafundisha uchaguzi usio na masharti, mtazamo kwamba Mungu huchagua watu kwa mjibu wa mapenzi yake kuu na si juu ya hatua yoyote ya wakati ujao ya mtu ambaye amechaguliwa.

Wale wanaoamini katika uchaguzi wa masharti mara nyingi wao hunukuu mistari kama 1 Petro 1:1-2, ampapo Petro ameandika “Kwa wateule wa Mungu, wageni katika ulimwengu, waliotawanyika kote katika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba.” Kifungu kuu hapa ni ninyi ambao mlichaguliwa … kulingana na alivyotangulia kuwajua. Au mstari mwingine wenye maana kama hiyo ni Warumi 8:29-30, “Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza.”

Walakini kwa kweli hakuna mjadala au kutokubaliana katika ukweli kwamba Mungu, kwa sababu yeye ni mjua yote, alikwisha jua mbeleni ya ni nani ataokolewa na ni nani hataokolewa. Mjadala kati ya uchaguzi wa masharti na uchaguzi usio na masharti ni kuhusu ikiwa mistari hii inafunza kwamba “uchaguzi wa hiari” wa mwanadamu ndio chanzo cha uchaguzi wa Mungu au kukubali kwamba Mungu ana ufahamu wa kabla wa ni nani atakayeokoka na ni nani hataokoka. Ikiwa hii ndiyo ilikuwa mistari pekee katika Maandiko ambayo ilishughulikia uchaguzi, basi, suala kuwa ikiwa Biblia inafunza juu ya uchaguzi wa masharti litakuwa wazi kwa kujadiliwa, lakini sivyo. Kuna vifungu vingine vilivyo wazi kabisa vinavyotuambia ni kwa misingi gani Mungu huwachagua watu kwa wokovu.

Mstari wa kwanza unaotusaidia kuelewa ikiwa uchaguzi wa masharti ndio kile Biblia inafundisha ni Waefeso 1:4-5: “Kwa maana alituchagua katika yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele zake. Kwa upendo, alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe.” Hapa tunaona wazi kwamba Mungu alikwisha tuchukua au chagua watu binafsi “kwa mapenzi yake mwenyewe.” Tunapolizingatia wazo la kufanywa wana na ukweli kwamba ni Mungu ndiye anayetuchagua sisi kufanywa wana na kwamba ilifanyika kabla ya ulimwengu kuwekwa misingi, inaonekana wazi kwamba msingi wa uchaguzi wa Mungu na kuchaguliwa tangu asili sio chaguo ambalo tungefanya katika wakati ujao bali kwa mapenzi Yake kuu pekee ambayo Yeye huyafanya “katika upendo.”

Mstari mwingine unaounga mkono uchaguzi usio wa masharti ni Warumi 9:11, ambapo Mungu anaeleza “Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama.” Ingawa wengine wanataka kutupilia mbali Warumi 9:11 kuwa haitumiki katika uchaguzi wa kishirika na sio wa mtu binafsi, hatuwezi kupuuza sehemu hii ya Maandiko ambayo inafundisha kwa uwazi kwamba uchaguzi HAUNA masharti yoyote ambayo mwanadamu amefanya au atafanya lakini msingi wake uu katika Mungu mwenye enzi.

Mstari mwingine ambao unafundisha uchaguzi usio na masharti ni Yohana 15:16, “Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu.” Fauka ya hayo, katika Yohana 10:26-27 Yesu anasema, “Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata.” Uchaguzi wa masharti unasema kuwa watu ambao wanaamini kuwa wamechaguliwa kuwa kondoo Wake kwa sababu wameamini, lakini Biblia inasema kinyume na hayo. Sababu yao kuamini ni kwamba wao ni kondoo lake. Uchaguzi hautegemei mtu kumkubali Kriso kama Bwana na Mwokozi bali ni sababu ya kukubalika kwake

Uchaguzi wa masharti ni mtazamo kwamba uamuzi wa “hiari huru” ya mwanadamu katika kumkubali Kristo kama Mwokozi ndio msingi wa kuchaguliwa kwake. Kwa hivyo, kwa maana halisi, uamuzi wa mwanadamu ndiyo sababu ya wokovu. Mtazamo huu wa uchaguzi ni muhimu kwa sehemu kubwa kwa sababu ya mtazamo wa kilimwengu wa Kiararati ambapo mwanadamu anamchagua Mungu, badala ya Mungu kumchagua mwanadamu. Katika mtindo wake rahisi, theolojia ya Kiararati ni kwamba, hatimaye, wokovu wa mwanadamu unategemea “uamuzi wa hiari huru” wake pekee na sio mapenzi ya Mungu. Uchaguzi wa masharti unaelekeza kwa tamatisho kwamba tendo la Mungu katika uchaguzi hutegemea uamuzi wa hiari huru wa mwanadamu. Mtazamo huu wa uchaguzi na wokovu unamfanya Mungu kuwa chini ya matakwa ya wanadamu na maamuzi yao, na mapenzi ya mwanadamu kimsingi huwa sababu na athari ya wokovu.

Kwa upande mwingine, katika uchaguzi usio na masharti ni mapenzi kuu ya Mungu ambayo huamua ni nani anayechaguliwa na ni nani asiyechaguliwa. Kwa hivyo, ni mapenzi ya Mungu na neema ya Mungu ambayo inawajibika kikamilifu kwa wokovu wa mwanadamu. Wale wote ambao Mungu amewachagua kwa wokovu watakuja kwenye imani iokoayo katika Kristo, na wale ambao Yeye hatawachagua hawatachagua imani iokoayo katika Kristo (Yohana 6:27).

Mitazamo hii miwili kuhusu uchaguzi haiambatani hata kidogo. Mtazamo mmoja uu sahihi na mwingie sio sahihi. Mtazamo mmoja hufanya uteuzi wa Mungu na hatima ya wokovu wa mwanadamu kutegemea mwanadamu, na hivyo kumpa mwanadamu sifa na utukufu, huku mtazamo mwingine ukitambua kwamba uchaguzi na wokovu hutegemea mapenzi ya Mungu kuu. Mtazamo mmoja una mwanadamu kama mtawala wa hatima yake, na kimsingi, yeye anadhbiti wokovu wake, huku mtazamo mmoja ukimtukuza mwanadamu, mtazamo mwingine unamtukuza Mungu. Mtazamo mmoja ni ushuhuda wa wema na uwezo wa mwanadamu, na mtazamo mwingine ni ushuhuda wa neema ya ajabu ya Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uchaguzi wa masharti ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries