settings icon
share icon
Swali

Je! ubatizo ni wa muhimu kwa wokovu? Ni nini maana ya ubatizo wa kuzaliwa upya?

Jibu


Ubatizo wa kuzaliwa upya ni imani kwamba mtu lazima abatizwe ili aokolewe. Ni ubishi wetu kwamba ubatizo ni hatua muhimu ya utii kwa Mkristo, lakini sisi kwa kusita kidogo hukataa ubatizo kama kuwa inahitajika kwa ajili ya wokovu. Tunaamini kwamba kila mmoja na kila Mkristo lazima apatizwe kwa maji mengi. Ubatizo unaeleza kitambulisho cha waumini kwa kifo cha Kristo, kuzikwa, na kufufuka kwake. Warumi 6:3-4 inasema, "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Krisot alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima." Hatua ya kuzamishwa katika maji inadhihirisha kufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Hatua ya kutoka nje ya maji yaashiria picha ya ufufuo wa Kristo.

Wanaohitaji kitu chochote Mbali na imani katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu waweka imani yao kitika matendo ili wapate wokovu. Kuongeza chochote kwa injili ni kusema kwamba kifo cha Yesu msalabani hakikutosha kununua wokovu wetu. Kusema ni lazima tubatizwe ili tuokolewe ni kusema kuwa ni lazima tuongeze matendo yetu wenyewe mazuri na utii kwa kifo cha Kristo ili tukifanye kutosha kwa ajili ya wokovu. Ni kifo cha Yesu peke kililipia deni ya dhambi zetu (Warumi 5:8, 2 Wakorintho 5:21). Yesu kulipia dhambi zetu imetuongezea akiba kwa imani peke yake (Yohana 3:16; Matendo 16:31; Waefeso 2:8-9). Kwa hivyo, ubatizo ni hatua muhimu ya utii baada ya wokovu lakini haiwezi hitajika kwa ajili ya wokovu.

Naam, kuna baadhi ya mistari inaonekana kuonyesha kuwa ubatizo unahitajika kwa ajili ya wokovu. Hata hivyo, tangu Biblia inatueleza wazi kwamba wokovu unapokewa kwa imani peke (Yohana 3:16, Waefeso 2:8-9; Tito 3:5), lazima kuwe na tafsiri tofauti ya mistari hiyo. Maandiko hayajichanganyi yenyewe. Katika nyakati za Biblia, mtu ambaye alitoka dini moja hadi nyingine mara nyingi hubatizwa ili kutambua uongofu. Ubatizo ni njia ya kufanya maamuzi hadharani. Wale waliokataa kwa njia nyingine wanasema kuwa hawakuwa wameamini kwa kweli. Hivyo, katika mawazo ya mitume na wanafunzi wa mbeleni, wazo la muumini ambaye hajabatizwa ni jambo ambalo halikuwa linasikika. Wakati mtu alidai kuwa muumini katika Kristo, bado iliona haya kutangaza imani yake hadharani, ilionyesha kuwa hakuwa na imani ya kweli.

Ikiwa ubatizo ni lazima kwa wokovu, kwa nini Paulo anasema, "Nashukuru kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo" (1 Wakorintho 1:14)? Kwa nini yeye alisema, "Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali nihubiri Habari njema, wala si kwa hekima ya maneno, mslaba wa Krisot usije ukabatilika" (1 Wakorintho 1:17)? Kwa kweli, katika kifungu hiki Paulo anapingamizi dhidi ya mgawanyiko ulioikumba kanisa la Korintho. Hata hivyo, ni jinsi gani Paulo anasema, " Namshukuru kwa sababusikumbatiza…" au "Maana Kristo hakunituma ili nibatize…" kama ubatizo ulikuwa muhimu kwa ajili ya wokovu? Ikiwa ubatizo ni muhimu kwa wokovu, Paulo kwa njia nyingine angekuwa anasema, "Namshukuru kwamba kwa sababu hamkuokoka ..." na "Kwa maana Kristo hakunituma kuokoa ..." Hiyo itakuwa taarifa kinaya isiyo aminika kwa Paulo kuisema. Zaidi ya hayo, wakati Paulo anatoa muhtasari wa kina wa anavyo iona Injili (1 Wakorintho 15:1-8), kwa nini yeye anaacha kutaja ubatizo? Ikiwa ubatizo unahitajika kwa ajili ya wokovu, ni jinsi gani kuwasilisha injili kukose kutaja ubatizo?

Ubatizo wa kuzaliwa upya si dhana ya Biblia. Ubatizo hauokoi kutoka kwa dhambi lakini kutoka kwa dhamiri mbaya. Katika 1 Petro 3:21, Petro alifundisha wazi kwamba ubatizo haukuwa tendo la sherehe ya utakaso wa kimwili, bali ni ahadi kwa dhamiri njema mbele ya Mungu. Ubatizo ni ishara ya kile tayari kimetokea katika moyo na maisha ya mtu ambaye amemwamini Kristo kama mwokozi (Warumi 6:3-5, Wagalatia 3:27, Wakolosai 2:12). Ubatizo ni hatua muhimu ya utii ambayo kila Mkristo anatakiwa kuchukua. Ubatizo hawezi kuwa hitaji kwa ajili ya wokovu. Kwa kufanya hivyo ni kushambulia ule uwezo wa kifo na ufufuo wa Yesu Kristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! ubatizo ni wa muhimu kwa wokovu? Ni nini maana ya ubatizo wa kuzaliwa upya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries