settings icon
share icon
Swali

Katika maamuzi ya kutamatisha maisha, ni lini ubora wa maisha unapaswa kuzingatiwa?

Jibu


Kuendelea kwa teknolojia ya matibabu kumeokoa maisha na ubora wa maisha kwa watu wengi, lakini pia kumezua maswali mapya ambayo vizazi vilivyopita havikuwa na budi kuyajibu. Karne moja iliyopita, chaguzi za mwisho wa maisha zilikuwa chache, na kifo kilikuja haraka zaidi bila mashine za kuweka viungo kufanya kazi wakati ubongo haufanyi kazi. Lakini, sasa dawa inaweza kusidisha muda wa ishara muhimu, kuwepo wa maisha sio kitu pekee cha kuzingatia. Ubora wa maisha unasonga mbele tunapoona wapendwa wetu wakiteseka au kukaa kwa muda mrefu kuliko mtu yeyote angetaka. Swali la kimaadili linazuka: kusungemza kibiblia, je, ubora wa maisha unapaswa kuzingatiwa katika maamuzi ya kutamatisha maisha?

Ubora wa maisha ni uamuzi wa kibinafsi. Kila mtu anapaswa kuwa na haki ya kujiamulia kile anachoona kuwa “bora.” Baadhi ya watu hushikilia sana kila sehemu ya maisha, wakitafuta kila uingiliaji kati wa kibinadamu uwezekanavyo kimatibabu ili kurefusha maisha ya kidunia. Wengine, hasa Wakristo, wanaweza kukubali kifo chao kinachokaribia kwa utulivu zaidi na hata kuonyesha shauku ya kuingia umilele mara tu Mungu anapowaita nyumbani. Haki ya kukataa ganga ganga za matibabu inapaswa kupatikana kwa kila mtu mzima aliyetulia kiakili na inaweza kurekodiwa kwa wosia hai au aina zingine za maagizo yaliyoandikwa. Hata hivyo, hati kama hizo zinaweza kuvuka mipaka ya maadili wakati chaguzi za mwisho wa maisha zinajumuisha kifo cha haraka au kusaidiwa kujiua. Kama vile kujiua hakuzingatiwe kuwa haki ya binadamu, wala kujiua kwa kusaidiwa kutokana na ubashiri wa kimatibabu hauzingatiwi.

Ingawa kila mtu anapaswa kuwa na sauti katika kauamua ufafanuzi wake mwenyewe wa “ubora wa maisha,” wanadamu sio waamuzi wa mwisho. Maisha ni mkusanyiko wa uzoefu mzuri na mbaya, na kuna nyakati katika maisha ya kila mtu wakati ubora unaonekana kuwa wa chini. Huzuni, wasiwasi, mshtuko wa moyo, au shida ya kifedha inaweza kuonekana kupunguza ubora wa maisha kwa msimu. Jeraha, ugonjwa, au ulemavu unaweza kuharibu sana ubora wa maisha ya mtu, lakini hiyo haimaanishi haki ya kukomesha maisha hayo. Mungu ndiye anayeamua maisha na kifo, sio maoni yetu juu ya ubora wake (Kumbukumbu 32:9; Zaburi 139:16).

Kuandika wosia ukiwa hai au kukabidhi mamlaka ya kudumu wakili wa familia anayeaminika ni njia mbadala nzuri ya kufanya maamuzi ya dadika za mwisho na familia zinazojaribu kubainisha matakwa ya mgonjwa. Kunyima dawa zinazojaribu kubainisha matakwa ya mgonjwa. Kumnyima dawa fulani, matibabu, au hatua za kuokoa uhai kunaweza kuwa kwa manufaa ya mgonjwa, na, ikiwa hilo limezungumziwa hapo awali, familia huondolewa daraka hilo la kiadili. Kuanzisha uhusiano wa kuaminiana na kaktari anayemtunza mgonjwa anayekufa kunaweza pia kuondoa mawasiliano yasiyofaa na majuto baadaye. Kwa bahati nzuri, bado ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi kwa madaktari kuagiza dawa ambazo zitamaliza maisha kikamilifu. Uwezekano wa matumizi mabaya ya chaguo hilo hufanya kuwa hatari kuacha kwa hiari ya kibinadamu. Hata hivyo, huduma shufaa inaweza kuongezwa hadi kuruhusu mwili kufa bila kumsababishia mgonjwa maumivu yasiyofaa. Wakati uwezekano wote wa tiba umekwenda, kuongeza dawa za kupunguza huruhusu mwili kuzimia kawaida, na kifo kinaweza kutokea bila kurefusha mchakato wa kufa bila sababu.

Ubora wa maisha hauwezi kufafanuliwa na mambo ya nje. Ubora wa maisha ya mtu ni wa kibinafsi sana na mara nyingi hufungwa nira kwa uhusiano wa mtu huyo na Mungu. Watu wenye afya njema na matajiri wanaweza kuwa na ubora wa chini wa maisha kutokana na machafuko ya kihisia na maamuzi mabaya ya maadili, wakati mtu mlemavu katika umaskini anaweza kuishi maisha yaliyojaa furaha. Ugonjwa wa kimwili pa hauamui ubora wa maisha ya mtu, hivyo sio uwezo wetu kujaribu kutathmini uwezo wetu. Jukumu letu mbele za Mungu ni kuandaa utanzaji bora zaidi wenye upendo kwa wale wanaoteseka na kutumaini kwamba Muumba wao ndiye atakayeamua maisha yatakapoisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Katika maamuzi ya kutamatisha maisha, ni lini ubora wa maisha unapaswa kuzingatiwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries